MAGEUZI KWELI
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,947
- 253
Huu Msakata wa Mwakiembe na Sumu hauna Tofauti na Sakata za Posho za Wabunge, Huku wanasema approved na huku wanasema not yet na huku wanasema still pending ....Crzy
Mkuu Richard samahani usiseme hatuna jeshi la Polisi Tanzania, sema ndani ya jeshi la Polisi kuna wababaishaji na wanatumiwa!!!! Kama kungekuwa hakuna jeshi la polisi, wewe usingelilala nyumbani mwako, panapostahili kusifia sifia, polisi wapo na wanafanya kazi zao vizuri tuu!!!!!Mimi nilikwishazungumzia huko nyuma kuhusu hili jeshi letu la Polisi kwamba linahitaji kuundwa upya kabisa (from the scrach).
Tanzania hatuna jeshi la polisi lenye kufanya kazi yake kikamilifu bila uoga na kujituma. na hii ni kwa sababu ya mfumo uliopo ambao hauwapi nafasi.
Hili suala la uchunguzi juu ya ugonjwa unaomsumbua Dr Mwakyembe, halihitaji mijadala namna hii bali polisi walitakiwa wawe busy kushughulika na uchunguzi wa kina juu ya hali aliyonayo Dr Mwakyembe.
Ila ukweli unabaki palepale kwamba Tanzania yetu ya leo imezungukwa na kiza kinene chenye kutoa madudu mengi ya ajabuajabu ambayo yanamaliza kabisa jitihada zozote za wanaharakati.
SCREW 'EM! Serikali moja, chama kimoja, utawala mmoja lakini wanafanya kazi utadhani nchi ya wagagagigikoko na wale wa mgonenagonago!
Rais hajui anachosema Wazrii Mkuu, Waziri Mkuu hajui anachosema Rais, Spika hajui Rais alisema nini, Waziri hajui Waziri mwenzie amesema nini! Sijui wakiingiaga kwenye hivyo vikao vyao wanafanyaje kwa kweli!
Hivi huu mtindo wa viongozi wa nchi kuwa na double standard kwa kila kitu utahisha lini? Kauli mbilimbili tofauti toka kwa viongozi wakubwa wawili wa nchi ni aibu kwa nchi yetu jamani.Hivi kwanini hii serikali inashindwa namna ya kurekebisha hili? DCI Manumba kasema wizara ndio imewapa ripoti,ndani ya siku mbili Waziri mwenye dhamana ya afya anadai yeye hajui kuhusu hiyo report,Hii imekaaje wakuu?Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema suala hilo limezungumzwa na Manumba, hivyo ni bora atafutwe na kueleza ametoa wapi taarifa hiyo na kueleza kuwa wizara hiyo kwa sasa haina la kusema.
Ugonjwa wake umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amenukuliwa akisema ugonjwa huo umetokana na kulishwa sumu na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina ushahidi.
.....Sure Mkuu, nami niliwaza hivyo kuwa baada ya mtoto huyo wa kigogo kuhitaji hiyo ripoti ya ugonjwa, wajanja wa wizara ya afya wakafyatua ripoti feki wakakamata mshiko wao. Na kwa vile kulikuwa na lengo la kuichapisha ripoti hiyo magazetini-hususani gazeti la Mtanzania (kama ilivyodai Thread hiyo) na wao Mtanzania kuhofia masuala ya kisheria na kimaadili juu ya kuichapisha, huenda plan B ikawa ni kuwapatia Polisi ili waitoe kama matokeo ya uchunguzi! Na kwa vile polisi wetu ni polisi jina, pasipo hata kuingia deep juu ya reliability ya taarifa hiyo (bila kuchanganya na zao), wakajiona tayari wamesha-win, wakakurupa (kama alivyosema Mwakyembe) kuhitimisha kuwa HAKUNA SUMU!
Na bado, lazima ataibuka Mkubwa mwingine kuongezea utata juu ya hili.
Hiyo nina mashaka DCI Manumba and team wamechomekewa na mtoto wa kigogo aliyesemwa hapa JF anatafuta riporti ya Mheshimiwa Mwakyembe KWA GHARAMA YA TSHS40,000,000/=!!!!lol kwa hiyo Manumba na "vijana wake" wametumia mbinu za kijasusi kuzipata ripoti za wizara ya afya bila wahusika wenye taarifa kuwapatia au kujua .
Mkuu Richard samahani usiseme hatuna jeshi la Polisi Tanzania, sema ndani ya jeshi la Polisi kuna wababaishaji na wanatumiwa!!!! Kama kungekuwa hakuna jeshi la polisi, wewe usingelilala nyumbani mwako, panapostahili kusifia sifia, polisi wapo na wanafanya kazi zao vizuri tuu!!!!!
Nakubaliana na wewe Mtumishi Wetu! Lakini fikiria uonevu unaofanywa na Jeshi hili. Hapa tunazungumza jinsi wanavyojikanyaga kuhusiana na WAZIRI! Je ingekuwa ni mwnanchi wa kawaida, si wanadharau tu! Ona ni kesi ngapi ziko mahakamani, tena za shutuma kali dhidi ya watu fulani fulani. Huyu Manumba na mwenzie DPP na yule Hosea walifanya usanii mkubwa kwenye kesi ya Richmond, EPA na hatuna uhakika sana kama wale walioko mahakamani na gharama kubwa za kesi zile kwamba ni wahusika. Kwa namna hii unashawishika kuamini hawa mapolisi wetu wanatumiwa na wababishaji- ndio maana nimekubaliana na hoja yako.
Sitaki niamini kuwa jeshi la Polisi ndio linanifanya nilale kwa amani! Ukipata shida ukapiga simu- watakuja kwa wakati wao, watauliza maswali ya kijinga! Usingizi wangu ninahakikishiwa na ulinzi shirikishi katika maeneo yangu na hawa makampuni ya binafsi! Polisi wanaua hovyo hovyo siku hizi, bora lifute- ni kama hatuna Jeshi la Polisi Tanzania!
Mungu Ibariki Tanzania
Soma na Mwananchi ya leo pia ingawa limepanda bei. Mwakyembe alimalize hili lisije likammaliza kama Richmond ilivyomgeuka sasa.Nimeipitia hiyo habari mwanzo mpaka mwisho mara tatu, sijaona pahala Wizara ya afya ilipomruka Manumba.
Wacheni udaku.