kuna watu hapa wanadai kuwa shirika limejaa wachaga kwasababu wao ati wamesoma sana, huo ni UONGO wa hali ya juu.. nitaeleza.. katika shirika la world vision majority wa staff wake ni jamaa wanaitwa CRS (mwaka 2012 walibadilishwa jina na kuitwa DA, na kuanzia Oct 1, 2013 wameanza kuitwa SPF) hawa jamaa (CRS/DA) kabla ya octoba mwaka jana karibia wote walikuwa ni form VI leavers!!! Walikuwepo mmoja mmoja wa kuokoteza ndio walikuwa form six, na wengine wana certificate!! Waratibu wa miradi na baadhi ya PF ( project facilitator) ndio walikuwa na shahada! Lakini DA's/CRS karibia wote hawakuwa hata na diploma (hapa tunaongelea zaidi ya wafanyakazi 1500 tanzania nzima)! Ni mwaka jana tu hapa octoba ndio wamebadilisha hiyo tittle na kuiita SPF (sponsorship and project facilitator) na wakaweka sharti muombaji awe na angalau diploma! Lakini miaka yote hawa jamaa walikuwa ni form VI leavers tena wale waliokosa nafasi za kwenda advanced level!! Sasa ninyi wenzetu: mnaopiga kelele kuwa wachaga ni wasomi ndio maana wamejaa World: Vision, mnataka kutuambia kuwa hakuna WALUGURU waliomaliza form VI mpaka mchukue form VI wa arusha muwapeleke Morogoro, inamaana hakuna WAHA Waliomaliza form 4 mpaka mpeleke wachaga kigoma, hakuna wazigua wenye form 4 pale korogwe na lushoto na korogwe????
Cha kushangaza zaidi kuna ADP moja pale Morogoro cluster office, ambapo wameajiri Office attendant (mfagiaji) mchaga kutoka arusha huyu dada anaitwa Matilda! Inamaana waluguru na wapogoro hawajui kufagia!!! Unaweza kusema hii ni coincidence?????