Wizara ya Afya yamruka Manumba, wahoji alikoipata ripoti ya Mwakyembe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Afya yamruka Manumba, wahoji alikoipata ripoti ya Mwakyembe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 20, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu.

  Wizara hiyo imetoa kauli hiyo siku moja baada ya Dk. Mwakyembe kusema kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa feki kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua tangu Oktoba mwaka jana kuwa hautokani na kulishwa sumu.

  Dk. Mwakyembe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, alieleza kuwa alichokieleza DCI Manumba hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya hospitali inayomtibu ya Apollo nchini India na kuongeza kuwa sumu inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema suala hilo limezungumzwa na Manumba, hivyo ni bora atafutwe na kueleza ametoa wapi taarifa hiyo na kueleza kuwa wizara hiyo kwa sasa haina la kusema.

  Mponda alisema wizara kama wizara haihusiki katika suala hilo na kuongeza kuwa si haki kuzungumzia ugonjwa wa mtu hadharani. "Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi," alisema Waziri Mponda.

  Kwa upande wake, Manumba alisema taarifa aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuhusiana na ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ameipata kutoka kwa madaktari waliokuwa wakimtibu. Hata hivyo hakueleza madaktari hao ni wa hapa nchini au wa nchini India.

  Alisema kwa kuwa Dk. Mwakyembe anatibiwa kwa gharama za serikali, ni lazima madaktari wanaomtibu wafikishe taarifa hizo serikalini.

  Aidha alisema huu si wakati wa kubishana kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa suala hilo linahusiana na ushahidi zaidi, hivyo ni vema ukasubiriwa wakati utakapofika. "Faili tayari limekwishafunguliwa na limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hivyo ni bora mkasubiri upelelezi utakapokamilika na haipendezi kuendelea kuliongelea," alisema Manumba.

  Juzi akihojiwa na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Taifa kuhusiana na suala hilo, DCI Manumba alisema alichokizungumza kimetokana na madaktari, hivyo kama kuna uongo basi waliosema uongo watakuwa ni hao madaktari.

  Akizungumzia suala hilo juzi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk. Mwakyembe alisema taarifa halisi ya hospitali ya Apollo inatamka kuwa kuna kitu kwenye uboho (bone marrow) kinachochochea hali aliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaika kukijua, kukidhibiti na kukiondoa.

  Alisema kuwa anapata taabu kuamini kama DCI Kanumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yake au walisoma taarifa feki.

  Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema anachokiona sasa hasa kutokana na kauli hiyo ya jeshi hilo kuanza kuingilia kati na kutoa taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wakati bado hajamaliza matibabu ni mpango wa wazi wa mafisadi kuingilia kwenye suala hilo. Ameeleza kukerwa na tamko hilo la polisi hasa katika hali aliyonayo ya ugonjwa na kushangazwa na ufinyu wa uelewa wa jeshi hilo kusisitiza kuwa hajalishwa sumu wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru.

  Amesema amelishangaa jeshi hilo kujiingiza kulizungumzia suala ambalo takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati kulichunguza na kulituhumu kwa kulifanyia mzaha jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Dk. Mwakyembe alianza kuugua Oktoba mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa kwa matibabu kwa takriban miezi miwili. Alirejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

  Ugonjwa wake umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amenukuliwa akisema ugonjwa huo umetokana na kulishwa sumu na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina ushahidi.


  CHANZO: Tanzania Daima
   
 2. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Rafiki yangu mmoja alisema 'Of me eyes' akimaanisha 'Yangu macho'!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  SCREW 'EM! Serikali moja, chama kimoja, utawala mmoja lakini wanafanya kazi utadhani nchi ya wagagagigikoko na wale wa mgonenagonago!

  Rais hajui anachosema Wazrii Mkuu, Waziri Mkuu hajui anachosema Rais, Spika hajui Rais alisema nini, Waziri hajui Waziri mwenzie amesema nini! Sijui wakiingiaga kwenye hivyo vikao vyao wanafanyaje kwa kweli!
   
 4. kitonsa

  kitonsa JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Push up, samba soti, kichurachura, kavu, beki, round kick, sarakasi zinaendelea pale wasikilizaji
   
 5. F

  Flucytosine Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Movie ndio kwanza inaanza ngoja nivute kiti nikae vizuri,sterling ndo anapiga jalamba saizi,Tanzania hii sijui tushike lipi na tuache lipi,asante kwa taarifa mkuu.
   
 6. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Manumba ni vyema angejiuzulu.
   
 7. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wakiingia vikaoni,wanakunywa juice tu. Hasa ukizingatia waongonzwaji nao hawana la kusema, Viongozi wanapeta tu.
   
 8. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  kuna thread hapa iliandikwa,mtoto wa kigogo kanunua faili,so inawezekana Manumba kapewa second Version.Patamu hapo
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  Serikali taahira kwa mara nyingine tena yaonyesha utaahira wake. Manumba bila hata ya kumuhoji muhusika, madaktari waliomtibu, kusoma ripoti ya madaktari kuhusiana na mgonjwa wao na bila haya ya kuongea na maofisa wa juu wa Wizara ya Afya aliweza kusimama hadharani na kutoa kauli ya uongo kwamba Mwakyembe hajalishwa sumu.

  Sasa sijui kama Mkuu wake wa kazi atamuadabisha kwa kumfukuza kazi, lakini ukiangalia utamaduni wa Serikali hii taahira ni vigumu mno kumfukuza kazi mkosaji yeyote yule vinginevyo Ngeleja angeshashaulika katika baraza la Mawaziri kwa miaka mingi sasa, Mkullo naye angeshasahaulika kwa miaka mingi sasa kwa kutangaza bajeti za mwaka mzima ambazo baada ya miezi miwili tu tangu kutangazwa bajeti hizo Serikali huishiwa pesa au Hussein Mwinyi naye angeshashaulika kwani pamoja na kuahidi kutoa ripoti ya milipuko ya mabomu kule gongo la mboto na mbagala hadi leo hii ripoti hiyo badi imekuwa ni ya hadithini. Kwa hiyo Manumba naye pamoja na kuudanganya umma wa Watanzania ataendelea kupeta tu. Haya ndio matatizo ya kuwa na Serikali taahira ambayo haijui chochote kuhusu neno kuwajibika.
   
 10. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Katika sakata hili Manumba amejipambanua kama jitu babaishaji na jitu lisilo na upeo wala ujuzi wa kazi yake hata kidogo, kama upuupu alotuambia juzi ni matokeo ya uchunguzi wa kina kama alivyosema, basi uchunguzi wa kipolisi/intellejensia yao kwa ujumla wake ni upuuzii matupu. Yani kumbe akisema uchunguzi wa kina anamaanisha ni hearsay?? Naamani aliyempa Manumba nafasi ya uDCI aliangalia ukubwa wa kichwa tu. Manumba amelikoroga halafu anasema haipendezi kuendelea kuliongelea sakata hili, hivyo ni bora tusubiri upelelezi ukakamilika. Kwani wakati yeye anaongea na waandishi wa habari alikuwa hajui kuwa upelelezi haujakamilika???

  Hivi kuna taratibu gani za kisheria za kuwapandisha kizimbani watawala waongowaongo???Mana naona hawa wakina Manumba wamejifunza kwa wakubwa zao, Waziri Mkuu Muongo, Mawaziri waongo, Spika Muongo nani sasa tumwamini???Kila siku hawa wakina Manumba wanatudanganya maana wanajua wananchi hatuwezi kuwafanya kitu mana serikali imejaa mijitu miongo mitupu. Hakuna sheria ya kudeal na watu wa hivi wananchi tuchangie gharama za hizo kesi????au sisi kama raia hatuna haki ya kuwaburuza mahakamani watu wa namna hii??Hizo si ndizo sifa za watu wanaofanya ma fraud???hakuna kajikosa kweli hapa wanasheria tusaidieni tuwapandishe mahakamani hawa majamaa??

  KATIKA KATIBA MPYA LAZMA TU CRAFT MECHANISM YA KUDEAL NA MITAWALA MIONGO. HII INAKERA SANA, JITU TUNALILIPA MSHAHARA WA BURE MAANA LINAWATUMIKIA MAFISADI BADALA YA WALIPA KODI BADO NA KUTUDANGANYA LINATUDANGANYA.

   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mwisho wanatapika ukweli ndugu wasikilizaji
   
 12. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Tanzania Daima kagazeti ka propaganda ka chadema.

  someni muone maneno ya waziri mengine ya huyo mwandishi wenu.
   
 13. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mimi nilikwishazungumzia huko nyuma kuhusu hili jeshi letu la Polisi kwamba linahitaji kuundwa upya kabisa (from the scrach).

  Tanzania hatuna jeshi la polisi lenye kufanya kazi yake kikamilifu bila uoga na kujituma. na hii ni kwa sababu ya mfumo uliopo ambao hauwapi nafasi.

  Hili suala la uchunguzi juu ya ugonjwa unaomsumbua Dr Mwakyembe, halihitaji mijadala namna hii bali polisi walitakiwa wawe busy kushughulika na uchunguzi wa kina juu ya hali aliyonayo Dr Mwakyembe.

  Ila ukweli unabaki palepale kwamba Tanzania yetu ya leo imezungukwa na kiza kinene chenye kutoa madudu mengi ya ajabuajabu ambayo yanamaliza kabisa jitihada zozote za wanaharakati.
   
 14. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Dada siku ulikuwa ushaimaliza vizuri tu kwa kweli, ila sijui shetani gani kakusukuma ujambe mawazo yako usiku huu wa manane. Kwanini usilale tu dada yangu??Chadema katokea wap kwenye hii habari??Mbona chadema inawaumiza sana???kwanini upate shida si ujiunge na chadema tu nawe uwe huru kifikra??

  Kwako wewe taarifa ya Tamko la waziri wa afya, taarifa ya Manumba na ya Dk. Mwakyembe iliyoelezewa humu na Tanzania Daima ni ya Chadema??Je ulitaka magazeti yasiandike habari hizi ili yaandike habari zipi???Dada hebu lala kabla wengine hawajaanza kukushambulia kwa upuupu uliouweka hapa. Yaani umeweka maneno machache tu ila umaharibu, hivi ukijaza paragraph si itakuwa balaa humu?
   
 15. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kumnukuu Mzee Mwanakijiji, hii ndiyo 'clowns paradise'. Clowns katika hii nchi isiyo na jina wanaendelea na vituko vyao. Kuanzia clown mkuu na clowns wengine wote wanaomfuata wamebakia kuvutana pua zao na kubabaisha. Kinachosikitisha tu ni kuwa mchezo wao ndiyo mauti yetu!!!
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  lol kwa hiyo Manumba na "vijana wake" wametumia mbinu za kijasusi kuzipata ripoti za wizara ya afya bila wahusika wenye taarifa kuwapatia au kujua .
   
 17. Taahira

  Taahira Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwanini idara ya DCI isibinaifisishwe tuwe na chaguo kama vile KK Security dhidi ya Jeshi la Polisi?
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Thundering typhoons!..........
   
 19. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Sasa nini cha ajabu hapo? Guyz kwani hamuishi Tanzania? hata mitandaoni hamuingii?
  Hii Ndo Tanzania bana.., Mzee wangu MwanaKijiji hapa ni kweli kabsaaa., So sad to have such kind of Governace, gademu:smash:

   
 20. Taahira

  Taahira Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwanini Mkapa alibadilisha mawazo na hivyo kuharibu makubaliano ya hawa na Chadema kugombea kupitia Chadema 2005?
   
Loading...