Wizara ya Fedha haina Waziri makini. Tutakwama!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Katika wizara ambayo ambayo haikutendewa haki ni wizara ya fedha. Sijui mama Mama alikwambia wapi kumpa Dkt. Mwigulu Nchemba dhamana ya kusimamia wizara ya fedha. Sijui mamlaka zetu zilikwama wapi kumshauri Mama kuhusu uteuzi huu.

Wizara ya fedha inahitaji mtu smart ambaye amekua kwenye field ya uchumi na fedha muda mrefu, huwezi kumfananisha Dkt Mwigulu na Dkt Mapango ambaye alikaa kwenye field hii ya Management vya masuala mipango na uchumi wa taifa kwa muda mrefu, Dkt Mpango kwanza alikua ni Mhadhiri wa chuo kikuu huwezi kumfananisha na Mwigulu ambaye alikaa BOT kidogo akiwa mfanyakazi wa kawaida kisha akakimbilia siasa, Masters Degree na PhD zake amezipatia kwenye siasa, sasa huyu kweli atashauri nini? Anaelewa nini kuhusu uchumi wa taifa?

Kama kweli Mhe Rais Mama Samia ana dhamira ya kweli ya kujenga uchumi kwenye taifa hili aondoe wanasiasa aina ya Mwigulu kwenye Wizara. Wapo vijana ndani ya bunge ambao ni samart kwenye business and Economic fields, wamekua viongozi kwenye mataasisi makubwa makubwa ya kibiashara nchini, wengine wamekuwepo kwenye idara nyeti za uchumi serikalini. Mnalipoteza taifa kabisa kwa kukosa mtu sahihi wa kumshauri Mhe Rais.

Ndugu yetu huyu yeye ni kuwaza siasa 24 hrs, kila kukicha yeye anatafuta wafuasi kwenye siasa wamuunge mkono kwenye mbio za Urais, hawezi akawa smart kwenye kumshauri Rais mambo muhimu ya uchumi wa nchi.

Waziri huwezi ukawa na mpango wa Tozo ambazo unaamka tu na kuandika pasina kufikiria athari yake mbele ya safari, hufikirii ni vipi utaathiri utoaji wa huduma inakopatokana tozo. Hujafanya research kwa kujipa muda kuangalia response ya watanzania kwenye jambo husika, yaani hapa Mama alidanganywa sana amtengue aweke mtu smart mambo yaende. Ona sasa badala ya pesa zipatikane ziende kwenye miradi matokeo yake tunakaa tena kuanza kujipanga upya na Tozo kwa sababu ya uzembe wa mtu mmoja asiyejua smart.
 
Basi heri hata apewe Kimei

JK si alishawahi kumfukuza Mwigulu akiwa Naibu au?

Kuna mtu anakumbuka?
 
Kuna sehemu nimesema hili nikahisi watu hawajanielewa. Huwezi kuwa kada kindakindaki ukafaulu kama Waziri wa Fedha utachemsha tu. Uchumi hautaki siasa, numbers do not lie utaangukia pua ni suala la muda tu. Mfano mzuri ni namna alivyoreact kwenye hili tozo et ohh 'Wapotoshaji. blah blah

Hili la tozo linahitaji upotoshaji upi Mr mbunifu uchwara? Chukua simu tuma pesa data unazo mkononi kwamba kilichopitishwa na Bunge ni majanga matupu upotoshaji wa nn hapo?
 
Huyu haelewi kitu. Alienda nyumbani akawapanga Wanyiramba wenzake wakahojiwa na TV eti wanakubaliana na tozo ni za haki. Yaani huyu mtu kila kitu kwake propaganda na siasa hata kama ni mambo senstive.
 
Nijuwavyo mimi kuna vijana kama kina Godfrey Mwambie na wengine wako smart sana kwenye masuala ya kibiashara,kina mzee Kimei, wapo vijana walikua kwenye makampuni ya kishindani ya kibiashara yaliyofanya vyema unampaje Mwigulu wizara ya fedha?
 
Tozo kandamizi ya kibwenyenye kuwahi tokea nchi hii.

Magufuli ndio rais pekee wa wanyonge na hakuwafurahisha matajiri wengi mabwenyenye.
 
Huyu jamaa me sijamuelewa kabisa. Eti tujivunie kutoa sh 5 kama zaka kwa ajili ya taifa. Me haijaingia akili ila nimejaribu kukariri ili tu niandike uzi. Atakayepata nafasi ya kumshauri ashushe coment hapa yenye mashiko juu ya makato mapya na uamzi alioufanya anadai hawezi kuufuta.
 
Back
Top Bottom