Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,233
kuna siku moja ,nilishuhudia kwa macho yangu katikati ya jiji, kijana mmoja mwenye asili y aki Asia akinyang'anywa mkoba wake pembeni ya barabara huku akiburuzwa na gari aina ya Mark II GX 110, Kwa bahati mmoja kati ya wale wezi aliteremka ndani ya ile gari ili kuokota ule mkoba ambao nafikiri ulikua na LAP TOP,niliigonga ile gari pamoja na yule aliyeteremka kwenye lile gari ,ile gari haikusimama nilijita hidi kuikimbiza sikuippata ila nakumbuka prifex za ile gari zilikua BQA
Mkuu usifanye makosa hayo tena, we mtu mpaka ateremke kutoka garini anajiamini nini!!! Bila shaka wanakua wako well armed wala hawafikilii mara mbili kabla awajafyatua risasi, chunga sana mkuu; katika situation kama zile unapaswa kukumbuka wimbo wa Tina Turner usemao "We Don't Need Another Hero"
Cha muhimu hapa ni Polisi kushirikiana na raia kama wako serious ku-nip in a bud tatizo hili linalo onekana limeanza kushamiri jijini, takwimu zinaonyesha karibu kila tukio kuna mashuhuda, na kwa bahati nzuri raia wengi wanatembea na simu zao za mikononi kwa hiyo ni rahisi kuwasiliana na Polisi Central au hata na IGP ili watoe instruction kwa polisi doria wa magari/pikipiki kufatilia waharifu - ni kazi rahisi tu, we sema hatujuhi polisi wenyewe wako commited/motivated kwa kiasi gani?
Wizara ya mambo ya ndani hisipo address tatizo hili the soonest, basi jiji la DAR litakuwa blacklisted kama ni jiji hatari kwa watalii wanao pendelea kutembea kwa miguu, si kwa watalii tu hata sisi raia tutahanza kuogopa ku-stoll kwenye barabara ambazo ziko karibu na ufukwe wa bahari, Masaki na part ya Kinondoni. Kifo cha Daktari wa Kigiriki mwana mama kilifedhehesha TAIFA letu, we sema tuna roho ngumu kama ya PAKA!!!! Mimi sikutegemea kama ushenzi huu ungekuwa unaendelea kuwepo bila ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu, Polisi ya TAIFA letu ni mahili sana wakiamua kushughulikia tatizo kikamirifu, ukiona wanasua sua ujuwe kuna tatizo somewhere sio kwamba hawajuhi jinsi ya kulishughulikia.