Kabla ya yote tuonyeshe huo uhakika umeupatia wapi.
Tuwekee reference na sio kutaka tuamini kauli yako kuwa ni ya ukweli usio shaka.
Hakuna katika mji wowote ule ambao watu watu wachache katika ofisi ya mipango miji wanaowaamulia wateja mionekano ya majengo yao.
Kwa sababu, kwanza hiyo ni sawa na kuingilia watu uhuru wao wa kujieleza (yes, majengo ni moja ya njia ya kujieleza). (Linganisha na: jee ni haki kwa Wizara ya Ustawi wa Jamii kutuamulia wakazi wa Tanzania namna ya kuonekana kwenye mipangilio ya mavazi yetu ya kila siku?)
Pia, watu wa mipangomiji wanaelewa kuwa miji inaevolve na kile kisichokubalika sasa kimuonekano kinaweza kuonekana kizuri katika siku za usoni. Hilo lishathibishwa na ujenzi wa yale majengo yanayoitwa modern.
Kwa hiyo kinachofanyika ni kufuata kanuni za ujenzi kwenye masuala ya uimara na usalama pamoja na zoning. Uzuri wa nje wa jengo hauwezi kuwa kazi ya mipango miji kwa sababu mbali na sababu nilizozitaja hapo kabla, beauty ni subjective. Kama kikundi cha watu mmoja hadi sita huko Wizara ya Ujenzi kinadhani jengo baya, pengine kuwa watu zaidi ya milioni wanaodhani ni zuri.
Kama upo katika mtaa ambao umepewa hadhi ya heritage, watakulazimisha muonekano wake uwe unaendana na usanifu wa enzi za majengo yaliyozunguka, lakini si vyenginevyo
Ningependa nikutanabahishe kuwa majengo ya aina hiyo unayoyalalamikia yamejaa tele katika majiji ya nchi zilizoendea
Hizi ni shopping malls zilizopo Japan na Marekani. Hayo majengo yanatofauti gani kwa nje na hilo la Bagamoyo Road?