Wizi arusha......

Jamani wana jamii ninaombeni sana msaada wenu..jana jioni siku ya Jumamosi maeneo ya Metropolitan karibu na Green heart restaurant kwa wale wanaofahamu Arusha nikiwa kwenye pikipiki nilivamiwa na kundi la Vijana zaidi ya 50 waliokua wanaandamana wakaninyang'anya hand bag yangu kwa kuivuta kwa nguvu hadi ikakatika mkanda, nikashuka kuwafatilia wakatoa visu pamoja na sime wakanambia kama nataka kufa niwafate watu waliokuwepo around walinisihi nisiwafate maana wale jamaa ni watu wabaya na waweza hata niua,mie bado mgeni hapa Arusha, then wakatokomea nayo kuelekea maeneo ya Unga limited...kwenye hand bag yangu kulikua na IPAD aina ya APPLE 32GB pamoja na vitu vingine vidogo vidogo...nilifika kuripoti kituo cha police cha Unga limited askari nilimkuta akitiririka jasho kanambia ndiyo tu kwanza katoka kukimbizana na jamaa hao hao walimu-attack jamaa moja na kumchania suruali yake wakachukua pesa pamoja na walet yake pia huko njiani walikua wakipiga watu na kuwanyang'anya vitu kama handbags kwa akina mama?dada...Ombi langu kwa wana Jamii wa Arusha PLease ukiona mtu anauza IPOD mtaani au anataka kukuuzia or umepata fununu inauzwa sehemu naomba uni-PM or toa taarifa kituo cha polisi.......Nimefungua file pale Central na nina RB.....ninahitaji sana msaada wenu ndugu zangu maana hiyo IPOD ndiyo ilikua inanisadia kufanyia kazi zangu zote hata ku-browse hapa jamvini......natanguliza shukrani zangu kwenu nyote...

Kwa nini uliamua kuripoti vituo viwili tofauti vya polisi issue hiyo hiyo? Inawezekanaje vijana 50 wanakupora? Na wasiwasi kama unayoyasema ni kweli. Nitakupa pole baada ya kupata majibu ya kuridhisha
 
Kwa sisi wanasheria naona kama kuingia kichwani ngumu. Kwa mitaa ya metropole na makao makuu ya polis ar ni mita 400 so wangetiwa nguvuni faster na kama wanawaibia watu wameanzia mbali mpaka kufika so polisi wangewazibiti. Oky lakini nafsi yako inajua.
Mkuu kama upo maeneneo ya Arusha waweza enda uliza wale wanaofanya biashara ndogondogo kwenye hilo eneo or uliza wale waendesha pikipiki wanao park hapo permanent watakueleza tukio hilo maana waliliona...
 
No nimeibiwa jana jumapili jioni na nimeripoti jana hiyo hiyo mkuu.

ukiwa muongo usiwe msahaulifu. Pitia tena uongo ulioandika... Kama kwel walikupora ingebd wa ku cameroon ili uje kudanganya zaidi humu.
 
Kwa nini uliamua kuripoti vituo viwili tofauti vya polisi issue hiyo hiyo? Inawezekanaje vijana 50 wanakupora? Na wasiwasi kama unayoyasema ni kweli. Nitakupa pole baada ya kupata majibu ya kuridhisha
...Nilenda unga limited police kwa sababu lile kundi la vijana lilielekea huko na police walinambia nikafungue kesi Central maana eneo nililoibiwa lipo ndani ya kituo cha police central na sio Unga limited......nilifika vituo vya police viwili ila maelezo yangu nimendika kituo cha police Central peke yake...
 
Mkuu! Huyu aliyeibiwa labda ndiyo wale wale kwani kama wewe ni mgeni kwenye mji wa watu na akashindwa hata kutafuta mwanajamiiforums yoyote hapa A town na anajua kbs kwmb tupo tumejaa na angalia siku aliyeibiwa ni jumamosi ni wikiend yeye anaenda kutembea na vibegi vyake lain ile ambayo inarecord hapa A town,Acha aibiwe,Mkuu! Kama cyo namwogopa MUNGU ningekushauri usihangaike naye iwe fundisho afikapo Mikoani atafutage wenyeji. Huyu ni Shwain kweli!!
Sikubaliani nawe kabisa LiverpoolFc, kwanza elewa kutafuta wenyeji ni option. Halafu kuibiwa ni mkasa kama ilivyo mikasa mingine tu, hivyo ni bahati mbaya sana. Mkuu pole, tupo pamoja.
 
...Nilenda unga limited police kwa sababu lile kundi la vijana lilielekea huko na police walinambia nikafungue kesi Central maana eneo nililoibiwa lipo ndani ya kituo cha police central na sio Unga limited......nilifika vituo vya police viwili ila maelezo yangu nimendika kituo cha police Central peke yake...

pole mkuu naamini wanajamii walioahidi kukusaidia watafanya hivyo
 
mkuu! Huyu aliyeibiwa labda ndiyo wale wale kwani kama wewe ni mgeni kwenye mji wa watu na akashindwa hata kutafuta mwanajamiiforums yoyote hapa a town na anajua kbs kwmb tupo tumejaa na angalia siku aliyeibiwa ni jumamosi ni wikiend yeye anaenda kutembea na vibegi vyake lain ile ambayo inarecord hapa a town,acha aibiwe,mkuu! Kama cyo namwogopa mungu ningekushauri usihangaike naye iwe fundisho afikapo mikoani atafutage wenyeji. Huyu ni shwain kweli!!

poor thinking
 
ukiwa muongo usiwe msahaulifu. Pitia tena uongo ulioandika... Kama kwel walikupora ingebd wa ku cameroon ili uje kudanganya zaidi humu.

hahahahahaa!maelezo yamekaa kimagumash vibaka 50
aliripoti unga ltd
akafungua file central
lool
 
jamani bado ni meni rusha...we huo hata hajui tofauti ya ipad na ipod!!
 
Pole sana mkuu. Usikate tamaa manake vibaka wa Arusha wao shida yao huwa ni cash ya fasta.

Nakumbuka 2010 pia niliibiwa Sanawari kama wewe nikaripoti central na kukaa nikingoja.

Bahati nzuri wale vibaka shida yao ilikuwa ni cash, basi wakatupa pochi yangu na vyote vilivyokuwemo nashukuru Mungu wasamaria wakaokota na kupiga namba zilizokuwemo kwenye business card. Huwezi amini nilipata mali zangu zote isipokuwa pesa taslimu tu.

Just pray mabye kuna mtu ameiona hiyo Ipad yako anaweza kukupigia simu muonane akuletee.
Pole sana mkuu.
 
Nashukuru sana Mkuu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom