Wasalamu wana JF,
UTANGULIZI:
Makosa ya jinai hupelelezwa na polisi, na uandaaji wa mashitaka hufanywa na DPP baada ya kusoma jalada la polisi na kwa kutumia taaluma ya sheria huandaa mashitaka yanayoendana na yaliyomo kwenye jalada la polisi. Katika mchakato huu DPP asiporidhika na yaliyomo kwenye jalada la polisi kiasi cha kuandaa mashitaka, kwa malaka aliyonayo anaweza kurudisha Jalada polisi kwa upelelezi zaidi kabla ya kuandaa mashitaka.
MASHITAKA YA LWAKATARE NA MWENZAKE:
Kwa ujumla Lwakatare na mwenzake wameshitakiwa kwa kosa la ugaidi ambalo kimsingi lazima mshitakiwa awe ametenda moja ama zaidi ya matendo ya kigaidi kama yanavyoainishwa kwenye sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002. hivyo basi ili kumtuhumu au kumshitaki mtu, au taaasisi, au kampuni n.k ni busara kuainisha au kudadavua maana ya ugaidi kama ilivyoelezewa katika sheria husika. kwa bahati mbaya sheria yetu haijaelezea ugaidi ni nini bali imeeleza tendo la kigaidi ni nini("terrorist Act).
Kifungu cha tatu cha sheria tajwa kimeeleza tendo la kigaidi ni kutenda au kutotenda kwa yanayoelezwa kwenye kifungu cha nne cha sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002. kifungu cha nne kifungu kidogo cha pili ndio kimeainisha matendo yote hayo. ili kutopoteza maana naweka nakala ya kifungu ambacho kipo katika lugha ya kizungu:-
"(2) A person commits terrorist act if, with terrorist intention, does an act or omission which;
(a) may seriously damage a country or an international organization; or
(b) is intended or can reasonably be regarded as having been intended to;
(i) seriously intimidate a population;
(ii) unduly compel a Government or perform or abstain from performing any act;
(iii) seriously destabilise or destroy the fundamental political, constitutional, economic orsocial structures of country or an international organization; or
(iv) otherwise influence such Government, or international organization; or
(c) involves or causes, as the case may be
(i) attacks upon a person's life which may cause death;
(ii) attacks upon the physical integrity of a person;
(iii) kidnapping of a person,
(3) An act shall also constitute terrorism within the scope of this Act if it is an act or threat of action which;
(a) involves serious bodily harm to a person;
(b) involves serious damage to property;
(c) endangers a person's life;
(d) creates a serious risk to the health or safety of the public or a section of the public;
(e) involves the use of firearms or explosives;
.....................................................................
................................................................................."
MAKOSA YALIYOFANYIKA:
Katika kifungu cha pili maneno " does an act or omission" nimeyapigia mstari kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa hapo ndipo kosa la upelelezi lilipo na makosa ya DDP yalipofanyika. kwa busara kabisa ugaidi lazima uwe na kitendo na katika ile video ya "you tube" ni wazi kuwa Lwakatare hakuwa amefanya kitendo chochote ambacho kwa akili za mtu wa kawaida angesema kinaelekea kuwa ni ugaidi na hili linathibitika kwa michango ya wana JF ambao wengi walioamini picha ile walisema ni video ya Kupanga utekaji. kwa sheria ya kanuni ya adhabu, hiyo ingekuwa ni kosa la kula njama ya kuteka mtu.
HITIMISHO:
kwa kuwa kupitia video ya you tube hakukuwa na tendo lolote la kuteka ni dhahiri upelelezi wa polisi umefanywa vibaya na DPP alikurupuka kuandika mashitaka, kwa sababu angeweza kumshitaki lwakatare kwa sheria ya kanuni za adhabu kwa kosa la kula njama ya kuteka mtu. hata hivyo ugumu upo kwa sababu maelezo ya aliyewarekodi ni muhimu , kifaa halisi kilichorekodi ni muhimu na yeye ndio atakuwa shahidi muhimu ambaye bila yeye kesi hakuna kwani yeyote atakayetoa ushaidi atakuwa anatoa habari za kuambiwa.