Wizi mpya: Kaeni chonjo!

Mkuu tuombe radhi.....wengine
hatuingiliki kirahisi hivyo......unakutanaje na watu huwajui unawapa
simu....?.....ofisi za kampuni hazijui.....?...aseme vizuri bana
kapeleka wapi pesa.....alishindwa nini kumpa mumewe simu aweke
internet..?....au na mumewe ndio wale wale.....angekuwa shoga'ngu
ningemzabua.......

Dada Preta, nisamehe bure!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana,mwezi juzi nilikutana na kisanga kama hicho, baada ya kucheza na simu yangu waliweza kudeactivate jina langu la M-pesa a/c,hivyo details zangu zote za m-pesa wakaziua,nilipotumiwa pesa ikaenda kwa mwingine namba ile ile i.e one number two people!
Inasikitisha sana

Technically its impossible
 
Sijafaham zaidi inakuwaje mtu unampa sim yako while haina tatizo lolote, mbaya zaidi mtu unakutana nae mtaani tu. Kipindi tunakamata maafisa usalama feki, matrafic feki na asikal feki ilitangazwa kabisa on public now iweje kusiwe na wafanya kazi wa vodacom feki na ile ni private sector. Mnatia hasira sana watu kama nyie.

Huyu mama mzururaji. Kama una issue za maana barabarani unakuwa na focus moja na huwezi ruhusu stranger kukuvamia na interest zao. Matunda ya uzururaji hayo
 
Huo mchezo hauanzii wala kuishia barabarani.....Ofisi kuu inahusika.

Ndugu zangu tuache kushawishiwa na sare na vitambulisho..Hii nchi ishazalisha matapeli wa kutosha mitaani. Wengi wameshaibiwa na hao wanaovaa sare. Kwangu uje na sare ya Polisi, DAWASA, Tanesco na zozote zile unaishia getini.Na barabarani hunisimamishi ovyo hata uvae sare za aina gani?!
 
Mimi wamewahi kutaka kuniibia kwa kujifanya kuwa ni watumishi wa NMB kuwa ninahitajika kubadili taarifa zangu za NMB mobile. Walinihoji kwa dakika moja hivi lakini nilishtuka na nikawatukana sana. Baadaye walifunga ile simu na hata nilipowafuatilia sikuwapata. Kaeni chonjo sana na wezi hawa ---------- na watumishi wasio waaminifu wa NMB na wanawafuatilia wale wateja wenye hela nyingi kwenye akaunti zao.
 
Jana nilipata kisa kimoja kutoka kwa my wife,alipotoka kanisani alikutana na vijana wawili waliokuwa wamevalia sare za kampuni ya simu ya Vodacom wakidai wanasaidia wateja wao kuunganishiwa huduma za internet.

Baada ya my wife kuwakabidhi simu yake waliifungua na kuirudishia na kumuahidi ataanza kutumia internet baada ya saa moja.Punde si punde akagundua simu yake haiko hewani na baadaye kidogo akagundua alikuwa amebadilishiwa sim card mpya isiyosajiliwa.

Tulipata hisia huenda walikuwa ni wezi ndipo tukaamua kubadili password nmb mobile kupitia ATM na baadaye tulipiga simu Vodacom ambapo walitujulisha walikuwa wameshatoa sh.laki 350 kutoka nmb.

Tahadhari: Tuwe macho tusiwaamini hata wanaojifanya ni wafanyakaZi wa kampuni za simu.
Du!!!! poleni sana.. lalini passwords za NMB mobile walitoa wapi??
 
Kama unaanza utapeli/wizi, anza kwa wanawake. Baada ya kubobea kidogo, uje kwa wanaume.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom