Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Bodi ya Famasia watoke maofisini na kufanya kazi yao.

Maduka ya dawa yanauza dawa hovyo bila maelekezo yoyote. Leo nimenda pharmacy moja akaja Mmasai mmoja na kudai apewe "RANGI MBILI"za elfu mbili, akapewa amoxicillin bila kuulizwa na kuelekezwa lolote 😭
 
Bodi ya Famasia watoke maofisini na kufanya kazi yao
Maduka ya dawa yanauza dawa hovyo bila maelekezo yoyote. Leo nimenda pharmacy moja akaja Mmasai mmoja na kudai apewe "RANGI MBILI"za elfu mbili, akapewa amoxicillin bila kuulizwa na kuelekezwa lolote
Wivu kwa wafamasia bado inaendelea?

Na kama angemuuliza au kumuelekeza chochote ungekuja kulalamika ana ingilia majukumu ya DAKTARI
 
Bodi ya Famasia watoke maofisini na kufanya kazi yao
Maduka ya dawa yanauza dawa hovyo bila maelekezo yoyote. Leo nimenda pharmacy moja akaja Mmasai mmoja na kudai apewe "RANGI MBILI"za elfu mbili, akapewa amoxicillin bila kuulizwa na kuelekezwa lolote
Mwandishi pia anaonyesha, Ubaguzi wa Makabila, akiamini Masai ndie mtu pekee anaweza ibiwa kirahisi au kupewa vitu vya ovyo.

Hoja ya maduka ya Pharmacy au DLDM kutokufata Taratibu hiyo ni hoja mtambuka, hawapo kusaidia wapo kibiashara, that'll.

Serikali inahitajika kufanya Utaratibu mpya katika kusimamia haya maduka ya Dawa, maana watu wanaamini maduka kuliko kwenda hospitali...Hakuna Utaratibu uko madukani wa huduma kama hospitali.
 
Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.

Happiness, aliyejifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro alisema Oktoba 31 mwaka huu alipohisi dalili za uchungu alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alipofika alipokewa na wauguzi.
Hata hivyo, alisema alipopata uchungu hakupewa ushirikiano badala yake alijifungulia sakafuni.

Juzi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Itikija Msuya alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo akisema ameunda kamati ya kuchunguza ili kubaini kilichotokea siku hiyo.

“Kwa taarifa nilizopewa mtoto alizaliwa zero beating (akiwa amekufa) japo kuna dalili za uzembe ulifanywa na watoa huduma. Nimeunda kamati kuchunguza na watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Dk Msuya.

Akizungumzia hali ilivyokuwa, Happiness alisema baada ya kupokewa hospitalini hapo alifanyiwa vipimo vyote ikiwamo ultra sound na kuambiwa itabidi alazwe asubiri wiki moja iishe kama hatojifungua kawaida, basi atafanyiwa upasuaji.

Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.

Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake. Yule (muuguzi) niliyeenda naye akaniambia nifanye mazoezi ya kutembea, nikawa nafanya hivyo, baadaye hali ikabadilika damu zikawa zinatoka mabongebonge huku nikiwa na uchungu mkali.”

Alisema alipoona hali hiyo alikwenda chumba cha kujifungulia na kumwambia muuguzi aliyekuwepo kuwa anasikia kusukuma mtoto na anatokwa damu nyingi. “Yule muuguzi alinijibu umeweka pamba usije chafua kitanda, nikamwambia ndio nimeweka pamba lakini akaniambia niache kusumbua niendelee kutembea.”

Alisema wakati anarudi wodini kwenye kitanda alichokuwa amelala alishindwa kutembea na kumlazimu kukaa chini huku akiomba msaada kwa kuwa alikuwa akisikia dalili zote za mtoto kutoka na damu ziliendelea kumtoka.
“Manesi walikuja wakaanza kuniambia sukuma huku nikiwa chini sakafuni, nilijitahidi lakini nikawa nasikia nguvu zinaniishia, mmoja wa wauguzi akawa anamwambia mwenzake pokea mtoto si unaona kichwa kile pale.

“Mwenzake akamjibu hapana huyu hasukumi napokea nini? Nikiwa nimelala pale chini wao wako kwa pembeni wananiangalia huku wakiniambia sukuma kwa zaidi ya nusu saa nikajitahidi mtoto akatoka akaanguka chini ndipo wakamnyanyua na kuniwekea kifuani huku wakiniambia niheme kwa kuwa mtoto hakulia alivyotoka ila alianguka chini sakafuni.”

“Baada ya dakika tano bado nikiwa chini sakafuni wakaenda kumuita daktari, huku wanaendelea kumkagua yule mtoto baada daktari kuja ndio akawambia wanitoe pale chini ndipo wakaniweka kitandani na kuanza kunifanyia usafi.”

Mwanamke huyo aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wauguzi hao akidai kifo cha mwanaye ni uzembe wa wakunga na angepewa msaada wangeokoa mtoto huyo.
 
Kuna Jambo mi nashindwa kuelewa kwenye sekta ya Afya. Hivi kwanini kwenye hospitali zetu ukienda kutibiwa Mara nyingi utaambia dawa hamna kanunue kwenye duka la dawa, hapo utaambulia vipimo tu? Nashindwa kuelewa je duka la dawa linawezaje kuwa na dawa alafu hospitali zikakosa? Hii ni aibu Sana kwa sekta yetu jamani mbona Mambo ya hovyo Sana. Basi wekeni dawa mtuuzie kuliko kutusumbua wagonjwa kufuata dawa madukani?
 
Hospitali nyingi ukienda kutibiwa utasikia dawa hizi hatuna wanakula Panadol tu na dawa za kiholela, Sasa Kama kuwek dawa hawawezi si Bora watanzania tujue kuwa tunakuja kupima tu dawa tutajua wenyewe? Sekta ya afya haiko makini kabisa katika hili ni Mambo ya hovyo tu.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Kwa Sasa mnaifanya kazi yenu ipasavy na soon ntaonesha ushirikiano kupitia katibu
 
MAONI NA MAPENDEKEZO KUHUSU UTARATIBU WA MFUKO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE (UHC):

Huduma ya afya ni haki ya msingi kwa kila mtanzania. Ni wajibu wa serikali kuweka utaratibu wa kuwezesha kila mtanzania anapata haki hii ya msingi. The Healthcare must be easily accessible and affordable to every tanzanian.

Huko nyuma hadi mwaka 1998 huduma hii ilikuwa inatolewa bure na serikali kupitia bajeti ya serikali. Mwaka 1999 serikali iliweka utaratibu wa wagonjwa kuchangia kiasi kidogo cha gharama ya matibabu yao ie cost sharing. Kiasi hicho cha mgonjwa kuchangia kikawa kinaongezwa kila mwaka hadi kuwa kikubwa sana.

Ikawa tena siyo cost sharing but full cost. Sana sana mchango wa serikali ukabaki ni kulipa tu mishahara ya watoa huduma. Hadi sasa watanzania walio wengi (takribani robo tatu au zaidi) hawana uwezo wa kupata huduma hii. Our health care is no longer affordable to the majority of our people.

Leo hii watu wengi matumbo yao yakijifunga (bowel obstruction) wanakufa kwani gharama ya kuyafungua kwa operesheni ni malaki kama siyo mamillioni ya pesa. Leo hii matibabu ni kwa wale pesa, wale wengine wamebaki wakihangaika kwa miti shamba na tiba mbadala. They have been denied access to our health care.

Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) ulianzishwa kwa ajili ya watumishi wa serikali ili kutatua tatizo hili. Baadaye serikali iliruhusu mtu ye yote kujiunga na mfuko huo. Lakini gharama za kujiunga na mfuko huo imekuwa kubwa sana hususana full bundle ni TSh 1.5 milioni kila mwaka, kitu ambacho watanzania wengi hawawezi.

Matumaini yao yalikuwa kwenye uanzishwaji wa mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote. Walitegemea utakuwa kweli kwa wote lakini gharama ya kujiunga na mfuko huo ilipopendekezwa na serikali kuwa Tsh 350,000 kwa mwaka, matumaini yao yaliyeyuka.

Serikali inabidi ikubali kwamba watanzania wengi (over 70%) ni wanyonge ambao kipato chao kwa siku hakizidi dollar moja ya kimerikani. Na kwamba mfuko huu wa Bima ya Afya kwa Wote ni kwa ajili ya hawa wanyonge. Tungeweza kuuita Mfuko wa ya Afya kwa Wanyonge.

Mapendekezo
1. NHIF: iendelee kwa wale wenye ukwasi wanaohitaji fast track service au private service au VIP service. Mchango wake ubaki huo wa TSh 1.5 millioni kwa mwaka. Watumishi wa umma waendelee na mfuko huu kwa kukatwa mishahara yao na kiasi kinachobaki kwenye hiyo 1.5 milioni kulipwa na serikali kwenye mfuko huo.

Kwa wale VIP iwe TSh 3.0 milioni kwa mwaka. Makampuni binafsi na watu binafsi wenye uwezo washawishiwe kujiunga na mfuko huu.

Wenye bima hii wataweza kutibiwa hata kwenye private hospitals. Hizo bando ndogo ndogo kwenye mfuko huu ziondewe, ibaki full package na vip.

. Bima ya Afya kwa Wote
Baada ya zoezi la kisasa la sensa kukamilika, sasa tuna takwimu zote zinazohitajika kukokotoa kiasi cha kila familia au kaya tunachotaka wachangie kujiunga na mfuko huu. Tatizo hadi sasa National Beural of Statistics hawajaweka wazi mchakato mzima wa matokeo ya sensa. Hivyo nilizotumia hapa ni maoteo.

- Kwa mjibu wa sera yetu, wazee wa umri wa miaka zaidi ya 60, watoto chini ya miaka 5 na akina mama wenye mimba matibabu yao ni bure.

Serikali iwalipie Sh 30,000 kwa kila mzee, mtoto na mjamzito kwa mwaka kwenye mfuko huu wa bima kwa wote. Hivyo hivyo kwa kila kaya za TASAF. Nimeotea kundi hili litakuwa na watu au kaya million 5. Hivyo kwa mwaka serikali italipa kwenye mfuko huu Sh 30,000 × 5,000,000 = Sh 150 billion. Hili ni jukumu ambalo serikali na tuiombe isilikwepe.

- Kaya za wanyonge kwa maoteo ya sensa ya 2022 ziko 15 millioni ( bado NB haijatoa takwimu yake hadharani). Nimegawa hiyo population ya 61 million kwa 4. Hawa nao walipe Shs 30,000 kwa kila kaya kwa mwaka. Hivyo watalipa kwenye mfuko huu Sh 30,000 × 15,000,000 = Sh 450 billion.

-Hivyo jumla ya Sh 600 billion kwa mwaka zitalipwa kwenye mfuko huu kwa ajili ya matibabu ya magonjwa yo yote watakayopata wanyonge hawa katika hospitali na vituo vyote vya serikali. Bima hii si kwa kupata matibabu kwenye vituo vya binafsi.

Kwa kiasi hiki cha sh 30,000 kwa mwaka, kuna uhakika wa karibu kaya zote kuweza kulipa bima hiyo kwa hiari bila shinikizo wala tozo.

Sh 600 bilioni zitaweza sana kugharimia au kuchangia gharama za dawa, vifaa tiba, vipimo na operesheni zo zote watakazopatiwa kwani kiasi hiki cha pesa ni sawa na takribani theluthi mbili ya bajeti ya wizara ya afya ya mwaka huu wa fedha.

Tusisahau kuwa population kubwa ya Tanzania (90%) ni la vijana na hivyo ni wachache sana (<10%) watakaougua na kuhitaji matibabu. Ndiyo maana hata mlipuko wa ugonjwa wa corona haukutusumbua sana Tanzania maana sisi ni nchi ya young population.

Tuking'ang'ania kuwachangisha malaki ya pesa kila kaya ya hawa wanyonge uwezekano wa kukusanya hata billioni 50 ni mdogo sana uhakika hatutaweza kukusanya zaidi ya sh 10 billion na tatizo la ku deny access to health care to our people because of affordability will continue.

Mfuko huu lazima uwe full package na kusiwe na ubaguzi au unyanyasaji wo wote kwa wale wenye kadi ya mfuko huo kimatibabu.

CC: WAZIRI WA AFYA
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
kwenye vituo vya afya na hospitali muweke kondom za kike , maana saa nyingine unakuta unampa mwanaume mlevi hata kuvaa haewzi sasa nikiwa nayo navaa mapema kabla ya show.
 
Nimeumizwa sana na bima ya kibaguzi.

Ndugu yangu kapatikana na Kansa. Kataka kukata bima kaambiwa hata akikata bima hiyo inaishia kupata vipimo. Bali kama ana ndugu mwajiriwa wa serikali au shirika akiunganishwa kupitia hao atapata tiba.

Sasa huu si ubaguzi kuwa pesa hiyo hiyo second class citizen hapati Tina. Lkn pia hata akilipa kwa ajili ya vipimo anapaswa asubiri miezi 3.

Najua maana ya bima lkn hata kwa kansa inayohitaji matibabu ya mapema.?!?

Ni aibu kwa taifa kwani juzi nimesikia watendaji wa serikali wametenga sh 200bil kujenga arena. Shame on u watendaji wa serikali
 
Hospitali/zahanati za serikali huduma mbovu sana kwa sasaa.Hawajali wagonjwa kabisa......dawa unaambiwa hamna.
 
Kwa kifupi,

Mtazameni huyu Bwana aitwaye Robert Heriel. Ni mwanahudhuri hapa JamiiForums.

Maandishi au makala zake ni za Kudumaza. Zinahatarisha Usalama wa Afya ya Jamii.



Ni maoni yangu.Asanteni.
 
Hahaha eti wizara ya afya, ni watu tusio na pesa tu ndio tunakuja kwenye hospitali zenu. Hata mimi nikizipata hamtaniona tena huko vichochoroni kwenu
 
Bima ya afya ni mauaji ya watanzania kweupeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

mama Ummy take note of that! Hakuna mdigo hata mmoja atakaye afford pesa hizo (natolea mfano ndugu zako, but this applies to all tanzanians).

Rethink this death row!
 
Kama mmewaona watanzania ni wajinga na mnaamua kuwatupia kila kitu sawa haina shda

ila katika kitu ambachi hamtoamini kitatokea nyie ipitisheni hiyo BIMA YA AFYA KWA WOTE
 
Salaam

Naomba Kuuliza swali hili, MImi ni Mkazi wa Dar nina watoto 4 ...Kuna shida gani kwa wanawake asilimia 95 ya wakazi wa Dar wakibeba mimba hujifungua kwa upasuaji?? Je ni tatizo la tiba hafifu au ni maamuzi ya wanawake hao au ni kweli wote wana matatizo ya kiafya yanayoweza kuhatarisha usalama wao?? Ni kwanini Mkoa huu mmoja pekee na mingine haina shida hizo?? Katika Uzoefu wangu na watu wengi ninaowajua ikiwemo mke wangu tulienda Hospital mimba ya kwanza wakampasua ya pili tena...Ya 3 tukasema ajifungue huko vijijini akapush vizuri tu wala hakua na shida...Nauliza nyie Wizara mnajua hili wanaharibu wake zetu matumbo....
 
Salaam

Naomba Kuuliza swali hili, MImi ni Mkazi wa Dar nina watoto 4 ...Kuna shida gani kwa wanawake asilimia 95 ya wakazi wa Dar wakibeba mimba hujifungua kwa upasuaji?? Je ni tatizo la tiba hafifu au ni maamuzi ya wanawake hao au ni kweli wote wana matatizo ya kiafya yanayoweza kuhatarisha usalama wao?? Ni kwanini Mkoa huu mmoja pekee na mingine haina shida hizo?? Katika Uzoefu wangu na watu wengi ninaowajua ikiwemo mke wangu tulienda Hospital mimba ya kwanza wakampasua ya pili tena...Ya 3 tukasema ajifungue huko vijijini akapush vizuri tu wala hakua na shida...Nauliza nyie Wizara mnajua hili wanaharibu wake zetu matumbo....
Vyuo kaka wanafunzi weng wanakuwa wako field kwahyo ufanisi kwa kias fulani unapungua nimeumizwa mno na wife kujifungua kwa oparation na wakati dr mbobevu aliniambia kwa hali aliyokuwa nayo oparation haikuwa lazima basi tu kwasabab ya hosptal zetu wanafunzi weng ndo maana
 
Back
Top Bottom