Andrew Chenge: KASHFA MPYA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Andrew Chenge: KASHFA MPYA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bujibuji, Mar 18, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Achunguzwa kutumia madaraka vibaya kama Yona
  [​IMG]Maswahiba zake wahaha kumuengua kashfa ya rada

  WAKATI kukiwa na mkakati wa kumnasua Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge katika kashfa ya ununuzi wa rada ya kijeshi, mwanasiasa huyo sasa anachunguzwa kuhusika katika kashfa nyingine ya kutumia vibaya madaraka alipokuwa Waziri wa Miundombinu, Raia Mwema limefahamishwa.

  Habari za ndani ya serikali zimeeleza kwamba, baada ya juhudi kubwa za kumuokoa, hali sasa imebadilika na vyombo vya dola vimeanza kuchunguza uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema ambaye Chenge anahusishwa nao kwa kupindisha taratibu kufanikisha uteuzi huo.
  [​IMG]

  Andrew Chenge

  Wachunguzi wameeleza kwamba, Chenge anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yake na wanamuandalia mashitaka kama yale ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Daniel Yona na Katibu Mkuu wake, Gray Mgonja, ambao hadi sasa kesi zao ziko mahakamani.

  Vyombo vya dola vinaelezwa kuchunguza pia utata katika mkataba wa ajira ya Mrema baada ya kubainika kutofautiana hata na barua ya uteuzi uliofanywa na Chenge, ikiwamo kipengele muhimu kinachozungumzia kipindi cha mkataba na suala la kodi mbalimbali za serikali ambavyo vimebadilishwa katika mazingira ya utata.

  Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba uchunguzi huo unaanzia mbali mwaka 2007 ambako Serikali, kupitia Wizara ya Miundombinu, iliajiri mshauri mwelekezi, kampuni ya Price Waterhouse Coopers kufanya mchakato wa kumtafuta Mtendaji Mkuu wa Tanroads, kabla ya Chenge kuamua kushinikiza kutupiliwa mbali kwa mapendekezo ya mshauri huyo na kuunda timu mpya ya uteuzi ambayo ilipokea maelekezo kutoka wizarani.

  Raia Mwema
  ilizungumza na Chenge kwa simu akiwa jimboni kwake, Bariadi Magharibi na kukataa kueleza kilichojiri katika mchakato huo, akisisitiza kuwa hawezi kuzungumzia masuala ya serikali kwa kuwa hayuko serikalini kwa sasa.

  “Sikiliza nikueleze bwana, mimi kwa sasa siyo waziri….siko serikalini nimekwishaondoka huko. Maadili hayaruhusu mtu aliyekuwapo madarakani kuzungumzia masuala ya ofisi hiyo kwa sababu waziri wa sasa yupo na pia rekodi zote za serikali kuhusu wizara hiyo zipo,” alijibu Chenge.

  Pamoja na majibu hayo ya Chenge, inaelezwa kuwa kwa mujibu wa wachunguzi, uamuzi wake wakati akiwa Waziri unahusishwa na kuyumba kiutendaji kwa Tanroads na kusababisha malalamiko kutoka katika Kamati ya Miundombinu na hata ndani ya Bunge ambako Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM), alihoji uteuzi huo waziwazi bila kupata majibu toka serikalini.

  Akichangia bungeni mwaka jana, Mporogomyi alisema Mrema hana taaluma ya uhandisi ujenzi; huku analipwa mamilioni ya fedha za Watanzania na kuongeza: “Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu.”

  Katika barua ya ajira ya Mrema iliyosainiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Enos Bukuku, inatajwa kwamba Mtendaji Mkuu huyo ameteuliwa na Chenge kwa kipindi cha miaka mitatu na kwamba “mapato yote yatalipiwa kodi kwa mujibu wa sheria”, lakini mkataba wa ajira uliosainiwa Juni 2007, unaonyesha kwamba ni mkataba wa miaka mitano na kwamba hatolipa kodi kutoka katika mshahara wake wa Sh 10, 900,000 na marupurupu mengine.

  Kumbukumbu rasmi za Bunge zinaonyesha kwamba mtendaji huyo ameelezwa kwamba alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).

  Pia ameelezwa kwamba analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya serikali, uchunguzi dhidi ya Chenge pia unajikita zaidi katika kuangalia sababu za gharama za ujenzi wa barabaara kuwa kubwa kulingana na nchi nyingine jirani ambako kwa Tanzania gharama za kutengeneza kilomita moja ya barabara ya lami zimeruka na kufikia 1.9 billion (Dola milioni 1.46) wakati inaelezwa nchi jirani kama Kenya na Zambia gharama ni kati ya Dola za Marekani 500,000 hadi 600,000.

  Tayari serikali inaelezwa kupoteza takriban Sh bilioni moja kwa mwezi kutokana na kuingia mkataba na wakandarasi bila ya kuwa na fedha za kuwalipa kuanza kazi, na hivyo kujikuta wakilipwa fidia kila mwezi bila ya kufanya kazi zozote, hali ambayo imeelezwa kuwafanya wachunguzi kufuatilia sababu hasa ya kusainiwa kwa mikataba hiyo bila ya kuwapo fedha.

  Hayo yakiendelea, habari zinaeleza kwamba, kuna mkakati sasa wa kumuengua Chenge katika mashitaka ya tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi yenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 28 (takriban bilioni 70/-), na kumuingiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Salim Msoma.

  Habari za ndani ya serikali zinaeleza kwamba, juhudi hizo ni katika mkakati wa kuzima kile kinachoelezwa “mgogoro wa kisiasa” ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako kundi la watuhumiwa wa ufisadi linaelezwa kupambana kuhakikisha kwamba wafuasi wake wanakuwa salama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vinginevyo “watajibu mapigo kiana”.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mbali ya Chenge kutaka kuokolewa katika mashitaka ya tuhuma za rada, watuhumiwa wengine wanaotajwa kutaka kuenguliwa ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idriss Rashidi ambaye kwa sasa anastaafu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Chenge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati rada ikinunuliwa, aliingia katika siasa Mwaka 2005 kwa kuwania ubunge jimbo la Bariadi Magharibi na baadaye kuteuliwa kuwa Waziri wa Afrika Mashariki kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Miundombinu, alikolazimika kujiuzulu kwa kashfa ya rada.

  Chenge alilazimika kujiuzulu nafasi yake baada ya kutajwa hadharani kuhusika kwake na ununuzi wa rada na kubainika kumiliki akaunti nje ya nchi yenye kiasi kikubwa cha fedha ambazo yeye aliziita kuwa ni ‘vijisenti.’

  Baada ya kuondoka BoT mwaka 1998, Dk. Rashidi aliingia katika sekta binafsi ikiwamo benki ya Akiba Commercial, Vodacom Tanzania na benki ya NMB kabla ya kuteuliwa tena kuongoza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) aliko hadi sasa.

  Watuhumiwa wengine wawili wakuu waliotajwa ni pamoja na mtuhumiwa mkuu, ambaye kwa sasa amekimbilia nje ya nchi Shailesh Pragji Vithlani na mshirika wake mkuu kibiashara Tanil Jumar Chandulal Somaiya.

  [​IMG]

  Shailesh Pragji Vithlani

  Chenge, Dk. Rashidi, Vithlani na Somaiya wote wametajwa kuwa washiriki wakuu waliowaongoza wengine katika kufanikisha biashara hiyo tata kwa upande wa Tanzania. Kila mmoja kwa sasa amekwisha kuchunguzwa kuhusiana na suala hilo.

  Wakati Chenge alishiriki kwa kiasi kikubwa kama Mtaalamu wa sheria, Dk. Rashidi ametajwa kushiriki kama mtaalamu na mhusika mkuu wa mambo ya fedha.

  Taarifa zinaonesha kwamba Vithlani na Somaiya walikuwa na hati za kiapo zenye kuwapa mamlaka ya kisheria kuwakilisha kampuni iitwayo Envers Trading Corporation.

  Uchunguzi unaonyesha kwamba Envers Trading ililipwa dola za Marekani milioni 12 na kampuni nyingine iitwayo Red Diamond Trading, iliyofunguliwa mwaka 1998 katika visiwa vya Virgin ambavyo ni sehemu ya dola ya Uingereza.

  Red Diamond Trading ilikuwa na uhusiano mkubwa na kampuni iitwayo BAE Systems, ambayo ilitengeneza na kuuza rada iliyouziwa serikali ya Mkapa mwaka 2002.

  Imedaiwa kwamba Red Diamond iliweza kujinufaisha kwa kutumia mianya ya kisheria katika visiwa vidogo vya Caribbean ambako kampuni kama hiyo zinaweza kuficha taswira ya akaunti zake benki ikiwa ni pamoja na majina ya wamiliki wake.

  Akihojiwa na wapelelezi wa Uingereza, Somaiya, ambaye anamiliki kampuni ya Shivacom ya mjini Dar es Salaam, alikiri kuwa na hati zao za kiapo zenye kuwapa mamlaka ya kisheria kuwakilisha kampuni iitwayo Envers Trading Corporation kwa miezi 11.

  Somaiya alikiri katika mahojiano hayo kwamba yeye na "rafiki yake mkubwa" Vithlani wanamiliki kwa pamoja kampuni iitwayo Merlin International.

  Hata hivyo, Somaiya kupitia kwa wakili wake aliiambia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwamba aliacha kuwa mwenye hisa na mkurugenzi wa Merlin International mnamo Januari 8, mwaka huu.

  Kwa sasa Vithlani pekee ndiye anayetafutwa na ameshitakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuwa sio mmiliki wa Envers Trading na kuhusu kupokea dola 390,000 kwa biashara ya rada wakati ukweli ni kwamba alilipwa kitita cha dola milioni 12.

  SOURCE: RAIA MWEMA
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maoni yangu: Watu hawa wote wanapashwa wawe keko na sio serikali kuwachekea. Everything is seen transparently
   
 3. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sijui serikali inasita nini kuwakamata halafu wanacheka nao meza moja, hivi uko NEC ya ccm hakuna maadili kabisa tangu mwalimu amekufa?? Make angekuwapo mwalimu wengine tayari wangekuwa wamechapwa hata viboko, mwalimu alikuwa hana mchezo na ujinga huo, kama sio mwadilifu anakwambia machoni pako

  Lakini si mnakumbuka hata mwaka 1995 huyu rais wetu aliambiwa sio mwadilifu na hawezi kuongoza nchi yetu, au WAATANZANIA NYIE WASAHAULIFU sana? Mwalimu alisema wazi kuwa JK na EDO hawafai kabisa kuiongoza Tanzania, sasa mimi ile kauli ya maskofu kuwa jamaa ni chaguo la Mungu ilinishangaza sana-------wewe jaribu kuangalia tu hao jamaa na round tables zao, hawafaiiiiiii kabisaaaaaaaa, wote wameoza hakuna wa afadhali
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Si mwingine huyu Chiligati kamuajiri Boss wa Shirika la Nyumba la Taifa kwa kutumia mlango wa nyuma? Waliajiri kampuni ifanye Mchakato wa kumtafuta CEO wa shirika na baada ya pesa kibao kutumika, wao wakaja wakaajiri mtu wao ambaye kwenye mchujo alitupwa kama pakacha la ulezi.

  Msiumie sana. Ndiyo pesa za Tshirt za njano na kijani, Pilau na nyama za uchaguzi zitatoka huko. Huku akina mama wakifurahia khanga za Chama chao cha Ma.......
   
 5. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu mbona hilo shirika lilikufa miaka kibao wakati hata chiligati hajulikani au una maana National Housing?
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kwa nini chenge hanyongwi?????
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tupo wote mkuu. Ndiyo uzuri wa JF, uko sawa kuwa ni National Housing Corp.
   
 8. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I am abit feed up with this Chenge person...inabidi akanyoe nywele zake kwanza aonekane smart :) lol
   
 9. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha!! Magezi unaonekana umekereka sana. Sisi sote bwana.

  Hanyongwi kwa sababu hatuko China au Saudi Arabia. Ni Bongo ambako mtu anachunguzwa kwa makosa makubwa kama haya lakini hastaafu, hasimamishw wala nini ili kupisha uchunguzi.

  Na ikifika Oktoba Bariadi watamchagua tena kuwa mbunge wao
   
 10. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu watu wa jinsi hii wala hawahitaji kunyongwa kwani huwa wanajinyonga wenyewe...!! Wajua nimetabili kifo cha huyu bwana kitakuwa kama cha kuku nikimaanisha chenye mateso makubwa..!!
   
 11. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh, umekuwa Sheikh Yahya?

  Watu kama hawa wala tusiwaombee kifo wala wasihukumiwe kifo.
  Kinachotakiwa ni wasote gerezani na wafanye shughuli za kujenga taifa wakiwa humo (community service)
   
 12. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahaaa!! Mkuu hapana mimi si Yahya, Bali ni utabili wangu binafsi. Namshauri aje nimsafishe NYOTA .Maana nyota yake imechafuka sana...hahahahaaa..! Watu wa jinsi hii ukiwasubiria magereza huwezi kuwa pata hata kidogo..! Labda Kipindi cha Mwalimu.
   
 13. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ila kweli, mjumbe wa CC ya kyama kyawala aende gerezani? Ghafla tu namna hiyo? Bado bado, some decades to come ndio hiyo mambo itakuwa labda
   
Loading...