Twin Tower
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 2,129
- 2,982
Poleni sote kwa msiba wa Rais wetu mstaafu Mzee Mwinyi. Mungu ampumzishe kwa amani.
Kufuatia kifo chake pamoja na kuwa ameishi miaka 98 ametangulia na kuwaacha wake zake.
Hii imenifanya nitafakari siri ya maisha yetu wanaume hapa duniani. Inaonekana yameshikiliwa na uzi tu, muda wowote unakatika. Inatia hofu 🥲.
Mifano ipo mingi hasa kwa kufanya rejea ya viongozi ama watu maarufu. Kutaja wachache tu ni Rais Mwl. julius Nyerere, Rais Mkapa, Rais Magufuli, Lowassa, Mengi wa ITV n.k hata huku pia mtaani tunaona hii hali ikitokea. Hawa wote wamekufa na kuacha wake zao tena wakiishi kwa muda mrefu zaidi.
Je, kuna maagano yoyote yale yaweza kuwa kiimani ama ni nature tu imeamua kuamua?
Najua humu kuna wajuvi wengi na pengine tukang’amua hii changamoto inayotukumba wanaume.
karibuni kwa tafakari hii juu ya uhai wa maisha ya mwanaume hapa duniani.