Wizi mpya wa "kuunganishiwa mabando (GBs)" umeibuka!

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,899
3,201
Leo katika pitapita zangu kwenye moja ya mitandao ya Kijamii, nimekutana na tangazo la kuunganishiwa kifurushi au bando kwa bei nafuu (Gb 7 kwa mwezi kwa Tshs. 5,000/=) na kulingana na hali ya mambo kwa sasa ilivyo, nikaona hii ita itanipa unafuu wa maisha maana vifurushi vimekuwa ghali sana kwa siku za hivi karibuni. Nikaamua kujitosa na kutuma muamala baada ya kuhakikishiwa kwamba nitaunganishiwa huduma baada ya dakika 4 tu, toka nimekamilisha malipo.

Basi bana, baada ya kutuma, nikamjulisha mtaalamu wangu kwamba tayari, halafu nikakaa kusubiria. Subiri we dakika 5 zikapita, ikabidi nimuulize tena, "Mkuu mbona sioni msg ya kuunganishwa?"

Akaniambia yuko kwenye process ya kuniunga.

Nikakaa we hadi nusu saa ikapita kisha nikamuuliza tena, vipi mbona hadi sasa sijaona?

Akaniambia inabidi uongezee elfu 7 (7,000/=) ili kuki-activate kifurushi changu.

Kwa sababu mimi ni kati ya watu ambao "tulishapigwa" sana japo hatukomi, nikajiongeza kwamba hapa tayari nimeshapigwa.

Lakini siku zote huwa napenda kuwataarifu wenzangu ili wasije kuumizwa kama ambavyo mimi nimeumizwa.

Hivyo lengo kuandika uzi huu, ni kuutahadharisha umma wa JF na Watanzania wote kwa ujumla kwamba kuna wizi mpya umeingia.

Tusipende vitu vya bei nafuu, maana mara nyingi huwa na gharama za ziada zilizofichika.
Screenshot_20230809-181502_Telegram.jpg
 
Waambie wakuunge ndio uwalipe tofauti na hapo hiyo ni scam

Japo kunakuwaga na trust issues lakini usiwe mwepesi kumwamini mtu otherwise wawe wanatoa free trial.
Ahsante sana kwa ushauri Mkuu
 
Umeibuka au wewe ndo umekufikia
Hakuna anaeuza bando zaidi ya mitandao husika kwa USSD au APP zao.Huu utapeli sio mpya ni wewe tu ndo umeingia kwenye mfumo wa kitapeli

Kaa kitaalam
Kha!
Basi leo naona ilikuwa zamu yangu.
Lakini anyway, kukosea njia ndo kujua njia.
 
Nilihisi tuu kua ni Telegram,
kuna wale wanakuja wakijidai wakenya/waganda au South Africans wakitaka mfanye business.
 
Kwaiyo na wewe ukaamini 5k inakupa GB 7...

Sema watz wengi hatujui kuhoji...
Acha tu tuendelee kupigwa ili akili zitukae sawa. Binafsi sitaki hata mtu anihurumie kwa hili.
😊😊😊😊😊
 
Life mtaani ni gumu ukijichanganya na tamaa zako kupigwa umeme ni sekunde tu.

Airtel wana SME Tigo nao wana ile program yao ya kulipa kwa mwezi watafute hao utakuwa salama nje ya hapo kilio hakiepukiki
Ahsante sana kwa ushauri Mkuu.
Hiyo SME ndo nini?
 
Nilichopenda umekiri kupigwa bila kupindisha pindisha😂😂😂.

Kuna kimalaya (nakiita kimalaya maana ni kijizi) nilikutana nako FB. Kakiniletea story hizo za kuungwa bundle kwa bei chee.

Nikakiambia kuwa kazi zangu nafanya sana online hivyo aniunganishe cha mwezi mzima lakini ningependa nikutane nae ili nimkabidhi pesa.

Kalivyo kajinga kakaja kweli. Nilikapeleka guest, kalivyokuwa kanaoga nikapekuwa kitochi chake nakuta msg za malalamiko kibao za waliotuma pesa bila kuungwa.

Fasta nikasevu namba yangu kama airtelmoney kwenye simu yake. Kalipotoka kakasema nikape pesa ya kuungwa maana cha mwezi kinachukua muda hivyo inabidi amjulishe mwenzie aanze process.

Nikamtumia msg ya muamala fake wa thamani ya kifurushi cha miezi mitatu. Nikamwambia wewe mwambie aunge sisi tufanye yetu.

Nilikapiga mbupu, baada ya kumaliza nikakaambia nauli akate kwenye pesa ya bundle aniunge cha miezi miwili badala ya mitatu.

Itoshe kusema baada ya dk kadhaa za kuachana nilitukanwa kila aina ya tusi kwenye msg.
 
Back
Top Bottom