Ya Lwakatare: DPP, Polisi watofautiana

[h=5]"IGP SAID MWEMA ni mwanafunzi wangu wa mwaka wa kwanza katika shule kuu ya sheria pale Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam hata yeye anajua hajanitendea haki katika hili.Kuteua kikosi cha askari wafanye upelelezi juu ya usalama wangu uliopo hatarini ambao miongoni mwao wanatuhumiwa na wameshatuhumiwa kwa majina na mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Ndug,Reginald Mengi kumtengenezea mwanae kesi bandia kwa kumuwekea madawa ya kulevya akiwa anasafiri pale uwanja wa ndege hivyo basi sina imani nao na sihitaji kuhojiwa na askari hao" maneno kama haya yalitamkwa na Dr,Harrison Mwakyembe alipotakiwa kutoa ushirikiano kwa kikosi cha askari upelelezi kilichoundwa na IGP SAID MWEMA kwaajiri ya kuchunguza usalama wake .

[/h]


 
Hahaha hii nchi bwana, yaani hapa ndio Wazungu wanapotuona vilaza.
 
Kama unajua kuwa tunatakiwa kuvuta subira, huu umbeya wako wa nini?
Hujui kuwa ulichoandika hapa ni swala la kawaida kati ya ofisi ya DPP na polisi kabla ya kufungua kesi? Kuna kipya kipi hapo?

Again,
Vuta Subira...

Mkuu hii taarifa kwangu imenifaa na naungana na wajinga wengine kutojua taratibu za hizo ofisi mbili. Naomba wewe uvute subira wakati na sisi mbulula tunajulishwa tuliyo na hamu nayo.
 
Polisi wa Tz bhana yaaani furu vituko! Kumbambikia mtu kesi inabidi kujipanga sio kizembe kama walivodhani
 
Warumi 1:28-31 Nao kwa kuwa walikataa kumkubali Mungu, Yeye akawaacha wafuate akili zao za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa.Wakiwa wamejawa na udhalimu wa kila namna, uasherati, uovu, tamaa mbaya na hila. Wamejawa na husuda, uuaji (Mwangosi, Kombe, Kolimba, nk.), ugomvi, udanganyifu (mafisadi wa meremeta,EPA,RICHMOND, nk.), hadaa na nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, wasingiziaji (Lwakatare, mkenya wa Ulimboka, nk.), wanaomchukia Mungu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno, wenye hila, wasiotii wazazi wao, wajinga,wasioamini, wasio na huruma na wakatili (Ulimboka, Kibanda, nk.).

Kwa hiyo sasa;

Matendo ya Mitume 17:30-31
Zamani wakati wa ujinga (wakati wa kufanya hayo yaliyotajwa hapo juu), Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu. Kwa kuwa ameweka siku ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu (YESU KRISTO) aliyemchagua, kwake huyo amewahakikishia watu wote kwa kumfufua Yeye kutoka kwa wafu.’’
 
Kuna sintofahamu kubwa kati ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam juu ya suala la Mkuu wa Idara ya Usalama wa CHADEMA,Winfred Lwakatare ambaye anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuandaa mipango ya kijasusi ya kudhuru watu.

Chanzo cha kuaminika toka ndani ya Ofisi ya DPP kinadai kuwa DPP amelitaka Jeshi la Polisi kukusanya ushahidi zaidi ili kuweza kumtengenezea Lwakatare makosa ya kisheria na kumsomea mashtaka kesho. Pia,amewataka Polisi kuamua,kwa kuainisha sababu mujarabu,kama Bwana Joseph Ludovick naye ashtakiwe pamoja na Lwakatare au la.

Vuta-nkuvute hiyo ilianza jana baada ya DPP na Wasaidizi wake kushinda Ofisini kuyapitia 'mafaili' ya Lwakatare na Ludovick yaliyotoka Polisi ili kujiridhisha na uchunguzi wa awali na makosa yanayoainishwa na uchunguzi huoili kuandaa Hati za Mashtaka dhidi ya Washukiwa hao.

'DPP alifika mahali haelewi kosa la kuwashtaki akina-Lwakatare kwa ushahidi uliopo.Akawataka Polisi wajiridhishe na kurudishe 'mafaili ' kwake hadi ifikapo saa kumi na mbili na nusu ya Jumatatu' kilidokeza chanzo hicho toka Ofisi za DPP

Kesho Jumatatu,Lwakatare anatarajiwa kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili. Bado haijulikani,atashtakiwa kwa mashtaka yapi hasa na kwa mujibu wa Sheria gani za nchi hii. Kesho,kutakuwa na taarifa zaidi na kamili.Tuvute subira.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
Si mchezo Tundu Lissu ameshawaambia wajipange kabla hajawameza wazima wazima chezea CDM weye jopo la wanasheria hata mahakimu uchwara wanatekenyeka masaburi!!
 
Pro-Chadema JF naona mnaamua kujifariji na kujilwaza kwa akili yenu polisi hawana kitengo cha IT kuamtia hatiana Lwakatare.
Hata kama wanacho watendaji wake watakuwa ni wale Failures na Vilaza
Nakumbuka walikuja Chuo wakati tuko Final year (UDSM) kutaka kuajiri watu kwenye hicho Kitengo, Mshahara 270,000!!!!??????
Wakaaambulia kapa, labda walienda kuwachukua Vilaza St Joseph
 
Si mchezo Tundu Lissu ameshawaambia wajipange kabla hajawameza wazima wazima chezea CDM weye jopo la wanasheria hata mahakimu uchwara wanatekenyeka masaburi!!
masaburi mpaka yanapiga makofi pwa pwa pwa.
 
Mkuu hii taarifa kwangu imenifaa na naungana na wajinga wengine kutojua taratibu za hizo ofisi mbili. Naomba wewe uvute subira wakati na sisi mbulula tunajulishwa tuliyo na hamu nayo.
mungu akupe nguvu.
 
Vuta nikuvute huna jipya...lwakatare amekamatwa na polisi kwa vitendo vyake vya uchochezi na kuandaa video inayohamasisha uvunjifu wa amani...video hiyo inaelekeza watu wakamteke mwandishi mmoja ambaye ni very very close to zitto kisha wamtese

Unauhakika ni kweli Lwakatare amefanya hivyo?Au kwa kuwa umesikia?Usitolee ushuhuda kwa kitu usichona uhakika nacho.Bado anatuhumiwa tu si mimi wala wewe wenye uhakika na alichotuhumiwa nacho.Tukumbuke akishinda kesi imekula kwenye kodi yetu tunayolipa.Na pesa atakazodai nafuu wangejenga kliniki au kununua madawati.
 
Hapana haja ya kuhamaki naamini kama kuna kosa limetendwa haki itatendeka kama kuna msukumo wa kisiasa itajulikana bila shaka yoyote tutulie tusubiri hii ngoma itamalizika vipi.
 
Ha ha haaaaaa!!!!!!!!!!. Ingelikuwa aliyekamatwa ni Ustadhi Ponda ungesema" Acha sheria ichukue mkondo wake". lakini kwa huyu muuaji na mtesaji kwa nembo ya chama unasema kabambikiwa kesi! Mungu yupo wapi hapo???
Acha sheria ifanye kazi. Pia Lwakatare anapewa maagizo na wakubwa zake. Woote wakamatwe na wahojiwe na sheria ifuate mkondo!!

Unauhakika na unachoandika.Haingii akilini kutetea kesi za kusingiziwa.Kesi ya Ponda na ya Lwakatare ni vitu viwili tofauti.Na hata huyo Ponda bado anatuhumiwa tu bado hajahukumiwa na hatusathili kumhukumu tulio nje ya hiyo mahakama.
 
huo ni umbea. nani kati yenu amewasiliana na watendaji wa polisi na kuambiwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha. ngoma ingekuwa ya kitoto hivyo jamaa angerudishwa siku ileile. leo ni siku ya ngapi yupo ndani. ondoeni uzushi wenu na kila kitu kitaWEKWA hadharani leo

Ngoja yakikufika utatafuta watu wakukupigia makelele,maana waswahili wanasema hivi"Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu................"
 
Wasalamu wana JF,

UTANGULIZI:

Makosa ya jinai hupelelezwa na polisi, na uandaaji wa mashitaka hufanywa na DPP baada ya kusoma jalada la polisi na kwa kutumia taaluma ya sheria huandaa mashitaka yanayoendana na yaliyomo kwenye jalada la polisi. Katika mchakato huu DPP asiporidhika na yaliyomo kwenye jalada la polisi kiasi cha kuandaa mashitaka, kwa malaka aliyonayo anaweza kurudisha Jalada polisi kwa upelelezi zaidi kabla ya kuandaa mashitaka.

MASHITAKA YA LWAKATARE NA MWENZAKE:

Kwa ujumla Lwakatare na mwenzake wameshitakiwa kwa kosa la ugaidi ambalo kimsingi lazima mshitakiwa awe ametenda moja ama zaidi ya matendo ya kigaidi kama yanavyoainishwa kwenye sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002. hivyo basi ili kumtuhumu au kumshitaki mtu, au taaasisi, au kampuni n.k ni busara kuainisha au kudadavua maana ya ugaidi kama ilivyoelezewa katika sheria husika. kwa bahati mbaya sheria yetu haijaelezea ugaidi ni nini bali imeeleza tendo la kigaidi ni nini("terrorist Act).


Kifungu cha tatu cha sheria tajwa kimeeleza tendo la kigaidi ni kutenda au kutotenda kwa yanayoelezwa kwenye kifungu cha nne cha sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002. kifungu cha nne kifungu kidogo cha pili ndio kimeainisha matendo yote hayo. ili kutopoteza maana naweka nakala ya kifungu ambacho kipo katika lugha ya kizungu:-

"(2) A person commits terrorist act if, with terrorist intention, does an act or omission which;
(a) may seriously damage a country or an international organization; or
(b) is intended or can reasonably be regarded as having been intended to;
(i) seriously intimidate a population;
(ii) unduly compel a Government or perform or abstain from performing any act;
(iii) seriously destabilise or destroy the fundamental political, constitutional, economic orsocial structures of country or an international organization; or
(iv) otherwise influence such Government, or international organization; or

(c) involves or causes, as the case may be
(i) attacks upon a person's life which may cause death;
(ii) attacks upon the physical integrity of a person;
(iii) kidnapping of a person,

(3) An act shall also constitute terrorism within the scope of this Act if it is an act or threat of action which;
(a) involves serious bodily harm to a person;
(b) involves serious damage to property;
(c) endangers a person's life;
(d) creates a serious risk to the health or safety of the public or a section of the public;
(e) involves the use of firearms or explosives;
.....................................................................
................................................................................."
MAKOSA YALIYOFANYIKA:

Katika kifungu cha pili maneno " does an act or omission" nimeyapigia mstari kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa hapo ndipo kosa la upelelezi lilipo na makosa ya DDP yalipofanyika. kwa busara kabisa ugaidi lazima uwe na kitendo na katika ile video ya "you tube" ni wazi kuwa Lwakatare hakuwa amefanya kitendo chochote ambacho kwa akili za mtu wa kawaida angesema kinaelekea kuwa ni ugaidi na hili linathibitika kwa michango ya wana JF ambao wengi walioamini picha ile walisema ni video ya Kupanga utekaji. kwa sheria ya kanuni ya adhabu, hiyo ingekuwa ni kosa la kula njama ya kuteka mtu.


HITIMISHO:

kwa kuwa kupitia video ya you tube hakukuwa na tendo lolote la kuteka ni dhahiri upelelezi wa polisi umefanywa vibaya na DPP alikurupuka kuandika mashitaka, kwa sababu angeweza kumshitaki lwakatare kwa sheria ya kanuni za adhabu kwa kosa la kula njama ya kuteka mtu. hata hivyo ugumu upo kwa sababu maelezo ya aliyewarekodi ni muhimu , kifaa halisi kilichorekodi ni muhimu na yeye ndio atakuwa shahidi muhimu ambaye bila yeye kesi hakuna kwani yeyote atakayetoa ushaidi atakuwa anatoa habari za kuambiwa.
 
Kwa DPP na IGP Mwema Denis Msacky ndio national na international figure ambaye amekuwa terrorised ha ha ha wanasheria endeleeni kuwaumbua mchana kweupe,sheria ya nchi haina tafsiri ya gaidi vipi Lwakatare anaitwa gaidi na jeshi la Polisi,Habarileo,Jambo leo,Uhuru na Ikulu duh hii team kweli imeharibu nchi yetu, so sad
 
Huku maofisini tupo kulipwa mishahara na posho tu na mambo ya sheria ni baada ya kuboronga ndo tunarudi kwenye makaratasi. Poleni!! Tumbo kwanza!!
 
Back
Top Bottom