Ya Kikwete Yamkumba Rais Magufuli

Ya Kikwete Yamkumba Rais Magufuli

acha kijiparura nipo hapa kwa minajiri ya kujibu hoja tumesema Magufuli haiheshimu sheria ya bajeti ya mwaka 2015 na haeheshimu sheria ya fedha za umma ya mwaka 2015 MAGUFULI NI JIPU anapaswa kutumbuliwa kwa kukiuka sheria hizi muhimu katika kutuletea maendeleo ya nchi kipi usichokielewa wewe nyie ndio munamjaza pumzi hewa huyo mtu wenu mwambieni kwamba kinga yake yakutokushitakiwa isimfanye akawa dictator na mvunjaji wa sheria maana hata seriklali yake ni serikali magumashi haijawa gazetted hijatangazwa kwenye gazeti la serikali wala hajatengeneza mwongozo,wa kuongoza wizara ambazo ndio zinatekeleza matumizi ya fedha

Ok, sheria ya fedha za umma ya mwaka 2015, good. Furahia jioni yako. Kwakwakwakwakwa!
 
Leo ndio nimejiona nyumbu kabisa! Sitarudia tena kuzungusha mikono, hawa ndio niliwapa kura yangu? Mbowe unaona bora safari za kamati za bunge kuliko madawati?
Haukuwa nyumbu kabla wala baada
Ila hoja yako ina mashiko kua mboe anaona ni bora safarivza dubai kwenye ngono kuliko shughuri za kimaendeleo
 
Mimi nawachukia sana hawa wanaojali sana processes (utaratibu) kuliko achievements. Wengi wao utakuta wanapenda kuendeleza uvivu, uzembe, rushwa na ufujaji. MAGU ndiye mtu tunayemhitaji as long as haamuru kuminywa mapu..u kwa wapinzani!
Kama wewe mkuu umeshawahi kuajiriwa serikalini, jaribu au mwambie ndugu yako afanye hicho unachoita Achievement ukiwa mtumishi au kiongozi mwadimizi wa serikali, kama hutanyea ndoo Segerea!
Kazi za serikali zina miiko yake, usichukulie kiurahisi rahisi tu, utakuja kusababisha wenzako wafungwe.

Ama hayo mengine siwez kuchangia, ila nilitaka kuweka kumbukumbu sawa isije hayo uliyoandika ukawaponza wenzako!
 
Mimi nawachukia sana hawa wanaojali sana processes (utaratibu) kuliko achievements. Wengi wao utakuta wanapenda kuendeleza uvivu, uzembe, rushwa na ufujaji. MAGU ndiye mtu tunayemhitaji as long as haamuru kuminywa mapu..u kwa wapinzani!

Kama taratibu hamzitaki mliziweka za nini?
 
Kujijenga katika uongo hakutamfikisha mtu yeyote popote. Yeyote mwenye kumfahamu mwanahabarihuru amshauri ki utu uzimaili asije akaharibikiwa mbeleni.Kama kuna watu wana mpa ajenda awaambie tu wampe mambo yenye ukweli.Mbona mambo ya kukosoa yaukweli yapo mengi mengi mengi kupitiliza. Hata angekosoakutokuwapo chombo cha kusimamia utekelezaji wa bajeti au hata angekosoa sheria inayompa mamlaka waziri wa fedha 'ku violate' maamuzi ya bunge. Mambo ya ukweli na ya maana yapo mengi na si hutu tu ajenda twa wanasiasa wakware.
 
Mimi nawachukia sana hawa wanaojali sana processes (utaratibu) kuliko achievements. Wengi wao utakuta wanapenda kuendeleza uvivu, uzembe, rushwa na ufujaji. MAGU ndiye mtu tunayemhitaji as long as haamuru kuminywa mapu..u kwa wapinzani!
Kwa yeyote mwenye uelewa akisoma tu mchango wa yeyote anaweza kujua uwezo wake wa uelewa,ufuata mkumbo,ukereketwa usio na manufaa n.k.Wewe bila kukapua macho au kujiuliza sana ni kiongozi wa hao.Tangu lini upinzani au watendaji wake wakanufaika na ukwapuaji wa mafisadi wa chama tawala ilihali wao hawateuliwi kwenye nafasi za uongozi wa nchi?Sawa mnampenda Magufuli kwa tendaji wake ila hamjamchagua ninyi peke yenu.Ana kura za upinzani na wasio na chama na ni raisi wa wote.Mch. Msigwa alipokua anasifia utendaji wa raisi Magufuli yeye ni wa ccm?Aliekwambia wapinzani hawaridhiki na utendaji wa raisi ni nani?Ila lazima aongoze kwa kufuata sheria na katiba au hata hilo hulielewi au unafikiri yeye yuko juu ya sheria na katiba ya nchi?Kwa awezo na uelewa wako hili jukwaa umekosea njia jaribu mengine na yapo mengi na ya udaku ndio hayo hayo ya mipasho.
 
Acha bhange wewe Chato huwezi kupalinganisha na Monduli wala huko Hai, Niambie kidogo tu ndiyo mfano wa mapungufu ya watu wako uliowaamini Monduli ni wilaya ya miaka mingi sana kabla ya chato lakini kuna njaa elimu na maji ni shida japokuwa mbunge wake amekuwa waziri wa maji, ardhi, na hatimaye waziri mkuu hata traffic light hakuna ila chato zipo huko hai ndiyo sisemi kabisa tabu kwenda mbele japokuwa mbunge wa huko anatamba kujua sheria na katiba sijui amewasaidia nini wanachi wa huko Mungu atahukumu ukweli na unafiki.







Tuwe wakweli,hivi zile traffic light pale Chato zimewekwa kwa kazi gani haswa?Hakukuwa na sababu za kuweka traffic light eneo ambalo zinaweza kupita hadi dk 20 bila kuona gari likipita hapo.Hata hivyo taa hizo haziwezi kuwa kitu cha kujivunia,Wilaya ya Chato kama zilivyo wilaya nyingine,ni moja ya wilaya zilizo na umaskini wa kutupwa.

Ukiiacha chato mjini ambako mh.amejitahidi kuwekeza kwa kujenga nyumba za wageni,mahiteli na bar,maeneo mengine ya wilaya hiyo yapo duni sana.Wakazi wengi wa wilaya ya Chato wanajishughulisha zaidi na Kilimo pamoja na uvuvi wa samaki katika mwambao wa Ziwa Victoria.Vijiji kama Bwanga,Bukiriguru,Busaka,Makurugusi,Nyakato,Musasa,Mabira,Buzirayombo,Kankanshe,Muganza,Nyabugera na maeneo yote yanayouzunguka meambao wa Ziwa,wakazi wake ni watu duni ambao kamwe hawawezi kujivunia uwepo wa Traffic light kama suluhisho la matatizo ya kiuchumi waliyonayo.

Unaonekana ni mtu unayeongozwa na mizuka zaidi kuliko uhalisia,kama wewe ni mwana Chato,ulipaswa kuguswa na hali duni ya maisha waliyinayo wanachato kuliko kushangilia mambo madogo ambayo hayajawahi kuwa suluhisho kwa wakazi wa Chato.

Au mwenzetu hujuwi uwekezaji wa mkubwa pale Chato?Unafikiri ni watu wa kawaida waliowekeza pale Chato?Pole sana.Wana Chato watabaki kujivunia "urahisi" wa mukulu tu,zaidi ya hapo watatakiwa wajikite zaidi katika Kilimo na uvuvi ili wapate mkate wao,kitu pekee ambacho wanaweza kukipata bure japo ni kwa msimu ni T-shirt,kofia,kanga na chumvi toka ccm.Kujivunia traffic light ni upumbavu wa kiwango kikubwa kinachoweza kutweza weledi wa jukwaa hili.Jaribu kuuficha upumbavu wako.

Je,mwananchi wa Chato anayekula kwa kukamata kambale kwenye majaruba ya mpunga wanaweza kujisifia eneo hili?



IMG-20160417-WA0033.jpg




Au anahisa kiasi gani kwenye hotel ile iliyo pembezoni mwa jengo la halmashauri ya wilaya ya Chato?Acha kujisifia upumbavu,tajili na Mali zake,maskini na watoto wake,kukaa kijiweni kutwa nzima kujisifia ukwasi wa wakubwa ni upumbavu zaidi ya upumbavu wenyewe,au nawe ni miongoni wa wale vijana wanaochunga ng'ombe na farasi wa mheshimiwa? Maana wachungaji wale wanaishi ghorofani,yawezekana kitendo cha kuishi ghorofani na kutunza mifugo ya mzee kimekufanya nawe ujihesabie haki kuwa na wewe ni mwana wa mfalme.

Acha mahaba ya kipumbavu,jaribu kuwa na huruma ya kiutu,jenga hoja zako kwa kuzingatia mazingira yako(Chato),usijenge hoja kwa kuegemea kwa jirani yako,vya jirani siyo vyako.
 
Ila mwisho wa siku wananchi warahisishiwe maisha......mengine porojo
 
Sasa ukweli wa kinachoitwa 'upinzani' kinaonekana. Hawa wanataka kutuchelewesha tu. Hakuna aliyekuwa akijali vipengee hivi kama JK pamoja na maovu yote yaliyotokea mbona bunge halikuweza kumdhibiti. Haihitaji elimu kubwa kuona kwamba MAG anafanya kwa manufaa ya wananchi. Upinzani sasa ni wazi wanagombea mlo, kwani walikuwa wakinyofolewa kitu katika hivi vijisenti senti !
Basi itangazwe kuwa kwa kipindi cha magu katiba inawekwa pembeni yeye awe kila kitu! Acheni kulea na kutetea upuuzi na udikteta
 
Haitawasaidia kitu kwa sababu taifa lote lipo na Magufuli
Sii taifa lote sema mbumbumbu WA taifa ambao kwa bahati mbaya Ni wengi Sana Wako Nate hats hawako tayari kuona ukweli mweupe
 
Mbona hausemi sheria gani zimekiukwa, unabaki kusema tu kakiuka sheria? Wewe hio sheria unazijua au unaishia kuambiwa tu wanasiasa? unawaamini vipi wanasiasa waliowahi kukuambia huyu ni fisadi na wakaitoalist of shame halafu wanasiasa wale wale leo wako na wale waliowataja kwenye list of shame huku waki wa endorse na kuwasifia nchi nzima? Usimtegemee mwanasiasa kukwambia ukweli.Utafute ukweli. Sheria zipo kwa kingereza na kiswahili. Jisomee sheria ya fedha za umma ya mwaka 2001,soma katiba,hautapata tabu kujua nani mkweli na nani laghai.Usiamini kuwa unajua, tafuta maarifa zaidi.
Kwahiyo mizuka ni sahihi kwako
 
Hapa ndipo ninapowaona wapinzani ni wajinga. Hivi kwao sherehe za uhuru ni bora zaidi kuliko Ujenzi wa Barabara ya Mwenge to Morocco? Hivi tuna wapinzani wa aina gani katika nchi hii kiasi ambacho wanapinga hata hatua nzuri Inazochukuliwa na serikali. Najua inawauma sana kuona ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea kwa kasi na soon itafunguliwa. Poleni sana

Inaonyesha wazi kwamba wapinzani shida Yao ni kupata furasa ya kuitawala nchi, bila kujali shida ya wananchi. Ingawa Magufuli anajitahidi kusaidia wananchi wa hili ya chini na dnio tunayoihitaji
Tanzania ya viwanda = Mzuka full

Kwahiyo ulidhani viwanda vinajengwa kwa siku au mwezi, tena isitoshe penye mafisadi na wa kwepa kodi...... Ndio maana waafrika ni rahisi kuwapa silaha na kuana, na ndio tunavyo ona vita kila kona ya bara la afrika... kwa sababu ya akili fupi ya kufikria...
 
Hizo sheria ziendelee tu kuvunjwa mana hakuna namna kama unaona kufanya sherehee ni bora kuliko madawa na vitanda muhimbili ,magu vunja tu ....mnataka bunge live kwani press conférence ile...pale ni sehemu ya kazi...pumbavu kabisa hawa wazungusha mikono
 
wewe nawe unaweza sema nini kupakata wanaume wenzako na umbeya ndio unakupa vyeo nakusha kwenye mitandao magari unayotumia ofisi unazotumia za walipa kodi kwani ni mali ya mama yako acha ujinga wewe mpenda misifa hafiki mbali kasha anza kulia lia kila siku mara muniombee tumuombee alivyomba kazi hakujua kuna ugumu mara ooh kuna wanaonipinga hakujuwa nchi ina wananchi milioni hamsini wana maoni yao mara huu wananisema alidhani nchi kakodishia kanga aache mara moja afuata sheia za nchi na wewe uacha kuchongea watu
Pumba kabisa,watu wengine sijui mnatumia nini kufikiri. .....
 
Hizo sheria ziendelee tu kuvunjwa mana hakuna namna kama unaona kufanya sherehee ni bora kuliko madawa na vitanda muhimbili ,magu vunja tu ....mnataka bunge live kwani press conférence ile...pale ni sehemu ya kazi...pumbavu kabisa hawa wazungusha mikono








Nafikiri bora mzungusha mikono kuliko wewe unayewazungushia wenzako kiuno.


10366327_585072384927714_8479812993842761565_n.jpg
 
Back
Top Bottom