Wizara Afya mnajiandaaje na Umeme vijijini?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Ni kweli sasa hivi umeme unasambazwa hadi vijijini kwa kasi. Hii inamaana kuwa hata kule vijijini kabisa kutakuwa na umeme, lakini tunapofurahia faida za umeme kule vijijini lazima pia tusikitie hasara zake. Faida za kuwa na umeme zinafahamika sana hivyo sitahangaika kuzitaja hapa kwakuwa itakuwa kuwachosha tu bure. Mimi nitajikita kwenye hasara zake kama Wizara ya Afya haitatangulia mbele na umeme ukafuata nyuma huko vijijini.

Mara zote inafahamika kuwa vijijini kuna shida ya maji mengi na safi, vyoo, mifumo ya ukusanyaji taka, nyumba zenye hewa safi na idadi ndogo ya watumishi wa afya. Hii inasababisha watu wengi vijijini kuugua magonjwa ya kimaskini ya kuambukizana (communicable diseases) kama kuharisha, TB, upele, funza, minyoo, kichocho na mapunye. Maana yake wanaugua na kufa kimaskini.

Inafahamika kuwa nchi zilizoendelea na watu wa waishio mijini wanahangaishwa zaidi na magonjwa ya kitajiri yasio ya kuambukizana (non communicable diseases) kama vile kisukari, shinikizo kubwa la damu, kiharusi, uzito mkubwa na kansa, hivyo wanaugua na kufa kw magonjwa ya kitajiri.

Kupeleka umeme vijijini kunaamaanisha kuwa sasa hata wa vijiji watachelewa kulala, watanunua mafriji na mafriza na kunywa kwa vingi soda, ice-cream, bia, juice, maji baridi na viporo vilivyohifadhiwa kwenye majokufu. Wataacha kula matunda, madafu na vyakula vyao vya moto. Maana yake hata vijijini sasa rasmi watakuwa na bisababishi vya kuwa na magonjwa yasio ya kuambukiza kama kisukari, high blood pressure, unene uliozidi, mafigo, nk. Kwamaana nyingine wataanza kkugua kimjinimjini na kitajiritajiri pia. Kwakuwa vijijini hakuna maji mengi na safi, huduma za vyoo, huduma za afya za kutosha, huduma za uzoaji taka wataendelea kuugua yale magonjwa ya kimaskini ya vijijini (communinicables) na sasa wataongezewa yale ya kitajiri (non communicables). Yaani wataugua na kufa kimaskini na kitajiri kwa wakati mmoja,

Maana yake harakati za kupeleka umeme vijijini lazima ziende sambamba na utoaji wa elimu ya afya kwenye magonjwa yasioambukiza, utoaji wa maji na usafi wa mazingira, uboreshaji wa afya kinga kwa jamii, kuboresha mitaala ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya afya ili kukabiliana na ukweli huu wa kuongezeka kwa non-communicable diseases ndani ya jamii zetu.
 
Back
Top Bottom