Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nakazia hapa Wizara ya Afya Tanzania condom hazina ubora kabisa, wiki mbili zilizopita nimepatwa na hii kadhia, mzigo wote ukamwagika ndani
Pole sana mkuu,lakini pia nikuswalike kidogo
Ulifuata vizuri procedure ya uvaaji wa condom
Kama bado unaona kizunguzungu kunijibu
Tembelea kituo chochote cha Afya watakupa
Msaada mzuri sana kuanzia ufunguaji wa condom mpaka uvaaji lakini life span ya condom
Pamoja na storage ya hizo condom (Asante mkuu)
 
Hospital ya wilaya ya bagamoyo hakuna huduma za kiserikali Bali ni biashara ya watu binafsi,haiwezekani mgonjwa alipie kiingilio, anunue madawa, alipie vipimo,anunua kila kifaa tiba kitakacho hitajika.naomba kujua kama ndio utaratibu wa serikali Kwa Sasa
Asante.
 
Wananchi wako tayari Kulipia Bima,pelekeni Maoni kwenye Baraza la Mawaziri Ili kila mtu atoe 4,000 kwa kichwa kwa mwaka

Serikali inaweza pata Til.4 ambazo zikieelekwa kwenye dawa na vifaa tiba tunaweza kupata Bima ya Afya kwa kila mtu..

Bajeti ya kawaida ya Wizara iende kwenye Miundombinu na gharama za Kiutawala.
 
Napenda kuulizia yakua diploma ya radiology hapa Tanzania,inaaptikana vyuo vipi na je,ziko chini ya NactVet??
 
Wizara lipeni posho za kampeni ya polio

Wizara hii ya afya imeanza ufisadi na kuwanyanyasa watumishi wake naona waziri wake wanamdharau

kwanza madakatari vituoni wanapewa basket funds wanatumia hizo fedha watakavyo bila kushirikisha kamati za vituo/zahanati, stahiki za watumishi wa chini yao hawalipi kama extra duties nk.

Pili wizara imepanga utaratibu mbaya wa mtumishi kusaini fedha kabla ya kupokea kwa kuwa atatumiwa kwenye simu yake, leo zaidi mwezi hawajalipwa posho za kampeni ya polio,pia kuna posho za uviko zinaliwa vibaya na wakubwa kupitia NGO zilizopewa kazi hiyo kwani unasaini kabla, unashangaa wengine wanalipwa wengine hawalipwi japo wamesaini, kuna NGO za uzazi wa mpango mambo ni hayohayo.
 
H
Mimi niwapongeze sana wizara ya afya kwa mageuzi makubwa ya sekta ya afya nchini

1.Kumekua na madaktari bingwa wa kutosha pamoja na vitendea kazi vifaa tiba katika hospitali zetu za mikoa na rufaa

2.Kumekua na uboreshwaji mkubwa wa huduma kwa wagonjwa ( Customer care) siku hizi matusi, kupuuzwa na dharau kwa wagonjwa vimepungua sana kama sio kwisha kabisa

3.Kumekua na ongezeko la watendaji, maboresho ya hospitali, kujengwa kwa hospitali mpya na vituo vya afya kwenye kata zetu na vijiji, hata wale waliokua hawajui hospitali siku hizi wanazijua na wanapata huduma

4.Kumekua na uboreshwaji wa bima ya afya ya taifa. Siku hizi watu wa NHIF hatudharauliki kama awali. Nimeshuhudia mke wa ndugu yangu ambae mumewe ni mwalimu na yeye mama wa nyumbani akifanyiwa upasuaji wa moyo kwa kutumia NHIF bila kikwazo na kupona. Hongera sana MNH

5.Niseme pia kumekua na huduma bora zaidi hospitali za serikali na hospitali na mashirika ya kijamii/dini kuliko hospitali binafsi. Kwakuwa nyie ndio wasimamizi mtusaidie wananchi kujua tatizo ni nini. Kuna hospitali ambazo ukifika mjamzito kujifungua wanakushawishi kufanya upasuaji sijui hili limekaaje kiafya

Ushauri
1.Matibabu ni gharama sana na watanzania wengi hawana uwezo wa matibabu. Tunaomba nyie na NHIF muandae mpango mzuri na rahisi wa kila mtanzania kuchangia bima ya afya. Kama ilivyo Ile 50,400 kwa watoto basi angalieni watu wazima na familia wanaweza lipia kiasi gani kwa kila mwaka.
NHIF wakiweza kuweka njia rahisi na nafuu na kutengeneza mfumo ambao wananchi wengi watakua wanachangia itakua rahisi pia wananchi wachache wanaougua kutibiwa, kuliko sasa wanavyochangisha wananchi wachache na pesa nayo inakua chache kuwatibia wananchi wachache wanaougua

2.Kingine basi niwaombe mshirikiane na wizara ya elimu kuweka somo litakaloweza kubeba maadili na desturi za mtanzania na maisha yake. Vijana wetu siku hizi hawana jando na unyago, wazazi wote wawili wamekua watu wa majukumu mengi huku watoto wakiachwa wanajifunza toka kwenye t.v. na wasaidizi wa nyumbani. Ukitengenezwa mtaala mzuri wa kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne nina uhakika vijana wetu wanaweza kuwa taifa bora sana baadae. Tutaepuka hata watoto kuendelea kuharibiwa kwa kurubuniwa kwani wengi wanakua hawajui na wanafanyiwa mambo mabaya wakiwa wachanga sana hadi inapojulikana inakua basi tena

3.Wizara ya afya na elimu angalieni hizi boarding za watoto wadogo jamani na mkiweza mzifungie kabisa au pale penye ulazima kibali kitoke kwenu. Hainingii akilini mtoto wa miaka 2, 3, 4, 5, hadi 10 kuwa shule ya bweni. Malezi na matunzo ya awali toka kwa wazazi ni muhimu sana kwa mtoto. Wamama na wababa kwanini tunazaa halafu hatutaki kulea? Kweli baba na mama wanampeleka mtoto mdogo bweni, mtoto ambae hata kujifunika shuka usiku au kupiga mswaki hawezi!! Halafu wanakaa nyumbani, wanakula kwa amani kabisa na kulala?? Kuna visa vingi nimekutana navyo vya kuumiza sana toka kwa hawa watoto

Cc Wizara ya Afya Tanzania
Hapa pia, itakuwa nzuri sana kama Wizara itazungumzia suala la UNIVERSAL HEALTH COVERAGE yaani Bima ya Afya Kwa Wote! Wizara na Serikali kwa ujumla, mmekuwa kimya sana on this issue, KULIKONI!?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Tunaomba tawi la NMB Chanika
 
Wizara ya afya kuna kitu kipi kinaendelea kuhusu uviko 19hasa cha Jo yake?

Nusu saa imepita nimepokea sms ya kunipa taarifa kua mke wangu ameomba chanjo ya 1 ya uviko 19 kupitia kituo cha afya Malamba Mawili Dare es Salaam siku ya jana. (Ilhali tuko Mkoa tofauti na Dar). Dakika tano baadae imekua sms kua tayari ashapatiwa chanjo hio siku ya Leo na mkaleta na link ya kutizama kadi hio online na kuithibitisha kama ni halali.

Nilichogundua kuhusu taarifa ZA kadi hio baada ya kuifungua ni kua, tofauti iko kwenye jina La babu, namba ya simu ndio hio ya mke wangu, majina Mawili ya mwanzo yote ni yale yale, Taarifa ZA kuzaliwa kuanzia tarehe adi mwaka vyote ni vile vile.

Naomba msaada wenu wa ufafanuzi hiki ni nini? Au ndio kile nilichokisikia cha kuunda kadi feki (kumpatia mtu kadi asiechanjwa kwa taarifa ZA mtu mwingine?)

Niko tayari kutoa ushahidi wa hiki nilichokieleza kwa kupandisha picha hapa Ila wizara ya afya kwa hili mnajishushia hadhi
 
Watanzania wanaumizwa na gharama za huu za matibu huduma zikiwa hazikidhi ex:

Siku moja mke aliugua ghafla tukiwa mjini tulifika Hospital ya Sekou toure saa 9:00 am - hadi saa 19:30 pm jioni nilikuwa ni melipia zaidi ya Tsh 120,000/- dawa aliopewa ni vidonge visivyo zidi 12 aina ya dawa aliopewa maduka binafsi inauzwa @ tsh 2,000/- tangu asbh hakuwa amepewa dawa yoyote.Swali je Hosp za selikali kwanini gharama za matibabu juu na huduma haiwiane na gharama mgonjwa anazolipia?

Au Hosp za selikali kwa mini zisijifunze kutoa huduma bora na kwa wakati kwa kuangalia privety sector hospitals?
 
Nyie wizara embu badilisheni utaratibu wa vikao huku mahospitalini hasa vito vya afya na hospitali za wilaya, unafika hospitali saa mbili kamili halafu manesi na madokta wapo vikaoni hadi saa nne ndio nini sasa?
 
Mnataka maoni gani wakati hamna majibu ya changamoto za afya kwa wenye nchi! Kila kitu ni siasa tu chukueni maoni ya CCM tuache tuangaike muda ukifika tuwaondoe madarakani naninyi mkaonje hali ya kitaa.
 
Mh Ummy angalia gharama za matibabu JKCI , Consultation fee 35000
Echo, umeme moyo na stress umeme moyo 700000.

Kila dawa inauzwa zaidi ya mara mbili being za pharmacy za private
Ukiuguaa moyo Kama huna bima ni Bora ukaombewe kwa Mwamposya
Ruzuku mnaipa ya nini?
 
Kituo cha afya mbuguni iliopo wilaya arumeru mkoa wa Arusha ni kero sana
Wagonjwa tunateseka sana.
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom