Maxence Melo
Kama inawezekana, uwekeeni pin huu uzi ili uweze kubaki juu wakati wote.
Ndugu wana diaspora wa Kitanzania, hususan kwenye nchi za Ulaya Magharibi, Scandinavia, Marekani, Canada, na hata Kenya pia, katika kuhakikisha tunamwajibisha Samia, tusimuache aishi wala kusafiri kwa faraja kwenda kwenye hizi nchi ambazo zinaheshimu haki za binadamu na zina uhuru mkubwa wa watu wake kujieleza.
Tuhakikishe kuwa, endapo itatokea huyu mtu anasafiri kwenda kwenye moja ya hizo nchi, basi Watanzania wote wapenda haki na walioumizwa na mauaji aliyoyafanya Oktoba 29, tunampa wakati mgumu sana kwa kuandamana alipofikia, atapotembelea, na popote pale atapoonekana akiwa huko.
Mimi na watu wangu tumeshajiandaa kikamilifu kuandamana na kumpinga, kumzomea, na kumfanya mengine ambayo kwa sasa ni siri yetu.
Hatutanii. Ajichanganye aje pande hizi aone. Huku hatuwaogopi hao wanaomlinda. Wakileta za kuleta, tutawapatia wanachokitaka.
Haiwezekani na haikubaliki kabisa aue Watanzania wasio na hatia yoyote ile kisa tu aendelee kutawala.
Hivyo basi, Watanzania muishio kwenye nchi za magharibi, jipangeni kwa namna muwezavto kumkabili endapo ataleta pua yake sehemu ambazo mpo.
Na siyo lazima muwe kwenye vikundi. Hata mtu binafsi tu unaweza kupanga jinsi ya kumkabili endapo atakuja sehemu ambayo nawe upo.
Wana diaspora hatuna kabisa sababu ya kumuogopa huyo mtu.
Yeye yupo upande wa uovu na sisi wema upo upande wetu. Na daima siku zote wema huushinda uovu.
Tumwandame huyu mtu mpaka awajibike.