SoC02 Wivu wa Mapenzi Unatumaliza

Stories of Change - 2022 Competition

Kilenzi _Jr

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
301
1,110
Miezi mitatu iliyopita nilikua nimekaa ofisini nikiwa naendelea na kazi zangu. Mara nikapokea ujumbe kutoka kwa rafiki yangu mmoja tuliesoma wote kuwa rafiki yangu wa karibu kajiua Kwa kujipiga risasi.

Ndiyo ni Davis kajiua kisa mapenzi baada ya kugundua mke wake anatoka nje ya ndoa. Davis alikua anafanya kazi mgodini pale Geita (GGM), Hivyo kulingana na kazi zake zilimfanya kuwa mbali na familia yake kwa muda mrefu.

Kitendo hicho kilinikumbusha maana sio mara ya kwanza kwa Davis kutaka kujiua, kwani mwaka 2021 alitaka kujiua kwa kujichoma kisu baada ya kukuta ujumbe wa mwanaume mwingine kwenye simu ya mke wake, ambapo Mimi pia nilikuepo katika harakati za kumuokoa asijitoe uhai baada ya kupewa taarifa na mke wake, kumbe sikumsaidia ipasavyo. Daah Davis!

Matukio ya kujitoa uhai kwa wanandoa kisa wivu wa mapenzi yanazidi kushamiri nchini kwetu, kwani Kila kukicha matukio haya yanazidi kuongezeka, Tanzania tumekosa hofu ya Mungu.

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO), asilimia 90 ya watu wanaotaka kujiua/kutoa uhai wa wengine, wamegundulika kuwa na matatizo ya akili na hii imekua zaidi kwa wanaume hasa wanandoa.

Lakini yote haya yanazuilika kwa jamii kupewa Elimu jinsi ya kuwagundua baadhi ya watu ambao wapo kwenye hatari ya kujitoa uhai au kutoa uhai kwa wengine kugundua makundi na dalili za awali mbalimbali kama; -

Hasira, Hofu, msongo wa mawazo uliokithiri, kuahidi kujiua au kuua mtu, kunywa pombe isiyo kawaida yake au kutumia madawa ya kulevya, makala zake kwenye mitandao ya kijamii, kutopata usingizi au kulala Kwa muda mrefu, kuacha kazi au kutokuwa makini na kazi, kujitenga na watu, kutoa au kuuza vitu vyake vya thamani pasipo na sababu ya msingi, kufanya uhalifu mfano kuua, kupoteza mtu wake wa karibu ambaye itampelekea katika msongo wa mawazo.

Yafuatayo yafanyike baada ya kugundua mtu akiwa kwenye dalili za awali;

1. Ongea nae.
Kabla hujaanza kuongea nae, unatakiwa utenge muda mrefu mzuri wa kuwa naye, ambao utaomba nafasi ukiwa umetulia maeneo yake ambayo anapendelea sana. Tumia muda huo kumjali na kumdadisi kiundani zaidi. Mueleze kuhusu mabadiliko yake unayoyaona mfano kunywa pombe sana, kutokuwa makini na kazi, kuwa na msongo wa mawazo n.k
NB. Kuwa makini pindi unapomdadisi usimkere.

2. Sikiliza, Eleza, Mtoe hofu.
Sikiliza; sababu za yeye kutaka kujitoa uhai/kutoa uhai wa mtu, onyesha kumjali Kwa kuguswa na matatizo anayoyapitia bila kumpinga wala kumlaumu. Mueleze kuhusu umuhimu wa kuishi au madhara ya kutoa Maisha ya mwingine na Mtoe hofu kuwa utakuwa nae bega kwa bega kumsaidia.

3. Tengeneza mbinu salama.
Muulize au dadisi lini ataweza kufanya tukio hilo na njia gani ambayo ataweza kutumia kujiua au kumuua mtu mwingine mfano, silaha, sumu, dawa n.k . Pindi baada ya kubaini njia hizo jaribu kutafta msaada wa karibu kwa ndugu yake au mwanafamilia kuhusu kuweka mbali vitu hivyo. Hii inaweza ngumu sana kukuambia ukweli lakini ukiwa upande wake lazima atakuambia.

4. Epuka hivi;
  • Usimlaumu kuhusu kitendo chake Cha kutaka kujitoa uhai au kutoa uhai wa mtu mwingine Kwani kweli yupo kwenye maumivu kulingana na alichofanyiwa.
  • Usiongee nae kwa ukali au kejeli, mfano aache ujinga wa kutaka kuendeshwa na mapenzi au "unataka kujiua? Jiue basi tuone"
  • Usimuahidi, kama akikuambia usimuambie mtu yeyote kuhusu kitendo chake atakachoenda kufanya, mweleze kuwa haupo teari kumwona anapoteza uhai wake kiurahisi au kupata madhara baada ya kutoa uhai wa mtu mwingine.
5. Msaada.
Omba msaada wa wahudumu wa afya wa jamii husika, Ili aweze kupata huduma zaidi na wataalamu wa afya na saikolojia.

HITIMISHO.
Wivu wa mapenzi umekuwa moja ya tatizo kubwa katika jamii zetu, ujumbe kwa wanandoa tuwe na hofu na Mungu Kwani uzinzi na kujitoa uhai au kutoa uhai wa mtu umezuiwa katika vitabu vyetu vyote vya dini. Pia kama mwanandoa haupo teari kuwa kwenye ndoa au haumpendi mwenza wako, ni bora usikubali kuingia kwenye ndoa kwani unajiweka katika hatari hii ya wivu wa mapenzi.
 
Tuendelee kupiga kura na kuchangia mawazo zaidi Ili tuweze kupiga vita hili suala la kujitoa uhai na kutoa uhai wa watu wengine
 
Back
Top Bottom