Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,941
- 3,259
Leo katika pitapita zangu kwenye moja ya mitandao ya Kijamii, nimekutana na tangazo la kuunganishiwa kifurushi au bando kwa bei nafuu (Gb 7 kwa mwezi kwa Tshs. 5,000/=) na kulingana na hali ya mambo kwa sasa ilivyo, nikaona hii ita itanipa unafuu wa maisha maana vifurushi vimekuwa ghali sana kwa siku za hivi karibuni. Nikaamua kujitosa na kutuma muamala baada ya kuhakikishiwa kwamba nitaunganishiwa huduma baada ya dakika 4 tu, toka nimekamilisha malipo.
Basi bana, baada ya kutuma, nikamjulisha mtaalamu wangu kwamba tayari, halafu nikakaa kusubiria. Subiri we dakika 5 zikapita, ikabidi nimuulize tena, "Mkuu mbona sioni msg ya kuunganishwa?"
Akaniambia yuko kwenye process ya kuniunga.
Nikakaa we hadi nusu saa ikapita kisha nikamuuliza tena, vipi mbona hadi sasa sijaona?
Akaniambia inabidi uongezee elfu 7 (7,000/=) ili kuki-activate kifurushi changu.
Kwa sababu mimi ni kati ya watu ambao "tulishapigwa" sana japo hatukomi, nikajiongeza kwamba hapa tayari nimeshapigwa.
Lakini siku zote huwa napenda kuwataarifu wenzangu ili wasije kuumizwa kama ambavyo mimi nimeumizwa.
Hivyo lengo kuandika uzi huu, ni kuutahadharisha umma wa JF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba kuna wizi mpya umeingia.
Tusipende vitu vya bei nafuu, maana mara nyingi huwa na gharama za ziada zilizofichika.