Mwaka 2024 na dhambi ya umeme vijijini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Kazi ni kubwa imefanyika 2023 lakini ni kazi chafu kwa wanavijiji walio wengi.

Baada ya kupata umeme wanavijiji waliachana kabisa ghafla na utaratibu wao wa maisha waliouzoea. Ghafla walizitupa mashine zao za kusaga na kukoboa zinazotumia mafuta ya diesel, walitupa vibatali vyao na hata vinyozi walitupa zana zao za jadi za kunyoana wakanunua mashine za umeme. Lakini ghafla kumbe hakuna umeme wa uhakika, wanashinda na kulala na njaa kutokana na kukosekana umeme kwenye mashine za kusaga nafaka.

Serikali imepeleka umeme vijijini bila kupeleka elimu na huduma za kuzima moto wa umeme vijijini. Wanaunguza vitu vyao kila siku.
 
Back
Top Bottom