Uadilfu ni sifa ya kwanza katika taifa kwani bila uadilifu hakuna haki kwa wasio kwenye network hasahasa wananchi wa kawaida ambao ndio wengi katika taifa,
Unapomweka kiongoz wa nchi ambaye ndio mkuu wa taifa akiwa mtuhumiwa mkuu wa kutokuwa na uadilifu, unapelekea taifa zima kuangamia kwani watendaji wa serikali na hata taasisi za uma watafanya aliyofanya mkuu wa nchi kwani hamna wa kumfunga mwenzake kengengele, kama mkuu wa nchi alifanya vitendo visivyo vya uadilifu, sembuse mtu wa kawaida atashindwa kufanya kama aliyofanya mkuu wa nchi?????
hivyo basi ili kuondoa ubinafsi wa kujilimbilizia mali, rushwa, na utendaji wa haki katika taifa,ni vizuri tukapata kiongozi mwadilifu ili awe mfano wa kuigwa kwa wananchi wake, pia atakuwa na uwezo wa kukemea maovu katika jamii kwani atakuwa na ujasiri kwa sababu sio miongoni, hivyo basi wananchi waelewe kuwa kiongozi ni kio cha jamiii, kama kiongo mkuu katika taifa ni mchafu hata wananchi hasahass watendaji wa serikali ni rahis kufanya uchafu,
ni heri kiongozi wa taifa kutuhumiwa kuuuwa kuliko kutuhimiwa kutokuwa mwadilifu kwani uadilifu ndio sifa ya kwanza ya kiongoz wa nchi,
ukiwa mwadilifu utatenda haki kwa kila mtu, utakuwa mzalendo na taifa lako,