Ya Kikwete Yamkumba Rais Magufuli

Ya Kikwete Yamkumba Rais Magufuli

Wenye fikra finyu hawezi kuona madhara ya kujiamlia mambo...sijui kama watu wanajua wanavyoibuka madikteta...kuna siku itaamrishwa kulala sa 1,kutoswali swala 5(iwe ijumaa tu) nk!ulizeni Zimbambwe,N/Korea walianzaje.Kibaya kutokana wengi wetu kukosa uelewa tumekuwa mashabiki wa kila kitu.Sasa hivi kuna ugumu sana wa maisha,hili ni kila kona.lakini watu wanalalamika kimya kimya.kuna majibu kama Kitwanga hakuna wakuuliza mbona bado yupo wakati wengine wamewekwa pembeni kwa tuhuma tu.Maono ya viongozi wetu yanaakisi pia upumbavu wetu.poor Tanzanians.Bora ningekuwa Somali ikajulikana moja kuliko kuwa sehemu ya nchi ililiojaa wapumbavu.Wasiojua kesho yao,
kazi sana kuturidhisha sisi watanzania.. kweli saa hizi kuna m.bwa mnatamani bora mngekua somalia kuliko kuwa hapa tz kweli???? ila msisahau pepo hazina sifa ila pawapo jehanam
 
Nilidhani wapinzani wangekuja na mpinu za kuonyesha uwezo na speed ya maendleo ya nchi zaidi ya Mh magufuli lakini wao wanakuja na masuala ya kupinga... Tutafiak wapi kama ndio hivyo?? mmoja ajitahidi kujenga na mwingine anajitahidi kubomoa.. Unweza ukapinga ndio lakini si lazima ukapinga kila kitu badalayake ukaonyesha njia mbadala ambayo ni nzuri zaidi.
Rudia kusoma hiyo hoja vizuri na uielewe kinachotakiwa ni taratibu za fedha zifuatwe mburula wewe
 
Sasa ukweli wa kinachoitwa 'upinzani' kinaonekana. Hawa wanataka kutuchelewesha tu. Hakuna aliyekuwa akijali vipengee hivi kama JK pamoja na maovu yote yaliyotokea mbona bunge halikuweza kumdhibiti. Haihitaji elimu kubwa kuona kwamba MAG anafanya kwa manufaa ya wananchi. Upinzani sasa ni wazi wanagombea mlo, kwani walikuwa wakinyofolewa kitu katika hivi vijisenti senti !
Kaka haya ni mambo ya kisheria, sio yanafanyika mkuu,panua Ubongo kidogo
 
Hiyo mihimili mingine ilikuwepo kabla ya majipu? Kama ndio swali ni je cha muhimu kwa wannchi ni mihimili au maedeleo?
 
Kuna baadhi ya hoja ikizileta harakaharaka hata kama zinamtetea mwanchi wa kawaida waweza pigwa mawe na huyo unayemtetea. Nashauri wapinzani wausome upepo wa kisiasa na utendaji wa kisanii wa anaina ya Magu....Wasijekuwa "a man of the people"...
 
Yule dada aliyepewa ubunge wa kupewa na unaibu spika,anajipendekeza mpaka kero!
 
HOJA nzito, uchunguzi na ufuatiliaji wa vyama vya upinzani uliokuwa unatesa utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, sasa zinaelekezwa kwa Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Rais Magufuli anakumbana na mtikisiko kutoka vyama vya upinzani ambapo sasa anakosolewa kutokana na kushindwa kutenganisha majukumu ya mihimili miwili –Bunge na Serikali-hivyo kusababisha sintofahamu.

Hatua anazochukua ikiwa ni pamoja na kuhamisha matumizi ya fedha jambo ambalo linatajwa kuingilia muhimili mwingine wa Taifa kinyume na taratibu za nchi.

Mjini Dodoma kabla ya kususa Hotuba ya Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu; Freeman Mbowe, Kiongozi wa Upinzani Bungeni amesema utawala wa sasa unavunja Katiba ya Jamhuri.

Mbowe ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni katika Ofisi ya Waziri Mkuu amesema, “kitendo cha serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.”

Amefafanua kwamba, ni Bunge la Bajeti kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio lililo na mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa Bajeti ikiwa ni kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Serikali.

“Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya serikali, kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba:

“Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa.”

Amefafanua kwamba, utaratibu huo unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka serikali kupeleka bungeni bajeti ya nyongeza kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.

Lakini utaratibu huo umekuwa ukivunjwa na Serikali ya Rais Magufuli kutokana na kufanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge na kwamba, jambo hilo linaua dhana ya madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri serikali.

Ametoa mfano kwamba, bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16 ilikuwa ni Sh. 883.8 bilioni ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni Sh. 191.6 bilioni.

“Jambo la kushangaza ni kwamba, hadi kufikia mwezi Machi 2016 wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.

“Ukitazama takwimu hizo, utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na Bunge,” amesema Mbowe.

Amesema tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyopelekwa bungeni na serikali ili kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.

Hivi karibuni Rais Magufuli amekuwa akibadili matumizi ya fedha zilizopangwa na bunge kwa ajili ya shughuli fulani na kuzipeleka kwenye kazi nyingine kinyume na utaratibu wa nchi.

Miongoni mwayo ni fedha za Sherehe za Muungano ambazo sasa zimeelekezwa kwenye upanuzi wa Barabara ya Makongoro – Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuanzia eneo la Ghana.

Fedha za Sherehe ya Uhuru ziliamriwa kuelekezwa kwenye upanuzi wa Barabara ya kutoka Mwenge kwenda Moroco jijini Dar es Salaam ambapo upanuzi huo unaendelea.
Kwani ametumia tirion 23? Pesa za sherehe,zote, oc, ziliidhinishwa na bunge na sasa zimebadilishiwa matumizi na kuwekwa kwenye maendeleo.
Hivi wewe mleta mada unamalengo gani na Tanzania? Mzalendo halisi tungebishana wapi pesa hii ipelekwe na si hivyo vioja na hekaya ulizoleta.
Tanzania itasonga mbele tu kwani wenye mapenzi mema na nchi yao wapo wengi na siku zote wema hushinda uovu.
Chadema na genge la wasiotakia mema Tanzania hawatafanikiwa kukwamisha maendeleo ya Tanzania.
 
Sasa ukweli wa kinachoitwa 'upinzani' kinaonekana. Hawa wanataka kutuchelewesha tu. Hakuna aliyekuwa akijali vipengee hivi kama JK pamoja na maovu yote yaliyotokea mbona bunge halikuweza kumdhibiti. Haihitaji elimu kubwa kuona kwamba MAG anafanya kwa manufaa ya wananchi. Upinzani sasa ni wazi wanagombea mlo, kwani walikuwa wakinyofolewa kitu katika hivi vijisenti senti !
ama kweli wewe utakuwa mwendawazimu
 
Waende wakawaambie wananchi kua Dr Magufuli anatumia fedha za wananchi kujenga barabara, na kupeleka mahospitalini Bila kupangwa na Bunge
 
majuzi kuna mwanajeshi mstaafu mmoja wa uingereza anaitwa rob lawrie alikua anafanya kazi kwenye makambi ya wakimbizi ufaransa sasa kwa kuona hali mbaya kwenye yale makambi na kwa kuepusha kifo ambacho kingetokana na baridi kali pale kambini alijaribu kumtorosha mtoto mkimbizi wa miaka minne kumpeleka kuungana na ndugu zake walioko uingereza akakamatwa na askari wa mpakani na kama akikutwa na hatia aweza kufungwa miaka mitano,, nilijisikia kumhurumia sana jaji atakaeamua hiyo kesi kwa maana kwa kumfunga jela huyo jamaa itakua ni kama kuifunga jela "HURUMA"! nachojaribu kusema ni kua hizi sheria zilitungwa na watu walioona mbali, waliotuzidi akili wengi wetu na ni kweli kabisa mwisho wa siku uhai wa huyo mtoto HAUTAKIWI kua muhimu zaidi ya hiyo sheria inayozuia kusaidia kutendeka uhamiaji haramu lakini hebu vaa viatu vya huyo jaji,, hivi akiamua amsamehe huyo mwanajeshi ni kwa kiasi gani atautia doa baya sana utawala wa sheria? lakin vipi tena akiamua kumfunga huyo mwanajeshi na akaamuru hicho kitoto kirudishwe kambini kisha siku kadhaa badae akaletewa taarifa kitoto alichoamuru kirudishwe kambini kimekufa kwa baridi kambini?? sio mfano mzuri ikiwa rais ataonekana kukiuka sheria ila binafsi namshauri wakati mwingine afumbe macho afanye kazi yake ambayo ina maslahi mapana kwa walio wengi, mwisho wa siku hawa wachache wanaopinga nao wataona matunda ya kufumba macho na kufanya maamuzi na historia itamkumbuka kwa hilo.
 
Wabunge Wa upinzani hawana nymbo....mfno zile bln 6 ambazo zimerudi serikalin wanazipigia kelele....zile pesa zilikuwa kwa ajili ya mambo yasio kuwa na msingi kama ....et matibabu ya wabunge nje ya nchi aiseee...hapa ndo nakoswa imani na mabunge ya vyama vya upinzani..halafu yanasema ety muhimili wao unaingiliwa.......aiseee Rais ikibidi hata posho zao punguza..
Hahahaaaa katika posho usijidanganye kuwa ni wapinzani ndo wanaumia wabunge wa CCM wanaumia kichinichini kimya kimya wanaogopa kusema lolote lililo kinyume na maamuzi au mipango ya serikali unafikiri zikirudishwa watapinga?? Hata wao wapo kwa maslahi yao binafsi wanasubiri waunge mkono hoja zote ili kulinda kitumbua. Acheni kuwa myopic
 
Rudia kusoma hiyo hoja vizuri na uielewe kinachotakiwa ni taratibu za fedha zifuatwe mburula wewe
Hivi matusi ya nini????Niliutukana au???
Sasa tusi lina rudi kwako, tena na zaidi ya tusi kwamba.. Anyway wala sintakutukana... Aliyekua mjingia usimuigizie lasivyo na wewe unakua mjinga...
 
Hahahaaaa katika posho usijidanganye kuwa ni wapinzani ndo wanaumia wabunge wa CCM wanaumia kichinichini kimya kimya wanaogopa kusema lolote lililo kinyume na maamuzi au mipango ya serikali unafikiri zikirudishwa watapinga?? Hata wao wapo kwa maslahi yao binafsi wanasubiri waunge mkono hoja zote ili kulinda kitumbua. Acheni kuwa myopic
Ndo mwisho wako Wa kufikiri¿??huo
Mi unajua wabunge Wa upinzani ndio wanaumia zaidi
 
Hapa namsifu sana Mh Mbowe kwa kunukuu vifungu vya katiba na sheria vilivyovunjwa. Nilisikitika na ninaendelea kusikitika kuwa wakati yeye Mbowe na wenzaka wakimtaka Rais wa JMT JPM aingilie Zanzibar baada ya uchaguzi wa Oktoba hawakunukuu hata tone la kifungu cha katiba wala sheria inayomruhusu rais wa JMT kuingilia uchaguzi wa Zbar ambao kikatiba imeorodheshwa mioingoni mambo ya ndani ya Zenji.
hapo waliteleza lakini hii nchi watawala ni wababe, utanukuu viftungu weee hakuna anaekuskia.
 
Bunge hili la sasa ni chombo cha serikali

mimi nilipomuona naibu spika akimpa Magufuli cheki ya pesa eti wamebana matumizi
nilijiuliza maswali kibao
body language yake tu ilikuwa kama vile ameenda kumuona boss wake

Huyu tunaambiwa ndo mwalimu wa sheria na katiba lakini hajui umuhimu wa uhuru wa bunge kwenye maamuzi...

Naheshimu sana maoni yako the Boss. Na najua fika unapigania utawala wa sheria. Katika hili sipingani nawe. Ila napenda ukunjue fikra zaidi uone kuwa katika Ulimwengu wetu wa tatu, kamwe hakuna Bunge huru 100%. Na itaendelea kuwa hivyo mpaka hapo wengi watakapokuwa economically independent au hakuna kitu kama abject poverty. Nadhani vitu hivi vinakwenda sambamba. Katika nchi ambayo watu ni wahitaji kiasi wanaweza kuuza uhuru wao, usitegemee bunge huru. Ni vizuri kukemea excesses za Maghufuli, lakini tusiwe extremists katika hilo. Kwani hakuna wakati wowote bunge letu halikuvutwa mashavu na wanasiasa. Ni vibaya sana wakati tumepata mwanasiasa mwenye utashi wa kuondoa umaskini na aliye honest kupigana na ufisadi.....tukaanza kumshughulisha na vita vya pambizoni.
 
Haitawasaidia kitu kwa sababu taifa lote lipo na Magufuli[/QU
  • Rais ana uwezo wa kufuta vyama vya upinzani. Nataka afanye hivyo na itakuwa bora kwa nyinyi mnaoumia kuona upinzani unasema kitu. Tuliishi bila vyama toka uhuru mpaka 1995 sasa kwanini tusirudi huko? Wewe mwana CCM umefaidika nini na vyama vingi zaidi ya kujifunza matusi ya kuwatumia upinzani?
TZ bado ni koloni la communisium hivyo vyama vingi ni ndoto. Endelea vvama china na cuba ila waulize wenzio mistari ya kununua vitu mtaikumbuka? tulifanya sisi late 80 na early 90's kwetu marudio je nyinyi kizazi kipya mtaweza?viva mabadiliko!!!!!!
 
Maamuzi mpaka ya Bunge yanafanywa na mtu moja au wawili alafu unayabariki?
Kama yana faida basi tunayakubali. Tena itakua bora zaidi kama hata hawa wabunge wangekaa nyumbani na bunge lifungwe kabisa. Hii itapunguza gharama na nchi itaendelea
 
Mimi niliwaambia mbona kuna mwingiliano wa kazi kwenye mihimili,rais anaingilia mihimili mingine kuanzia siku ile ktk sherehe za majaji,ikaja bunge,watu wakasema kwa jins tulipofikia inabid iwe hivyo!kama watu wanashangilia haya basi kuna haja ya kufanya marekebisho,utaratibu uliowekwa ukikiukwa huko mbele madhara yapo.
 
Back
Top Bottom