Katibu Mkuu Yakubu amesema Wizara ipo mstari wa mbele kuhakikisha sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zinapata ufadhili

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa masuala ya ushirikiano kimataifa kutoka kampuni ya vinywaji vya Heineken Bw. Frank Ford ambapo wamejadiliana namna bora ya kushirikiana na kuendeleza Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao cha viongozi hao kimefanyika Agosti 30, 2023 katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana kutumia matukio ya Michezo na Sanaa katika kuwahudumia wananchi kupitia matamasha, mikutano mbalimbali, tuzo za michezo, tuzo za filamu, tuzo za muziki pamoja na uibuaji na uendelezaji wa vipaji vya michezo na Sanaa.

Katibu Mkuu Yakubu amesema Wizara ipo mstari wa mbele kuhakikisha sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zinapata ufadhili kutoka kwa makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuendeleza vipaji vya Sanaa na michezo nchini.

Kwa upande wake Bw. Frank Ford ameupongeza uongozi wa Wizara kwa kazi nzuri inayofanya kuendeleza sanaa na michezo nchini na kuahidi kampuni yake itaendelea kushirikiana na Wizara katika kuendeleza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

IMG-20230830-WA0135.jpg
 
Back
Top Bottom