Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Dkt. Gwajima D

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
543
3,575
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
 
Daktari karibu sana jukwaani na pia naomba nikupongeze sana kwa uamuzi wako uliouchukua kuungana na wana JamiiForums ili kuweza kupata mawili matatu kuhusu wizara yako...

Daktari ushauri wangu unalenga zaidi vituo vya kulelea yatima vingi vimekuwa ni miradi ya watu ya upigaji, watu wanaanzisha vituo vya watoto yatima lakini misaada inayotolewa ukweli ni kwamba haiwafikii walengwa.

Daktari ninaomba iundwe kamati itakayokuwa inapita na kufanya uchunguzi wa vituo hivi....kituo kitakachoonekana kina utata katika uendeshwaji wake kifungiwe na ikiwezekana kinyang'anywe kabisa usajiri...

Mfano kuna kituo kipo mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba mjini kinaitwa nusuru yatima association center hiki kituo ni miongoni mwa vituo vya watoto vyenye utata katika uendeshwaji na pia niko tayari kukupa ushirikiano wowote ule utakaohitaji kutoka kwangu.
 
Mh. Karibu sana... tunashida ya homosexual kwenye jamii na mashuleni kwa sasa.

Kama wizara mna kauli gani?

Mbili nini tathimini ya mitaala ya elimu ya msingi kwenye nchi yetu mpaka sasa hasa nimejikita kwenye malengo mahususi ni kweli yanafikiwa?

Asante.
 
Umefanya jambo jema kuanzisha mjadala huu....

Ila nafasi/cheo ulichonacho hapo wizarani, si nafasi ya kudumu! Maana ni mteuliwa wa Raisi!

Hivyo muda wowote aliekuteua akiamua....Unaweza usiwepo kwenye hiyo nafasi!

Hivyo kama ingependeza ungeanzisha page rasmi ya wizara kama wizara, na si kwa hii account Yako...

Ukianzisha page rasmi ya wizara kama wizara...page hiyo itaendelea kupokea maoni kama wizara hata pale utakapokuwa wewe haupo.

Hizo nafasi za kuteuliwa zinategemea sana maamuzi ya yule aliekuteua, ama wananchi waliokuchagua kama mbunge...then kuteuliwa kama waziri...

Hayo ni maoni yangu tu.
 
Daktari karibu sana jukwaani na pia naomba nikupongeze sana kwa uamuzi wako uliouchukua kuungana na wanajamii forum ili kuweza kupata mawili matatu kuhusu wizara yako...daktari ushauri wangu unalenga zaidi vituo vya kulelea yatima vingi vimekuwa ni miradi ya watu ya upigaji...
Ahsante Sana, nimepokea. Na kwa mawasiliano zaidi ya ushirikiano kwa maendeleo na ustawi wa jamii unaweza kunifikia kwa ujumbe kwenye 0734124191 au 0765345777 (tuma ujumbe nitakusoma). Ubarikiwe. Tunahitaji umoja wa jamii kwa maendeleo na ustawi wa jamii
 
Karibu Mh. Waziri, nakushukuru kwa kuwepo hapa JF kupata maoni mbalimbali na nikupongeze kwani huenda ndie Waziri wa kwanza wa serikali hii ya Mheshimiwa Mama Samia kujumuika na jamii hii ya wana JF.

Mimi naomba niwasilishe changamoto kuhusu ustawi wa watoto wetu katika jamii zetu. Watoto yatima na wazee wasiojiweza wamekuwa na shida kubwa wanapohitaji misaada ya matibabu ya afya.

Sera na miongozo ya matibabu ya kina mama wajawazito, watoto wadogo na wazee ipo lakini haisimamiwi ipasavyo katika ngazi za chini za huduma za afya kama vile zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya.

Watoto, wazee na yatima wanataabika sana na kupelekea kua omba omba. Maafisa Ustawi wa Jamii na wasimamizi wa huduma za afya hawajali kabisa. Wameingiza siasa na matokea yake, utendaji wao umekua hafifu.

Naomba uwepo mfumo wa ufatiliaji wa huduma za afya kwa makundi maalumu ya jamii, na mfumo huu uishirikishe jamii moja kwa moja, yaani viongozi wa kidini, viongozi wa kisiasa na wengineo wapewe nguvu ya kuwasimamia watoa huduma wa msingi katika vituo vya afya na hospitali zetu.

Ahsante.
 
Umefanya jambo jema kuanzisha mjadala huu....

Ila nafasi/cheo ulichonacho hapo wizarani, si nafasi ya kudumu! Maana ni mteuliwa wa Raisi!

Hivyo muda wowote aliekuteua akiamua...
Uko sahihi kabisa, nimeanzisha mwendo ku stimulate safari, wanakuja huko utawaona muda si mrefu, kisha na mimi nitawaaga kwa heshima na kuwaelekeza sasa karibuni huku ukurasa wa daima.

Lakini nao pia Wanapata moyo hata wakistaafu wengine wataona kumbe inawezekana.

Ahsante Sana kwa maoni yako, ubarikiwe 🙏🏾
 
Karibu Mh. Waziri, nakushukuru kwa kuwepo hapa JF kupata maoni mbalimbali na nikupongeze kwani huenda ndie Waziri wa kwanza wa serikali hii ya Mheshimiwa Mama Samia kujumuika na jamii hii ya wana JF.

Mimi naomba niwasilishe changamoto kuhusu ustawi wa watoto wetu katika jamii zetu. Watoto yatima na wazee wasiojiweza wamekuwa na shida kubwa wanapohitaji misaada ya matibabu ya afya.

Sera na miongozo ya matibabu ya kina mama wajawazito, watoto wadogo na wazee ipo lakini haisimamiwi ipasavyo katika ngazi za chini za huduma za afya kama vile zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya.

Watoto, wazee na yatima wanataabika sana na kupelekea kua omba omba. Maafisa Ustawi wa Jamii na wasimamizi wa huduma za afya hawajali kabisa. Wameingiza siasa na matokea yake, utendaji wao umekua hafifu.

Naomba uwepo mfumo wa ufatiliaji wa huduma za afya kwa makundi maalumu ya jamii, na mfumo huu uishirikishe jamii moja kwa moja, yaani viongozi wa kidini, viongozi wa kisiasa na wengineo wapewe nguvu ya kuwasimamia watoa huduma wa msingi katika vituo vya afya na hospitali zetu.

Ahsante.
Ahsante kwa maoni
 
Back
Top Bottom