Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ijajua kwa wizara ya afya lakin najua mpo pamoja na tamisemi kwa upande wa watumish wa afya jaman tusaidieni pesa za kujikimu tunakufaaaa🥹🥹
Msitufanyie hivyo pitien uko kwenye ma halmashaur watumishi wenu tunateseka tupo kama wagonjwa akati sisi ndo yapaswa tuhudumie wagonjwa.

Sent from my TECNO KI7 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Evening!!! Mimi Nina shida binafsi mnanisaidiaje nilifika dodoma kurekebisha mshahara wangu niliambiwa baada ya siku 21 nitapata majibu yangu,sasa nawaza ili swala nitafanikisha kweli kupitia kupiga simu naombeni mnisaidie kurudisha mshahara wangu ulisimamishwa Asante Nina imani mtanisaidia
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Katika hali ya kushangaza Mh Naibu Waziri wa Afya Mh Molleli alielekeza huduma za Hospitali ya rufaa ya Mkoa kuhama katika majengo yaliyokuwa ya kitumika hapo awali ambapo huduma za maabara na vipimo zilikuwa zinatolewa katika jengo lenye hadhi na vifaa vya kutosha. Matokeo ya kutekeleza maelekezo ya Mh Naibu Waziri Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa waliamua kuhamishia huduma za maabara na vipimo katika jengo ambalo ni jiko la kupikia na jengo la kufulia nguo kitu ambacho ni hatari kwa Afya za Wananchi.

Sio tu huduma za maabara hata huduma za kulaza wagonjwa waliopasuliwa na wagonjwa wa magonjwa ya ndani wanalazwa katika Korido na vyumba ambavyo sio wodi kitu ambacho ni hatari kwa afya za wananchi
 
Wizara ya Afya Malalamiko yangu ni kwa Hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza imekua ni chuo cha kujifunzia kwa wanafunzi wanaosoma hapo, Badala ya kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa. Mfano kuna wodi namba nane ukiona mgonjwa wako amepelekwa huko kata tamaa kabisa mana imekua sehemu tu ya kujifunzia kwa vitendo. Mgonjwa anakufa kwa njaa na kukosa huduma hii inaumiza sana.
 
Hii huduma ya toto afya NHIF wamefeli kwenye Promotion sasa wanaamua kuwafanyia ukatili watoto mfano leo hii makampuni makubwa tunaona Kila siku matangazo yao wakijitangaza tuchukulie Mfano Kama makampuni ya Simu ukiwasha radio/Tv haipiti dk 30 hujaona tangazo la Eidha voda tigo au Airtel,leo hii nani asie ijua kampuni ya Coca ila kila siku wanatangaza ukija taasisi za Fedha kama Mabanki ndo hadi yanaamua kwa sasa kuingia kwenye soka ili kuendelea kujipatia wateja...
unaweza kaa wiki nzima usisikie Tangazo la Bima unaweza katiza mji mkubwa usikutane na bango lolote la BIMA.....mfano leo mtu wa Kijijini ndani akihitaji Laini ya Simu msajili anakuja hadi mlangoni ila Bima lazima atasafiri si ajabu km zaidi ya 100 na anaweza fika akashinzdwa kamilisha mchakato siku hiyo hiyo ikambidi alale tena bado siku bima ikitoka inabidi asafiri tenaa..na hii elimu ya Bima Watanzania wengi mno hawana....Tatizo ni kuwa NHIF wanachukulia Bima kama msaada na Si Biashara wangeichukulia Kibiashara ingeenda...mimi nashauri kabla MAMA UMMY na anaejua Uchungu wa Mtoto hajafuta zilizopo na kuleta mfumo mpya Angeweka Benchi watu wa masoko walete ambao wataweza piga Promo na watakuja na mbinu mpya za usajili kama ilivo makampuni ya Simu..unasajiliwa popote sio hadi ofisini maana hata hii wanasema ya mashuleni mimi nina watoto wawili na wana Toto afya card zinaisha Mwezi wa 10 ambapo ndo nilipaswa kulipa tena ila shule wanazo soma nauliza Mwalimu mkuu anasema hajapokea mwongozo wowote na shule baadhi nimeuliza jibu ni hilo hilo hakuna mwongozo wowote kwahiyo bado tu watafeli tena....
nashauri wale watoto wenye BIMA waendelee kuzitumia BIMA zao alafu wizara ya Afya na NHIF waje na promo wapite kila kijiji kusajili watoto..watumie watendaji wa vijiji,Mitaa,walimu,vituo vya afya ambapo kuna kliniki yani mama ikibidi pale mama tu anapojifungua anapewa na Fomu ya BIMA ajaze pia wawe na Freelencers kama Mitandao ya Simu,,mbona kwenye kusambaza condom za bure inawezakana kufika pote au kwennye chanjo kama za Surua inawezekana Nchi nzima why NHIF washindwe??
... @ummymwalimu NHIFTZ @wizara_afyatz @samia_suluhu_hassan @gersonmsigwa @ikulu_mawasiliano @thebestfetty @masoudkipanya @malisa_gj
 
Mimi ni mwanachama wa NHIF,nimegundulika ni presha ya macho na kuandikiwa dawa mbili za kutibu, tatizo hilo 1).Dorzolamide hydro chloride &Timolol maleate eye drops 5mls-1 drop two times a day na 2).Latonoprost.0005%w/V eye drops solution I drop a day.
Uzoefu unaonyesha kuwa vichupa vya dawa hizi,hutumika kwa wiki 2 na humaluzika.Mgonjwa inabidi arudi clinic ya macho mara ya pili katika mwezi moja.Suala hili huleta usumbufu na gharama za usafi na muda kwa wagonjwa.
Ushauri
1).Wizara ya afya,iangalie uwezekano wa kutoa vichupa vya dawa hizo kwa mwezi mmoja badala ya wiki 2.
2).NHIF ifanye mapitio ya vitita vya dawa zinazotolewa kwa wateja wao.
3). kutokana na ukweli huo hapo juu,dozi ya ocudor-T ni 10 mils kwa mwezi badala ya 5mls na dozi latonoprost Ni 5 mls kwa mwezi badala ya 2.5mls.Wakati ni kweli tiba nyingi hutibiwa kwa kipindi Cha wiki 2, lakini ni dhahiri tiba ya presha ya macho inachukua kipindi kirefu kutibika.
 
Kwanini kupewa bima ya afya baada ya kuandikisha inachukua muda mrefu nini tatizo 2. Ikiwezekana OFISI ZA NHIF zichunguzwe kuna uzembe mkubwa sana unaofanyika humo ndani na pia hawajali wateja wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi Rapid test (HIV) zimekuwa adimu sana mitaani kwenye pharmacy mf Mji wa Kahama hakuna duka linauza kwa sasa!

Serikali ingefanya namna upatikanaji wake uwe rahisi kwa wenye uhitaji.
 
Kuondoka Bima Toto NHIF ghafla paap iliwaacha maelfu ya watoto katika shida kubwa. Wizara ilikurupuka Kwa maamuzi Bila elimu na utayarishaji wa Transition:

Kufuta Bima Toto ya 50000 na kuweka ya 120000 iambatane na mzaxi ya 240000 ni ngumu Kwa masikini Watanzania.

Pili: Maafisa wa NHIF wanasema ili upate Bima ya 50000 Kwa Mtoto, inakatwa Kwa makundi Shuleni. * Wizara ya afya ilipaswa kutoa elimu Kwa walezi au Wizara ya elimu..ili wazaZi wajiandae.

Kwa Nini NHIF isingetoa taarifa kwanza kwenye mashule?
 
Bima ya afya kwa watoto
Ili kuhimiza wamama kuzalia hospitali na kuondoa udanganyifu, kila mtoto anaezaliwa apate kadi ya Bima na akija clinik aandikishwe bima ya afya. Hilo litasaidia kuongeza mahudhurio cliniki pia
Badala yake Walifuta paap

Watoto wa TANZANIA jamani
 
aoni yangu kwa wizaraya afya hasa hospitali ya taifa Muhimbili
1. Kwanza nitoe pongezi kwa maboresho mazuri ambayo so far yanafanyika MNYONGE MNYONENI LAKINI SIF AZA KE MPE
2. Kuna sehemu za watoa huduma bado sana zinahitaji jicho la pili hasa WALINZI, WAKUNGA NK WALINZI WANA MAJIBU YA HOVYO SANA ESP PALE OUTPATIENT UNACHUKUA NUMBER KUAMKA SAA 10 ILI KUWAHU FOLENI YA NO HAKUNA MAELEKEZO MAZURI ESP KWA KADI ZA BIMA MARA UPANDE GOTROFANI KUPATA NO N AKUINGIZWA KWENYE SYSTEM DAKTARI AWEZE KUONA KERO WALE WA DADA NA KAKAS WANAONGEA NA SIMU NA KUTUMA SMS ...
3.mANESI KWA MADAKTARI KUPANGWA JINSI YA KUKAA DADA ANAKUKEMEA MPAKA UNASHANGAA KAMA VILE mUHIMBILI NI HYTT AU SERENA WAKATI KILA UMUONAYE ANA CHANGAMOTO
4.Prof Janabi ongeza uelewa wa huduma kwa hao wato huduma
5.MANESI MANESI MANESI HATA WODINI NIU KERO NAONA WENGI WAKO BILA WITO
 
Nipo tayari kuwatengenezea mfumo ambao mwananchi atakuwa na uwezo wa kufanya booking hospitalini kufungua faili na kufanya malipo ya awali akiwa nyumbani kwa simu yake. Hii itasaidia kupunguza foleni mahospitalini pamoja na Habari ya Rushwa. Pia itapunguza usumbufu wa kwenda hospitali kumuona daktari ambaye kumbe siku hiyo hayupo.

Ni wakati sasa wa sekta ya afya kutumia teknolojia ipasavyo.
 
Baadhi ya hospitali binafsi zimegeuza NHIF kama mradi wa kujipatia pesa na wakati huohuo kuhatarisha afya zetu wananchi! Mfano; nilikwenda hospitali X kupima UTI , majibu yakatoka naambiwa Nina UTI sugu na kupewa lundo la dawa, (sikutumia hizo dawa), kesho yake nikaenda hospitali Y ninayoiamini kutokana na uadilifu na weledi wao nikapimwa kipimo kilekile na majibu yakatoka nipo negative!
Tafadhali fanyeni utafiti!
 
Nipo tayari kuwatengenezea mfumo ambao mwananchi atakuwa na uwezo wa kufanya booking hospitalini kufungua faili na kufanya malipo ya awali akiwa nyumbani kwa simu yake. Hii itasaidia kupunguza foleni mahospitalini pamoja na Habari ya Rushwa. Pia itapunguza usumbufu wa kwenda hospitali kumuona daktari ambaye kumbe siku hiyo hayupo.

Ni wakati sasa wa sekta ya afya kutumia teknolojia ipasavyo.
Wasipokuelewa shauri yao. Wengine tumekuelewa!!
 
Kuondoka Bima Toto NHIF ghafla paap iliwaacha maelfu ya watoto katika shida kubwa. Wizara ilikurupuka Kwa maamuzi Bila elimu na utayarishaji wa Transition:

Kufuta Bima Toto ya 50000 na kuweka ya 120000 iambatane na mzaxi ya 240000 ni ngumu Kwa masikini Watanzania.

Pili: Maafisa wa NHIF wanasema ili upate Bima ya 50000 Kwa Mtoto, inakatwa Kwa makundi Shuleni. * Wizara ya afya ilipaswa kutoa elimu Kwa walezi au Wizara ya elimu..ili wazaZi wajiandae.

Kwa Nini NHIF isingetoa taarifa kwanza kwenye mashule?
KWANZA WIZARA YA UMMY INAONGOZWA NA WASIOMJUWA MUNGU KABISA.
UKISOMA CHATI YA BEI ZA UMMY ZA BIMA YA AFYA NDIO UTAMJUWA UMMY.
UMMY KWANZA ACHILIA MBALI KUAMINI, HAJUI KAMA NAYE AMEANZA KUZEEKA.
ANADHANI BADO NI MDOGO.
NA NADHANI KWA MUONEKANO WAKE, HUWA ANA AMKIA WAZEE KIPINDI CHA KAMPENI TU.
NDO MAANA ANAPENDA WAZEE WOTE TZ WAFE.
 
Back
Top Bottom