Wizi wa Fastjet, TCAA mpo kweli?

Wizi wa Fastjet, TCAA mpo kweli?

Nairobian

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
873
Reaction score
2,282
Leo asubuhi nikielekea Mwanza, nimekutana na kisa cha ajabu sana na Fastjet.

Kuna mtoto mdogo wa kiume miaka kama 14 aliyekuwa wa mwisho kwenye foleni kwenye check in kuelekea Mwanza. Ilipofika zamu yake, akafungiwa kwamba muda umepita. Huyu mtoto hakuelewa cha kufanya na kukosa ndege.

Matokeo yake kaambiwa aende kwenye desk iliyopo nyuma ya check in desks. Mbaya zaidi pale pia akaambiwa atoke nje ya Geti akabadilishe ticket. Kwa vile nilikuwa na muda, nililazimika kutoka naye nje. Huko nje pia kaambiwa alipie Tsh. 300,000. Kwa kipi, nilishindwa kuelewa kusema kweli.

Hii nchi inaendeshwa kana kwamba hakuna sheria. Mtu unanunua ticket kwa Shillingi 130,000 lakini hawajali, wana kuambia ulipie karibia mara tatu? TCAA na Ndugu Suleiman nadhani wamelala au kama wako macho, wameyafumbia macho haya.

Watanzania hii ya Fastjet tulipiganie. Huu ni wizi wa mchana kweupe!
 
Kama genuinely amechelewa huo ndio utaratibu. Lakini unaiomba serikali ipi ukusaidie? Unajua nikigogo gani yupo nyuma ya fastjet? au kwavile unaona viongozi wake wazungu basi unadhani niyakigeni hii kampuni? Utapiga kelelee buree wanakuangalia tu maana nchi ishatekwa nakundi lawanyang`anyi mnapoona wabunge wa ukawa wakipiga kelele bungeni kuwa serikali imetekwa, uongozi ni dhaifu, Katiba pendekezwa namajanga, ccm haifai mnaona niwasaka tonge nawana njaa. Hii ichi ina wenye nchi ambao washaweka mizizi ya mirija yao wanakamua tu maziwa ... Ata uyo Magufuli haujui moto wao. Msidhani wapo silent maana wanauwezo haswa! Haya
 
Kama mnaweza kujustify hiyo scenario, wasiliana na TCAA-CCC. Ofisi zao ziko PPF tower, hawa ndo wanahusika moja kwa moja na kumlinda mlaji wa huduma za anga. Otherwise poleni sana wakuu.
 
Mwakyembe mwenyewe alikuja namkwara wakufufua Air Tanzania ...aliishiabwapi?, tafakali haya wakati unakula supu ya sato apo Mwanza!
 
Wewe ni mwongo.Haiwezekani mtu akiwa kwenye foleni akaambiwa muda umeisha.
What if check in Clerk alikuwa too slow katika kazi yake?

Hilo unalolisema halipo.As long as upo kwenye mstari, au umeikuta foleni ni lazima ucheck in.

Usitake kutufanya wote humu wajinga.
 
Nyuma ya huyo dogo wa 14 yrs kulikuwa na watu? Au yeye ndo alikuwa wa mwisho?
Kama hao watu waliokuwa nyuma yake walifanya nin baada ya hapo?
 
Na yy hicho ndicho kinacho mchanganya kiasi kwamba anaona sio haki hakuna usawa
 
mdogo wako alichelewa,next time muwahi maana ndege si daladala.ukishachelewa rules apply,it means km untaka kwenda na ndege ya saa hiyohiyo inabidi ulipe express ticket na ndo hapo badala ya 32000 unalipa 300000.for the same trip.
 
Kama ni kweli hili halipaswi kufumbiwa macho na mamlaka husika
 
Wewe ni mwongo.Haiwezekani mtu akiwa kwenye foleni akaambiwa muda umeisha.
What if check in Clerk alikuwa too slow katika kazi yake?

Hilo unalolisema halipo.As long as upo kwenye mstari, au umeikuta foleni ni lazima ucheck in.

Usitake kutufanya wote humu wajinga.

Ndugu yangu usibishe kama haujui kitu,hao fastjet ni watu wa ajabu sana!watu wanashindwa kucheck in wakiwa kwenye msitari.
Tatizo hapa hiyo system yao inajifunga automatic na ipo Nairobi,na wanakuambia kuwa hawana uwezo nayo,kibaya zaidi watumishi wake nao hawana nidhamu ya kazi hata kidogo,kusafiri na hawa jamaa ni kero ila hatuna jinsi,kibegi kidogo tu unakilipia!na ukishangaa nacho wakati unalipa system ikajifunga inakula kwako!nilishashuhudia watu wakikwama wakiwa kwenye msitari ndugu yangu,inauma sana jinsi serikali inavyojitia upofu kutetea wananchi wake.
Dharula ni kitu cha kawaida katika maisha,ikitokea bahati mbaya umepata tatizo la ghafla,tiketi kuibadili ni bora kununua nyingine!!gharama ni za kutisha!binafsi tiketi 2 niliachana nazo,moja ilikuwa kwenda mwanza tarehe 22/5/2015 na nyingine mwaka jana mwezi 4,nilipojaribu kubadili tarehe ilikuwa ni balaa!sikuamini!
 
Mhhh hawa jamaa ni wahuni sana last week, mwanza to dar reporting time saa 6:05 am tumefika 6:10 am tukakuta check in tayari ndege badala ya kuondoka 8:05 am tukandoka 7:05 am nahisi kuna watu waliachwa wasio enda na muda
 
  • Thanks
Reactions: amu
Wabongo hatujui kufika kwenye vitu in time ndo tatizo, ukifika kwa mda unaotakiwa sidhani kama unaweza kujikuta bado upo kwenye foleni wakati check in inafungwa. Pia ticket kuwa non refundable ni kitu cha kawaida duniani kote hasa kwenye low cost airlines.
 
Nairobian

mkome,
muwe mnapanda hivi videge vidogo vidogo vya wazawa
hatuna ubaguzi wala nini
kama umechelewa foleni tazara,unanipigia simu nakusubiri, mpaka ufike,bei 95,500..dar`````` mwanza``````karibu
 
Last edited by a moderator:
mdogo wako alichelewa,next time muwahi maana ndege si daladala.ukishachelewa rules apply,it means km untaka kwenda na ndege ya saa hiyohiyo inabidi ulipe express ticket na ndo hapo badala ya 32000 unalipa 300000.for the same trip.

Unalolisema ni jipya sidhani kama unaweza kuondoka na ndege hiyhiyo maana ungekuwa hujachelewa bac kama inawezekana, kama vp ckunyngine mfly na prcision ss ambao hata ukichelewa kidogo wanaweza wakakufanyia mpango coz wanahudumia ndege zao wenyewe unlike fastjet
 
Ila tu chili shirika Huduma Zao si user friend. Kweli MTU upo security check foleni wao close desk bila kuja kucheck na waliokwenye ukaguzi kama mashirika mengine wafanyavyo . Gate check ni moja queue ni ndefu. Wabadilike hapo kiukweli
 
Unalolisema ni jipya sidhani kama unaweza kuondoka na ndege hiyhiyo maana ungekuwa hujachelewa bac kama inawezekana, kama vp ckunyngine mfly na prcision ss ambao hata ukichelewa kidogo wanaweza wakakufanyia mpango coz wanahudumia ndege zao wenyewe unlike fastjet


Kuna uwezekano kuwa imetokea na si makosa ya FJ, labda kutokujua, kuna siku binti alikuwa anakwenda Mbeya alfajiri, nilimsindikiza hadi JNIA nikamwelekeza vizuri kuwa apange foleni ya kwenda Mbeya na akisha-check in anipigie simu ili nami niondoke kuelekea kazini

Basi nimesubiri hakuna kitu, kuchungulia nikakuta binti yupo kwenye foleni ya kwenda Mwanza wakati huo Mbeya karibu wanafunga gate, ikabidi nimwombe jamaa akamwambie ndo ikawa salama yake vinginevyo angeishia kulalamika kaonewa.
 
nafikiri mleta uzi hataki kusema ukweli kuhusu huyo mdogo wake kuwa alichelewa. jamani usafiri wa ndege sio kama dala dala au mabasi ya mikoani una taratibu zake. siku nyingine muwahishe huyo mdogo wako masaa 2 kabla ya safari halafu uone kama ataachwa. watanzania walio wengi wagumu sana kwenda na muda.
 
Back
Top Bottom