Wizi mpya: Kaeni chonjo!

Columbus

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,004
1,195
Jana nilipata kisa kimoja kutoka kwa my wife,alipotoka kanisani alikutana na vijana wawili waliokuwa wamevalia sare za kampuni ya simu ya Vodacom wakidai wanasaidia wateja wao kuunganishiwa huduma za internet.

Baada ya my wife kuwakabidhi simu yake waliifungua na kuirudishia na kumuahidi ataanza kutumia internet baada ya saa moja.Punde si punde akagundua simu yake haiko hewani na baadaye kidogo akagundua alikuwa amebadilishiwa sim card mpya isiyosajiliwa.

Tulipata hisia huenda walikuwa ni wezi ndipo tukaamua kubadili password nmb mobile kupitia ATM na baadaye tulipiga simu Vodacom ambapo walitujulisha walikuwa wameshatoa sh.laki 350 kutoka nmb.

Tahadhari: Tuwe macho tusiwaamini hata wanaojifanya ni wafanyakaZi wa kampuni za simu.
 
mwambojoke

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
941
1,000

Password ni siri yako, bila mkeo kuwapa password asingeibiwa kamwe.
 
delako

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
2,596
2,000
Poleni sn!shem amefunga mwaka!ungetaja mkoa na hata sehemu tuongeze umakin na tuwasake kimya kimya.
 
Eddy Love

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
13,140
2,000
kumbe hamuwajui mahackerz hzo ATM zinaibiwa daily mabank yanalalamika me nasema kilichotengenezwa na binadam akishindwi kwa binadam mwingine
 
Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,423
1,500
Inamana password zako unarikodi kwenye simu??walipataje hizo nmb mobile password??hata wakichukuwa sim card bado hawatoweza kuchukua pesa zako kama hukuweka wazi password zako,haijaniingia bado sorry.

unajua kitu inaitwa udukuzi, udukuaji au hacking. we kama unatambaa technologia inapepea, kalaga baho!
 
mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,340
2,000
muulize vizuri mkeo nini kilitokea eneo la tukio sio unakubali tu kuburuzwa wakati ukuwepo
 
mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,340
2,000
Tatizo la kuoa wanawake wasiosoma. anamwamini vipi total stranger hata akagawa simu yake. alikua ameangalia wapi wakibadilisha line ? mhoji vizuri huyo my wife wako huenda kuna vingi umeibiwa

ww jamaa taratibu utavunja ndoa ya mwenzio mkuu...ukila na kipofu usimshike mkono
 
Sanoyet

JF-Expert Member
Apr 3, 2013
1,324
1,225
Pole sana,mwezi juzi nilikutana na kisanga kama hicho, baada ya kucheza na simu yangu waliweza kudeactivate jina langu la M-pesa a/c,hivyo details zangu zote za m-pesa wakaziua,nilipotumiwa pesa ikaenda kwa mwingine namba ile ile i.e one number two people!
Inasikitisha sana
 
Galamtogela

Senior Member
Aug 25, 2013
101
195
Tatizo la kuoa wanawake wasiosoma. anamwamini vipi total stranger hata akagawa simu yake. alikua ameangalia wapi wakibadilisha line ? mhoji vizuri huyo my wife wako huenda kuna vingi umeibiwa

simu nyingi internet inajiconnect automatically labda mimi ndio sijui?
 
Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,186
2,000
mchunguze vizuri mkeo, atakuwa keshafundishwa na shoga zake namna ya kula bata mujini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom