Ya Lwakatare: DPP, Polisi watofautiana

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kuna sintofahamu kubwa kati ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini(DPP) na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam juu ya suala la Mkuu wa Idara ya Usalama wa CHADEMA,Winfred Lwakatare ambaye anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuandaa mipango ya kijasusi ya kudhuru watu.

Chanzo cha kuaminika toka ndani ya Ofisi ya DPP kinadai kuwa DPP amelitaka Jeshi la Polisi kukusanya ushahidi zaidi ili kuweza kumtengenezea Lwakatare makosa ya kisheria na kumsomea mashtaka kesho. Pia,amewataka Polisi kuamua,kwa kuainisha sababu mujarabu,kama Bwana Joseph Ludovick naye ashtakiwe pamoja na Lwakatare au la.

Vuta-nkuvute hiyo ilianza jana baada ya DPP na Wasaidizi wake kushinda Ofisini kuyapitia 'mafaili' ya Lwakatare na Ludovick yaliyotoka Polisi ili kujiridhisha na uchunguzi wa awali na makosa yanayoainishwa na uchunguzi huoili kuandaa Hati za Mashtaka dhidi ya Washukiwa hao.

'DPP alifika mahali haelewi kosa la kuwashtaki akina-Lwakatare kwa ushahidi uliopo.Akawataka Polisi wajiridhishe na kurudishe 'mafaili ' kwake hadi ifikapo saa kumi na mbili na nusu ya Jumatatu' kilidokeza chanzo hicho toka Ofisi za DPP

Kesho Jumatatu,Lwakatare anatarajiwa kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili. Bado haijulikani,atashtakiwa kwa mashtaka yapi hasa na kwa mujibu wa Sheria gani za nchi hii. Kesho,kutakuwa na taarifa zaidi na kamili.Tuvute subira.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
 
Hapa kazi ipo.....nadhani hata mjadala wa matokeo ya kidato cha Nne itabidi yasubiri kwanza mpaka hili lipite.
 

Kesho Jumatatu,Lwakatare anatarajiwa kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili. Bado haijulikani,atashtakiwa kwa mashtaka yapi hasa na kwa mujibu wa Sheria gani za nchi hii. Kesho,kutakuwa na taarifa zaidi na kamili.Tuvute subira.
VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam

Kama unajua kuwa tunatakiwa kuvuta subira, huu umbeya wako wa nini?
Hujui kuwa ulichoandika hapa ni swala la kawaida kati ya ofisi ya DPP na polisi kabla ya kufungua kesi? Kuna kipya kipi hapo?

Again,
Vuta Subira...
 
Ile kauli inayosema.....ukweli daima hujitenga na uongo ndo hapa inapotawala. Wakijikanyaga tu waende mahakamani na ushahidi wa video ya youtube. Kazi ipo kwa polisi.
 


Kesho Jumatatu,Lwakatare anatarajiwa kupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili. Bado haijulikani,atashtakiwa kwa mashtaka yapi hasa na kwa mujibu wa Sheria gani za nchi hii. Kesho,kutakuwa na taarifa zaidi na kamili.

Ndiyo sababu wamevamia ofisi za CHADEMA Jumapili, ili wapate chochote kwa ajili ya Jumatatu?
 
Kama unajua kuwa tunatakiwa kuvuta subira, huu umbeya wako wa nini?
Hujui kuwa ulichoandika hapa ni swala la kawaida kati ya ofisi ya DPP na polisi kabla ya kufungua kesi? Kuna kipya kipi hapo?

Again,
Vuta Subira...
Labda hiyo subira mnayotaka ivutwe ni hadi lini? Kama kesho asubuhi Lwakatare anatakiwa kufikishwa mahakamani, je atashitakiwa kwa kosa gani kama hadi hivi sasa ushahidi wa kutosha kuweza kumshitaki haujapatikana? Nafikiri ndiyo maana polisi leo walikuwa ofisi za CHADEMA kujaribu kutafuta ushahidi mwingine zaidi ya ule wa video. Na inaonekana pamoja na kukamatwa kwa Ludovick bado hawajaweza kupata sababu za msingi za kuwashitaki hawa bwana.

Kukosekana kwa ushahidi mwingine zaidi ya huo wa video unaweza kuwa ni ushahidi mwingine kwamba video ni ya CCM. Kwanini wasianze uchunguzi wa kimtandao kujua aliyeupload video kwenye youtube ni nani? Naamini wakimpata aliyeupload video kwenye youtube watakuwa na uwezo wa kujua alikoitoa. Lakini hivi sasa naona kama wanatapatapa.
 
Kama unajua kuwa tunatakiwa kuvuta subira, huu umbeya wako wa nini?
Hujui kuwa ulichoandika hapa ni swala la kawaida kati ya ofisi ya DPP na
polisi kabla ya kufungua kesi? Kuna kipya kipi hapo?

Again,
Vuta Subira...

Povu la nin blaza,mlifkiria kwa kutumia masaburi matokeo yake mmeangukia ugoko!!
Kwishneey
 
Nimeongelea swala la video kutokuwa ushahidi wa kutosha katika thread ya Pasco.

Katika court of law polisi/DPP inabidi wajipange zaidi ya video.

Katika court of public opinion wengine hatuna such a lofty threshold. Tungekuwa hivyo tungeamini Chenge hana hatia.
 
Hivi jamani hawa watu hawana hofu ya Mungu!!? Unambambikizia mtu kesi kwasababu ya mambo ya kidunia tu!!?

Kesi tengenezeni, muhukumuni tu mnavotaka ila kumbukeni "DUNIANI TUNAPITA NA SIKU MOJA MACHUNGU HAYA YA LWAKATARE YATAWAGEUKIA!!"
 
Kama ccm wana mbavu, huyo aliyejitambulisha katika JF kama Bukoba boy ajitokeze mahakamani tuone!!! Kwa nini polisi waifanyie kazi anonymous video? CDM inazidi kupaa kila kukicha!!!!!!
 
Inabidi warudi studio ku-record upya!! Hiyo ya sasa hata DPP amesema imechuja!!!
 
sijawahi kuona ushahidi wa youtube ukatumika mahakamani , hii ndio kazi mpya pekee kwa jeshi la polisi, sidhani hapa wanataka kumlipa lwakatale hela tu kwa ajili ya uchaguzi T 2015 chadema
 
Kama unajua kuwa tunatakiwa kuvuta subira, huu umbeya wako wa nini?
Hujui kuwa ulichoandika hapa ni swala la kawaida kati ya ofisi ya DPP na polisi kabla ya kufungua kesi? Kuna kipya kipi hapo?

Again,
Vuta Subira...

Hivi hadi jumapili mnatakiwa muwe kazini, au nape analipa overtime kubwa?
 
Back
Top Bottom