Wizara ya Afya yamruka Manumba, wahoji alikoipata ripoti ya Mwakyembe!

Hapo lazima kuna kitu nyuma ya pazia...HAKUNA KINACHOJIFICHA CHINI YA JUA MILELE.
 
Sita, Mwakyembe, Manumba, Mponda, Pinda wote wapo kwenye timu ya JK. Kwa nini mtoe majibu tofauti kwa umma kwa suala moja? Hamuwasiliani wenyewe mpaka mkurupushwe na magazeti?
 
Serikali taahira kwa mara nyingine tena yaonyesha utaahira wake. Manumba bila hata ya kumuhoji muhusika, madaktari waliomtibu, kusoma ripoti ya madaktari kuhusiana na mgonjwa wao na bila haya ya kuongea na maofisa wa juu wa Wizara ya Afya aliweza kusimama hadharani na kutoa kauli ya uongo kwamba Mwakyembe hajalishwa sumu.

Sasa sijui kama Mkuu wake wa kazi atamuadabisha kwa kumfukuza kazi, lakini ukiangalia utamaduni wa Serikali hii taahira ni vigumu mno kumfukuza kazi mkosaji yeyote yule vinginevyo Ngeleja angeshashaulika katika baraza la Mawaziri kwa miaka mingi sasa, Mkullo naye angeshasahaulika kwa miaka mingi sasa kwa kutangaza bajeti za mwaka mzima ambazo baada ya miezi miwili tu tangu kutangazwa bajeti hizo Serikali huishiwa pesa au Hussein Mwinyi naye angeshashaulika kwani pamoja na kuahidi kutoa ripoti ya milipuko ya mabomu kule gongo la mboto na mbagala hadi leo hii ripoti hiyo badi imekuwa ni ya hadithini. Kwa hiyo Manumba naye pamoja na kuudanganya umma wa Watanzania ataendelea kupeta tu. Haya ndio matatizo ya kuwa na Serikali taahira ambayo haijui chochote kuhusu neno kuwajibika.


Umeuliza swali na kulijibu vema. Thanks
 
hivi inaingia akilini kweli kwamba Mwakyembe hajalishwa sumu...reference ikiwa ni ripoti ya madaktari ambao ndio kwanza wanahangaika kubaini tatizo...hivi jamani ripoti ya mwisho si ndio pengine itakua na majibu sahihi, sasa hii ya Manumba imetoka wapi?
 
Najarbu kufkria hatma ya maisha ya raia maskn, ilhal matajir na wa2 wenye dhamana bado wananyanyaswa
 
Najiuliza kama Dr Mwakyembe anaweza kuwashitaki hao jamaa kina Manumba - hata kama anasema hela/gharama za matibabu zinatoka serikalini, nijuavyo mimi hospitali haiwezi kutoa taarifa ya ugonjwa bila ridhaa ya mgonjwa!
Serikali taahira kwa mara nyingine tena yaonyesha utaahira wake. Manumba bila hata ya kumuhoji muhusika, madaktari waliomtibu, kusoma ripoti ya madaktari kuhusiana na mgonjwa wao na bila haya ya kuongea na maofisa wa juu wa Wizara ya Afya aliweza kusimama hadharani na kutoa kauli ya uongo kwamba Mwakyembe hajalishwa sumu.

Sasa sijui kama Mkuu wake wa kazi atamuadabisha kwa kumfukuza kazi, lakini ukiangalia utamaduni wa Serikali hii taahira ni vigumu mno kumfukuza kazi mkosaji yeyote yule vinginevyo Ngeleja angeshashaulika katika baraza la Mawaziri kwa miaka mingi sasa, Mkullo naye angeshasahaulika kwa miaka mingi sasa kwa kutangaza bajeti za mwaka mzima ambazo baada ya miezi miwili tu tangu kutangazwa bajeti hizo Serikali huishiwa pesa au Hussein Mwinyi naye angeshashaulika kwani pamoja na kuahidi kutoa ripoti ya milipuko ya mabomu kule gongo la mboto na mbagala hadi leo hii ripoti hiyo badi imekuwa ni ya hadithini. Kwa hiyo Manumba naye pamoja na kuudanganya umma wa Watanzania ataendelea kupeta tu. Haya ndio matatizo ya kuwa na Serikali taahira ambayo haijui chochote kuhusu neno kuwajibika.
 
Ukisikia UKENGE ndio huu. Serikeli moja tukio moja kila mtu aseme lake. Haya bwana Manumba taarifa yako umeipata wapi.? Mheshimiwa wetu bwana Kikwete una kazi kufanya kazi na watu wasiokuwa pamoja.
 
Mwakyembe akae kwa tahadhari sana kwani maisha yake yanawindwa kama pembe za ndovu, akizubaa tu wanamuua na Muvi ka kihindi linafikia the end.
 
......... ...... DCI Kanumba na wenzake ........... .... walisoma taarifa feki.Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema anachokiona sasa hasa kutokana na kauli hiyo ya jeshi hilo kuanza kuingilia kati na kutoa taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wakati bado hajamaliza matibabu ni mpango wa wa mafisadi kuingilia kwenye suala hilo.Ameeleza kukerwa na tamko hilo la polisi hasa katika hali aliyonayo ya ugonjwa na kushangazwa na ufinyu wa uelewa wa jeshi hilo kusisitiza kuwa hajalishwa sumu wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru........

BABA YETU ULIYE MBINGUNI NA JINA LAKO LITUKUZWE..... Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani hawa jamaa (police force) wanatumia nguvu bila akili kucheza ngoma wanayopigiwa na wale wanaowatumwa. Wanaonyesha ukaragosi wao, kucheza ngoma anayopiga mpuliza zumari.
Bila aibu na soni DCI ana dhalilisha cheo alichokuwa nacho. Inanifanya niwe na hisia kweli kwamba kuna mafisadi wanaotoa maelekezo ni nani azuliwe au afe.
- Utasikia wanasema mwenye ushahidi wa Kagoda waulete lakini wakati huo huo kuna kesi ya madai kati ya Kagoda na Manji. Hawawezi kuanzia hapo, na hiyo ndo 'clue' aliyowaambia Mwakyembe.
- Mtoto wa Mengi anabambikwa madawa ya kulevya, kuna maaskari wanatuhumiwa lakini hawakamatwi, na je hayo madawa waliyapata wapi? 'Clue' nyingine ya kupata source ya hayo madawa.
- Mwakyembe alimwandikia IGP a very detailed report kuhusu yeye (Mwakyembe) kusukiwa MPANGO WA KUULIWA KWA SUMU, hiyo report ilikaliwa na hakuna kilichoendelea KUNA NINI hapa. Katika report hiyo kuna watu wanokuwa implicated: EL na RA.
- POLICE, wanashindwa kuhoji kwa nini RA alikuwa anakana kuwajua wenye Dowans, lakini baadaye ikagundulika ni yeye mwenye power of attorney ya kampuni hiyo. Kuna nini police yetu?
Sasa waziri mwenye kuna na dhamana kawaruka pamoja na mgonjwa, aibu hamna au ndo mtafungua kesi za ajabu ajabu mlete ushahidi uchwara kwa sababu hiyo kesi itakwenda kwa mahakimu ambao nao maisha yao yana kashfa?
JIRUDINI JAMANI, hamko katika dunia nyingine, ni hapa hapa, mabo yakibadilika,Manumba utakuwa manumbu.
 
Hata Mwakyembe mwenyewe hajakiri kuwa alikula sumu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Amejitahidi tu kuonyesha kuwa ni jinsi gani Jeshi la Polisi halimpi ushirikiano.
Akiwa kama Kiongozi inabidi wangeongeas haya mambo katika forum zenye kuleta muafaka badala ya kutumia vyombo vya habari mara kwa mara hasa kuongelea afya yake.
Nadhani Jeshi la Polisi na Mwakyembe mwenyewe wanahitaji busara zaidi katika matumizi ya vyombo vya habari maana mwisho wa siku wataanikwa tu na hakutakuwa na mshindi.
Hata hivyo nachukia sana mtu kufa kusipo na ridhaa ya Mwenyezi Mungu!
 
Tutasikia mengi sn kwa hili,kila mwenye nafac ya kuongea ataongea lkn mwisho wa cku itafahamika tu kwan wakati wa mungu kutenganisha ukweli na uongo kuna watakao tafuta pa kuweka nyuso zao!
 
Naapa hawa jamaa tukifanikiwa mipango yetu lazima tuwaburuze The HAGUE(ICC),Hatuwezi endeshwa na vichaa wawili EL +RA.Wafuasi wao tutamalizana taratibu,lakini target hawa wawili tukiwapoteza kabisa TANZANIA itapata neema.Utajiri wa nchi hii umemezwa na wao,tupambane kama wazalendo ambao tumechoka maisha ya dhiki katika nchi tajiri.....
 
DCI amesema taarifa ameipata kwa madaktari wanaomtibu Mwakyembe, bila shaka doctors hao wako chini ya wizara ya afya. Swala ni kwamba Manumba anapata wapi nguvu kudai kuwa kama ni uongo basi madaktari ndio waongo. Vyovyote vile hii taarifa ya Manumba kuhusu Mwakyembe inamkanganyiko na kwa kweli kama alitumia vijana wake wa kazi kuipata basi lililkuwa tango pori., na ndio maana Mponda kamruka. Na kama ametoa taarifa chini ya shinikzo la mafisadi imekula kwao!
 
tanzania daima kagazeti ka propaganda ka chadema.

someni muone maneno ya waziri mengine ya huyo mwandishi wenu.

Acha kukurupuka we binti hii habari imeandikwa pia na gazeti la mwananchi. Hii nchi imekuwa kama toroli la miti, kila kiongozi anasema lake na wanakaa vikao kibao na kulipwa posho. Bahati mbaya kuna watu kama wewe mnatetea huu uvundo. Kuwa mzalendo ndugu yangu; Yanayofanywa na hawa viongozi ni hatari sana kwa usalama wa taifa.
 
hakuna jeshi la polisi TZ,kuna kikundi cha watu kinachoongozwa na watu fulani ndani ya Cham fulani.Kama kweli jeshi hilo lingekuwa linajua nini maana ya haki zao siku zote wangewalinda wanamapinduzi.FISADI AKISHAPATA ANACHOKIPATA SI RAFIKI YAKO TENA.
 
Back
Top Bottom