Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
- Thread starter
- #21
Usichoelewa hapo ni niniHapo kwenye red tatizo hapa ni kiswahili hakieleweki au ndio ukishazoea kuongopa unajikuta unajiongopea hata mwenyewe
Usichoelewa hapo ni niniHapo kwenye red tatizo hapa ni kiswahili hakieleweki au ndio ukishazoea kuongopa unajikuta unajiongopea hata mwenyewe
Watanzani hawataki amizukaHaitawasaidia kitu kwa sababu taifa lote lipo na Magufuli
Sasa ukweli wa kinachoitwa 'upinzani' kinaonekana. Hawa wanataka kutuchelewesha tu. Hakuna aliyekuwa akijali vipengee hivi kama JK pamoja na maovu yote yaliyotokea mbona bunge halikuweza kumdhibiti. Haihitaji elimu kubwa kuona kwamba MAG anafanya kwa manufaa ya wananchi. Upinzani sasa ni wazi wanagombea mlo, kwani walikuwa wakinyofolewa kitu katika hivi vijisenti senti !
Maendeleo yasiyofuata sheria ni yapi hayoLakini hata kama anaingilia si tunataka maendeleo...
Mpaka sasa performance rate ya Magufuli ni kati ya 28-35 % hakuna mtu anamuonea wivu mtu aliyeanza kwa kushindwa na kutumia udictator anatakiwa kuimprove alipopakuta sio kuuwa na kurudisha nyuma bandari mizigo haiji, reli inafanya kazi mara moja kwa wiki, makusanyo ya kodi static tangu mwanzao contrast haijaongezwa wivu gani aonewe he has to check his house vinginevyo ana kazi sana aiseeWana wivu wa kike. Mafanikio ya Magufuli ni kifo cha upinzani
Kama nyie mlivyoonekana kwa Watanzania kua ni niwamizuka tuWapinzani sasa wameonekana kwa wananchi na hata kwa mataifa ya nje kuwa NI wasaka TONGE!!!
Queen Esther
failures ndivyo walivyo wananchi wanasema asilimia 80 kwa hiyo ni wapinzani Magufuli anawashauri wenye maono finyu sana kama ndio hivi pole yakeWapinzani sasa wameonekana kwa wananchi na hata kwa mataifa ya nje kuwa NI wasaka TONGE!!!
Queen Esther
Tanzania ya viwanda = Mzuka fullMpaka sasa performance rate ya Magufuli ni kati ya 28-35 % hakuna mtu anamuonea wivu mtu aliyeanza kwa kushindwa na kutumia udictator anatakiwa kuimprove alipopakuta sio kuuwa na kurudisha nyuma bandari mizigo haiji, reli inafanya kazi mara moja kwa wiki, makusanyo ya kodi static tangu mwanzao contrast haijaongezwa wivu gani aonewe he has to check his house vinginevyo ana kazi sana aisee
Kama kupambana na mafisadi na kuelekeza fedha za anasa kwenye shughuli za maendeleo ni kuvunja sheria, bora rais wetu aendelee tu kuzivunja kwani zina manufaa kwa taifa
Maendeleo yasiyofuata sheria ni yapi hayo
Kiongozi yeyote anayeshindwa kufuata simple rules regulations and principles hafai hata kuongezewa siku anaendesha nchi hana hata mipango ya kuongoza wizara zake what a loss tunakazi another lost decade ndio hii huyu ataupigisha mark time kwa kujifanyia mambo ya vichororni kuyaleta kwenye utawala wake tutagota kulikoMbunge wa Viti Maalumu, Lucia Mlowe alisema moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia Serikali, lakini anashangaa kuona yenyewe ikilisimamia Bunge katika mambo mbalimbali.
Alisema hata suala la Rais kuhamisha fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe ya Muungano, ni kuingilia madaraka ya Bunge, kwa sababu fedha hizo tayari zilikuwa zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo.
“Naomba kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalamu hapa, Rais ana mamlaka gani ya kuhamisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya jambo fulani? Pia, ni namna gani wabunge tunaweza kuisimamia Serikali kama hamna uwiano kati ya mihimili hii mitatu,” alihoji mbunge huyo.
Akijibu hoja hizo, Dk Semboja alisema Sheria ya Bajeti ya 2015, inampa mamlaka Rais kupeleka fedha katika eneo analoona inafaa.
Alisema sheria hiyo inatoa sharti moja, kwamba Rais kupitia Waziri wa Fedha, atatoa taarifa bungeni juu ya matumizi ya fedha hizo.
Dk Semboja alisema mamlaka hayo yanatambuliwa pia katika Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hivyo Rais hajakosea kuhamisha fedha hizo kwenda kujenga barabara isipokuwa taarifa ya matumizi itolewe bungeni hata kama matumizi yanaonekana.
“Bunge lazima lifahamishwe kuhusu matumizi ya fedha hizo.Kama ni udhaifu wa kipengele hiki, basi unaanzia kwenye Katiba,” alisema Dk Semboja.
Kitu kibaya kwa binadamu wa leo nimizuka sasa hapo ndio umetoa wazo?NI kweli Lizaboni
Avunje tu Hanna namna!! Madawati ni muhimu kuliko Safari za Mbowe Dubai na wale wabunge wake Viti maalum.
Queen Esther
Mbowe hakuzaliwa kwenye vibanda vya nyasi wala hakujifunzia kuvaa viatu na nguo za ndani baada ya kufika chuo kikuu baba yake ndio alikuwa anampa Nyerere suti na nauli ya kwenda UN itakuwa yeye kwenda Dubai you must be jocking maskini nyie, ndio maanaa munataka kuturudisha nyuma tuanze kuvaa suruali za viraka kwa kisingizio cha watu maskini CCM imetawala miaka yote hiyo kwa nini hakuwezesha shule kuwa na madawati achene porojoNI kweli Lizaboni
Avunje tu Hanna namna!! Madawati ni muhimu kuliko Safari za Mbowe Dubai na wale wabunge wake Viti maalum.
Queen Esther
Tanzania ya viwanda = Mzuka full
Wabunge Wa upinzani hawana nymbo....mfno zile bln 6 ambazo zimerudi serikalin wanazipigia kelele....zile pesa zilikuwa kwa ajili ya mambo yasio kuwa na msingi kama ....et matibabu ya wabunge nje ya nchi aiseee...hapa ndo nakoswa imani na mabunge ya vyama vya upinzani..halafu yanasema ety muhimili wao unaingiliwa.......aiseee Rais ikibidi hata posho zao punguza..Maendeleo yasiyofuata sheria ni yapi hayo
Asilimia kubwa ya wadanganyika ni misukule kabisa, yan ni watu wasiojua wanataka kuachieve nini hasa, tena sample space kubwa iko humu jf.
HOJA nzito, uchunguzi na ufuatiliaji wa vyama vya upinzani uliokuwa unatesa utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, sasa zinaelekezwa kwa Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.
Rais Magufuli anakumbana na mtikisiko kutoka vyama vya upinzani ambapo sasa anakosolewa kutokana na kushindwa kutenganisha majukumu ya mihimili miwili –Bunge na Serikali-hivyo kusababisha sintofahamu.
Hatua anazochukua ikiwa ni pamoja na kuhamisha matumizi ya fedha jambo ambalo linatajwa kuingilia muhimili mwingine wa Taifa kinyume na taratibu za nchi.
Mjini Dodoma kabla ya kususa Hotuba ya Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu; Freeman Mbowe, Kiongozi wa Upinzani Bungeni amesema utawala wa sasa unavunja Katiba ya Jamhuri.
Mbowe ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni katika Ofisi ya Waziri Mkuu amesema, “kitendo cha serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.”
Amefafanua kwamba, ni Bunge la Bajeti kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio lililo na mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa Bajeti ikiwa ni kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Serikali.
“Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya serikali, kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba:
“Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa.”
Amefafanua kwamba, utaratibu huo unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka serikali kupeleka bungeni bajeti ya nyongeza kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.
Lakini utaratibu huo umekuwa ukivunjwa na Serikali ya Rais Magufuli kutokana na kufanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge na kwamba, jambo hilo linaua dhana ya madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri serikali.
Ametoa mfano kwamba, bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16 ilikuwa ni Sh. 883.8 bilioni ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni Sh. 191.6 bilioni.
“Jambo la kushangaza ni kwamba, hadi kufikia mwezi Machi 2016 wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.
“Ukitazama takwimu hizo, utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na Bunge,” amesema Mbowe.
Amesema tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyopelekwa bungeni na serikali ili kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.
Hivi karibuni Rais Magufuli amekuwa akibadili matumizi ya fedha zilizopangwa na bunge kwa ajili ya shughuli fulani na kuzipeleka kwenye kazi nyingine kinyume na utaratibu wa nchi.
Miongoni mwayo ni fedha za Sherehe za Muungano ambazo sasa zimeelekezwa kwenye upanuzi wa Barabara ya Makongoro – Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuanzia eneo la Ghana.
Fedha za Sherehe ya Uhuru ziliamriwa kuelekezwa kwenye upanuzi wa Barabara ya kutoka Mwenge kwenda Moroco jijini Dar es Salaam ambapo upanuzi huo unaendelea.