Wizara za Utamaduni, Elimu na Utumishi zakutana kujadili Maendeleo ya Kiswahili na Michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Makatibu Wakuu wa Wizara za Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamekutana kujadili maendeleo ya lugha ya Kiswahili na michezo Juni 8, 2023 Mtumba Jijini, Dodoma.

Lengo la kikao hicho ni kuweka mipango na jitihada za pamoja za kukuza na kubidhaisha lugha ya Kiswahili nje ya Tanzania.

Aidha, wamejadili juu ya kuboresha maendeleo ya michezo nchini kwa kuangalia changamoto zinazowakabili wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.

Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na kuhudhuriwa na Katibu mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Caroline Nombo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi pamoja na wataalam kutoka katika Wizara hizo.

IMG-20230608-WA0225.jpg
IMG-20230608-WA0224.jpg
 
Back
Top Bottom