Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Mi maoni yangu kada ya udaktari imedominate wizara ya afya kimapato na kimuundo hata baadhi ya malipo sasa ni kama unyonyaji kwa kada nyingine ni muda mwafanya wizara ya afya kuleta usawa na mgawanyo sawa wa maslahi yanayozalishwa kwenye taasisi mbalimbali za afya

Au kuruhusu autonomous kwenye kada kila kada ijitegemee kimuundo na kimaamuzi
 
Wizard ya afya chukueni huu ushauri muhimu sana, Futieni usajili vituo vyenye hadhi ya Zahanati ambavyo vina watumishi wachache mfano kuna vituo kuna watumishi watatu

Naandika haya kwa sababu zifuatazo

1. Mgonjwa anatibiwa na timu, matibabu yake yanapaswa kupitia kwa wataalam mbalimbali mfano Tabibu, Mtaalam Wa maabara, Muuguzi , Mfamasia nk

Iweje Mgonjwa azikiwe na Muuguzi pekee, huu ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu,

Mgonjwa wa hivi vituo hatibiwi ipasavyo,

Bahati mbaya tumeziamini hizi Zahanati kutibu mamilioni ya watanzania waishio vijijini na kama hamjui zimesababisha madhara makubwa sana kwa watanzania,

2. Zahanati zenye watumishi wachache zimegeuka kuwa Mali binafsi ya wakuu wa vituo yaani, wengine wamezigeuza kuwa Saccos wanachuma pesa wanakopesha na kukopa wao,

Bahati mbaya sana hazisimamiwi ipasavyo, hawa mnaowaita makatibu wa afya na ma DMO kazi zao ni semina na safari hawana muda na maoni ya wananchi wanaopokea huduma mbovu na hata kama wakipokea hamna anayejali.

3. Watumishi wa Zahanati hizi ni kama wamekata tamaa, muda mwingi wanatumia kujaza makaratasi na kutekeleza majukumu mnayowapa kutoka huko juu kuliko kuwahudumia wateja.

Unaweza kuniamba ni vipi watumishi wawili kituoni wanaweza kujaza hiyo MITUHA yenu kwa usahihi ,fikiria Stoo ya dawa, njoo wagonjwa wa nje, RCH nk..yaani mnawarundikia mambo lukuki bila kujali uchache wao.

4. Zahanati hizi zina idadi kubwa ya vifo visivyoripotiwa, sisi tunaona nyie mpo mpo tu mnasubiri data, Watu wanafia majumbani kwa makosa ya wahudumu, niseme uwezo wa wahudumu wa Zahanati hizi kugundua tatizo mapema na kusaidia kwa haraka ni mdogo sana.

Tunapoteza wamama wajawazito kwa vifafa vya mimba , wazee kwa presha ambao unakuta walipita kimatibabu katika zahanati hizi wakaambiwa wanaumwa uti .

Ikiwezekana tuwe na vituo vichache vyenye wafanyakazi wa kutosha wanafanya kazi kama timu,

Zahanati awesome mhasibu, matabibu, wauguzi, wataalam maabara, angalau tutasema mtanzania wa chini anapata huduma bora na sio kituo wanakuwa watu wawili.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Niko na shida ya muda mrefu kupata choo kuna muda inakuwa kavu sana lakini pia mkojo nakojoa ila unatoka kwa unyonge sana, choo kubwa pia kuna muda napush mpaka naona sehemu ya aja kubwa inavimba kidogo kwa ajili ya kupush mzigo. Naomba anayejua ni dalili za nini anijuze
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Hiili laleseni za udaktari na utabibu kuchukulia Dodoma wote mliangalie vizuri halijakaa sawa, hasa kwa karne hii ya sayansi na teknolojia.Anngalau mngeligawa kikanda.
 
Juzi nimeenda hospitali moja binafsi kumpeleka mtoto wangu akiwa na severe constipation, akahitajika afanyiwe Enema. Lkn cha ajabu nikaambiwa NHIF doesn't cover Enema, yaana kale ka chupa cha dawa Enemax hakipo kwenye bima. I had to pay 20k huku roho ikiuma. Bima gani hata dawa ndogo hivi hazipo?
 
Imefika wakati sasa kuwe na mfumo mmoja wa Tiba kwa Hospitali zote za Serikali na Binafsi pamoja na maduka ya dawa ili kuwe na maelezo sahihi ya matibabu.

Kwamba history ya matibabu ya kila mtu iwe inajulikana na popote atakapokwenda iwe rahisi kufanyiwa FOLLOW-UP..

Kwasababu kumekuwa na matumizi mabaya sana ya BIMA hasa NHIF na matumizi ya dawa vile vile yanayofanya baadhi wa magonjwa kula dawa bila utaratibu..
 
Salaam.Ninatamani nikae kimya kwakuwa nilitoka salama lakini naona itakuwa ni dhambi maana kuna wengine wapo na wanaendelea kwenda.Dukuduku langu ni kuhusiana na namna mteja anavyohudumiwa na watumishi wanaoingia zamu za usiku katika kituo cha afya Pugu Kajiungeni.Hakuna kauli nzuri kuanzia kwa walinzi hadi madaktari.Nilishuhudia mlinzi anamfokea mzazi aliyejifungua kwa njia ya upasuaji kisa kamuomba azime au aoneshe wanapozimia feni kwa ajili ya usalama wa afya za watoto.Pili ukifika pale unaambiwa huruhusiwi kuwa na simu.Awali niliamini lengo ni zuri lakini baadaye nimeamini kuwa lengo ni kuficha maovu yao kwani wanajua namna wanavyofanya.Tarehe 24/3 /2023 usiku wa saa 3/4 kuna mzazi alijifungulia chini baada ya kilio na mateso ya muda mrefu na hata alipobeba vifaa vyake kuingia leba alifukuzwa atoke akafanye mazoezi kwakuwa tu wahusika wanahitaji muda mwingi wa kupiga soga na kucheza game kwenye simu zao.Muda mwingi wauguzi wako busy na simu zao hivo mgonjwa akihitaji huduma kwao ni kero.Ajabu zaidi ni wodi ya wazazi kukosa taa mpaka ninajiuliza Incharge wa kituo cha afya Pugu Kajiungeni anamajukumu yapi kama sio kusimamia huduma katika kituo hicho. Nina ushuhuda pia wa Amana na Cardinal Rugambwa lakini leo nimeanza na Pugu kwanza maana huduma zinahuzunisha.
 
Salaam
Kuna changamoto ya huduma za malipo ya Bima ya afya GEPG na malipo mengine ya serikali kupitia mawakala inaonyesha hakuna commission wanayopata kwa kupokea na kuwasilisha benki malipo hayo, kinachojitokeza ni kwamba mawakala wamekuwa wanakataa kupokea fedha kwa mteja ili kumwezesha apate risiti ya malipo! jambo hili limekuwa likileta usumbufu kwa wananchi. Serikali iangalie namna ya kuwezesha mawakala watoe huduma kwenye malipo ya serikali, hoja yao ni kwamba risiti zile wanazinunua lakni hakuna %inayorejeshwa kwao wakati wanapoteza muda katika kutoa huduma, gharama za roller na risk zinazoambatana na utunzaji fedha. Mkoa wa Songwe jambo hili limekuwa kubwa ukianzia makao makuu ya mkoa
Nawasilisha
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
MAZINGATIO KUHUSU BIMA YA AFYA"TOTO AFYA KADI"

Kuondolewa kwa bima ya TOTO AFYA KADI kunaweza kukarudisha hatari ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano,vilivyokuwa vimepungua kwa kiasi kikubwa sana,na moja ya sababu zilozochangia kupungua kwa vifo hivyo ni pamoja na mpango huu wa TOTO AFYA KADI.

Ushauri wangu wakati mnaangalia ustawi wa mfuko,pia mzingatie maendeleo ya jamii kwa vipato vyao,kwa gharama ya TOTO AFYA KADI ilivyokuwa ilisaidia watu wengi kumudu ,hivyo watoto wengi waliweza kupata huduma za kimatibabu kwa wakati tofauti na hapo awali.

kuondolewa kwa mpango huu kutafanya watoto wengi kutopata huduma ya matibabu kwa wakati kwa ukosefu wa pesa,au upatikanaji wa huduma hafifu kwa kuzingatia unafuu wa gharama ,hari itakayopelekea watoto wengi kupoteza maisha.
Binafsi naona ni wakati wa mifuko ya kijamii kujitathmini na kujua njia ipi sahihi ya kujiendesha badala ya kuhangaika,iwe sehemu ya kurahisha na sio kuweka ugumu,kuna njia nyingi za kudhibiti na kujiboresha lakini sio kuondoa huduma ambazo tayari ni msaada kwa jamii.
 
Vituo vya afya kweli mmjenga vingi,lakini sehemu zingine,wananchi wasita kuvitumia kutokana na gharama,mtu anaumwa kituo Cha afya Cha mpuguso huku Tukuyu kwa mfano,kumwona daktari eti 8000,mtu anasema Bora angenda moja kwa Moja duka la dawa nikanunue dawa za malaria tu,
 
Kituo cha Afya kumuona daktari 8000 Wapi uko mzee? Hiyo gharama sina hakika kama ipo kwenye vituo vyetu nchi hii.
 
Asante kwa kuwasiliana nasi.
Kupima Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (Covid-19) kwa Raia wa Tanzania ni Shilingi 40,000, raia wa kigeni ni USD 50$

Kwa nini Wizara msibebe hizo gharama ukizingatia hili ni janga la kidunia na serikali inatakiwa kuwa mstari wa mbele kulitokomeza haswa kwa kushawishi watu wapime bure, nashauri Wizara muondoe hizo charges za kupima au mpunguza walau iwe hata elfu mbili @ head.
 
Habari.! Mke wangu kaacha kutumia sindano za uzazi wa mpango ni miezi 6 sasa tangu aache kutumia mara ya mwisho alichomwa mwaka jana mwishoni lakini mpaka sasa haoni siku zake tatizo laweza kuwa nini? Naomba msaada.

Nb, Alikuwa anachoma kila baada ya miezi 3 na ametumia kama sindano 4 - 6

Wizara ya Afya Tanzania
 
Back
Top Bottom