Wizi Masaki wakati wa jioni

Wizi Masaki wakati wa jioni

rugumye

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
561
Reaction score
179
Ndugu wana jamii kuna gari aina ya Toyota Rav 4 Model ya zamani rangi ya kijani ina zunguka mitaa ya masaki mida ya jioni na kunyakua vitu vya mikononi hasa laptop. Juzi jumatatu rafiki yangu mmoja mida ya saa 11:20 maeneo ya Masaki TANESCO akiwa anatembea kwa miguu baada ya kutoka kazini kuelekea kituo cha daradara gari hilo lilitokea kwa nyuma na kunyakua kibag cha lap top bahati mbaya alikuwa amekivaa begani hivyo alianguka kwenye rami na kuumia vibaya. Yawezekana wakawa wanabadili gari, piki piki na bajaj hivyo kuweni makini.
 
Matukio hayo yapo kitambo hususan maeneo ya sea cliff; watu wengi wameporwa, wageni ndio zaidi.
Pamoja na kuripotiwa polisi, madhara yanaongezeka jamaa wanaendelea na kazi yao.
Inasikitisha sana!!! Jana nimepata kisa kingine cha polisi wa bongo.
Kuna wachina walikuwa wanatokea kupata burudani serena hotel wanaelekea richmond towers, upanga kwenye makazi yao wakati wa usiku. Walipofika maeneo kati ya redcross na agakhan wakasimaimishwa na polisi wawili wenye silaha wakadai driving licence, wakaoneshwa; wakadai working permit, wachina wakawaambia vibali tunavyo tunapoishi twendeni. Jamaa wakaingia garini wakawatia pingu wakawaambia sasa tunakwenda polisi lakini walichofanya ni kuwasachi pochi zao wakachukua pesa zote kisha wakawaachia. Basi wachina wakabaki wameduwaa huku polisi wakiwatishia silaha.
 
Hilo siyo eneo la polisi/trafiki kusimamisha gari na kulikagua.
Hao jamaa wanaweza wakawa ni "polisi-majambazi" au "raia -majambazi"
 
Huko sahihi mkuu, Polisi ambao wako zamu hawawezi kufanya matendo kama hayo, naona wahusika aidha ni raia-majambazi wanao vaa nguo za polisi na waliwahi kufanya kazi polisi au ni polisi majambazi, mkuu nchi hii anything goes na hawaogopi kitu!

Hili suala la watu kuporwa mabegi yao na kuhumizwa limekwisha zungumzwa humu mara nyingi, nakumbuka kuna mwana JF aliwahi kueleza alivyo nyanganywa simu na fedha barabara ya Ali Hassan karibu na Salender Bridge karibu kabisa na kituo cha Polisi, bahati nzuri alikuwa anafahamiana na afisa polisi wa kituo hicho ambaye aliwahi kuwa classmate wake, baada ya kueleza kilicho mtokea - jamaa akashauliwa haje baada ya siku mbili, baada ya siku moja kupita kapigiwa simu akutane na afisa huyo kwenye baa fulani - kwenda kule karudishiwa SIMU yake lakini hela hazikurudishwa - sasa hii inatoa picha gani?

Haiwezekani waporaji hawa wakawa wanatamba na magari/pikipiki wakiumiza watu barabarani hasa hasa sehemu za masaki na kinondoni bila ya kukamatwa, wakati kuna polisi wa doria wenye pikipiki - kwa nini hawawekewi mtego, juzi juzi mama daktari wa kigiriki alipoteza maisha kutokana na kundi hili - Mh. Kova alisema mtandao wa majambazi hao umekwisha vunjwa sasa hawa wamehibuka kutoka wapi tena!
 
Ni kweli jamani,huu wizi upo sana DSM,hasa maeneo ya huku kwa watu wa daraja la kati,mimi mwenyewe May,2011 waliniibia laptop na vitu vingine kama simu,mbaya zaidi waliniburuza na kuniumiza vibaya,SITOSAHAU,..tukio lenyewe lilitokea njia ya kwenda chuo cha Uandishi wa habar(UDSM) Mikocheni kutokea Millenium tower,Makumbusho..Ewe Kova hebu tokomeza hawa Magaidi pia wandugu tuwe makini tutembeapo kandokando ya barabara,ni HATARI!!!!
 
unaweza kuwatofautish

ndio,jambazi ni mtu anayemnyang'anya mwingine mali yake kwa nguvu (mfano kutumia silaha)
Polisi jambazi = ni polisi (kiajira) ila akawa amefanya ujambazi
Raia jambazi = ni raia ambaye amefanya ujambazi
 
Huko sahihi mkuu, Polisi ambao wako zamu hawawezi kufanya matendo kama hayo, naona wahusika aidha ni raia-majambazi wanao vaa nguo za polisi na waliwahi kufanya kazi polisi au ni polisi majambazi, mkuu nchi hii anything goes na hawaogopi kitu!

Hili suala la watu kuporwa mabegi yao na kuhumizwa limekwisha zungumzwa humu mara nyingi, nakumbuka kuna mwana JF aliwahi kueleza alivyo nyanganywa simu na fedha barabara ya Ali Hassan karibu na Salender Bridge karibu kabisa na kituo cha Polisi, bahati nzuri alikuwa anafahamiana na afisa polisi wa kituo hicho ambaye aliwahi kuwa classmate wake, baada ya kueleza kilicho mtokea - jamaa akashauliwa haje baada ya siku mbili, baada ya siku moja kupita kapigiwa simu akutane na afisa huyo kwenye baa fulani - kwenda kule karudishiwa SIMU yake lakini hela hazikurudishwa - sasa hii inatoa picha gani?

Haiwezekani waporaji hawa wakawa wanatamba na magari/pikipiki wakiumiza watu barabarani hasa hasa sehemu za masaki na kinondoni bila ya kukamatwa, wakati kuna polisi wa doria wenye pikipiki - kwa nini hawawekewi mtego, juzi juzi mama daktari wa kigiriki alipoteza maisha kutokana na kundi hili - Mh. Kova alisema mtandao wa majambazi hao umekwisha vunjwa sasa hawa wamehibuka kutoka wapi tena!

Tatizo polisi wamekuwa reactive sana badala ya proactive. Yaani hujifanya wapo serious linapotokea tukio ila jinsi ya kuvunja hii mitandao ya wezi na majambazi hawafanyi hivyo. Yaani jamaa wanatamba kila kona! Hii ndio maana inapelekea raia kujichukulia sheria mikononi!
 
wanakera hawa sasaivi wana pikipiki BAJA mmoja anakaa nyuma wakikutana na mwanamke anasuhuka anamkaba anadandia pikipiki uyooo tena ni watoto wa kiarabu ndo wanafanya michezo iyo
 
Matukio hayo yapo sehemu nyingi sana Dar, hapo ndio umuhimu wa CCTV unaonekana. Kuna wengine wanatembea na gari yao pickup wakiona pikipiki wanapakia na kutokomea.
 
Huko sahihi mkuu, Polisi ambao wako zamu hawawezi kufanya matendo kama hayo, naona wahusika aidha ni raia-majambazi wanao vaa nguo za polisi na waliwahi kufanya kazi polisi au ni polisi majambazi, mkuu nchi hii anything goes na hawaogopi kitu!

Hili suala la watu kuporwa mabegi yao na kuhumizwa limekwisha zungumzwa humu mara nyingi, nakumbuka kuna mwana JF aliwahi kueleza alivyo nyanganywa simu na fedha barabara ya Ali Hassan karibu na Salender Bridge karibu kabisa na kituo cha Polisi, bahati nzuri alikuwa anafahamiana na afisa polisi wa kituo hicho ambaye aliwahi kuwa classmate wake, baada ya kueleza kilicho mtokea - jamaa akashauliwa haje baada ya siku mbili, baada ya siku moja kupita kapigiwa simu akutane na afisa huyo kwenye baa fulani - kwenda kule karudishiwa SIMU yake lakini hela hazikurudishwa - sasa hii inatoa picha gani?

Haiwezekani waporaji hawa wakawa wanatamba na magari/pikipiki wakiumiza watu barabarani hasa hasa sehemu za masaki na kinondoni bila ya kukamatwa, wakati kuna polisi wa doria wenye pikipiki - kwa nini hawawekewi mtego, juzi juzi mama daktari wa kigiriki alipoteza maisha kutokana na kundi hili - Mh. Kova alisema mtandao wa majambazi hao umekwisha vunjwa sasa hawa wamehibuka kutoka wapi tena!

Yooote umenena... ila ilipofika kwa Kova umeniacha hoi!!!! Hivi kweli bado unaamini huyo bwana anachosema kinatoka kwenye roho(moyoni) mwake????@@@!!!!!!
 
Matukio hayo yapo sehemu nyingi sana Dar, hapo ndio umuhimu wa CCTV unaonekana. Kuna wengine wanatembea na gari yao pickup wakiona pikipiki wanapakia na kutokomea.

CCTV my god!!!! Hapa wachangiaji wanazungumzia moral authority ya polisi(PoliCCM) wetu. Hata kama una CCTV mji mzima na polisi ni washiriki wa haya matukio itasaidia nini? Unless kama una divert attention kutoka kwenye main topic then you must be very blind!!!!
 
kuna siku moja ,nilishuhudia kwa macho yangu katikati ya jiji, kijana mmoja mwenye asili y aki Asia akinyang'anywa mkoba wake pembeni ya barabara huku akiburuzwa na gari aina ya Mark II GX 110, Kwa bahati mmoja kati ya wale wezi aliteremka ndani ya ile gari ili kuokota ule mkoba ambao nafikiri ulikua na LAP TOP,niliigonga ile gari pamoja na yule aliyeteremka kwenye lile gari ,ile gari haikusimama nilijita hidi kuikimbiza sikuippata ila nakumbuka prifex za ile gari zilikua BQA
 
Huo wizi ni kweli upo. Kuna watu ninaowafahamu, ninafanya nao kazi wameporwa Ipad mitaa ya Oysterbay, nyuma ya shule ya msingi Oysterbay. Ni vitendo vilivyoshamiri maeneo mengi sana ya jiji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom