Wito kwa wana CHADEMA wote!

chezea ben sa nane....na degree yake toka india kwenye maswala ya technology kamkamata samson mwigamba kiulaini kama kumsukuma mlevi
 
Nimekusoma mpaka mwisho. Kuna hoja japo unatakiwa kuleta data ili ziwe kamili. Kila mtu ana haki ya kukosoa. Lakini je, haya mambo hayakuonekana mapema? Isije ikawa mpango wa kuiua CDM kuelekea 2015. Kaofisi ka Kinondoni hakafai hakana hadhi.
 

Zito anautaka uwenyekiti sana
 
Naomba nipewe mbinu na mimi nithibitishe kama ni kweli id iliyotumika niya mwigamba,,msaada tafadhali
 
Kupenda ni ugonjwa mbaya sana, ukisha penda hata ukimfumania mkeo na jamaa kitandani jamaa Yuko juu, hutakosa sababu ya kumtetea, utasema tu: jamaa alikuwa amemlalia kwa juu ila hakuwahi kuingiza.

Body without head
 

Uwe utakaekuwa nakuhakikishia sisi Arusha hatuna huruma na upuuzi wo wote. Na Mwigamba kwa kukiri amejitenga na sisi keshakufa kisiasa ndani ya CHADEMA.

Nakuhakikishia kila masalia anapong'olewa panachipuka kitu kipya kinachoisukuma CDM kwenye mafanikio zaidi. Buriani Mwigamba
 

Well stated mkuu
 
Kwanini wafuasi wa CCM na anti CHADEMA wote wanataka uongozi wa CDM ubadilike?Wenye akili zetu tunajua kwamba huu ndio Uongozi utakaoipeleka CDM ikulu na kutuondoa kwenye utawala wa mkoloni mweusi CCM

Najiuliza mbona wanaosupport viongozi wa cdm watoke ni magamba na huyo Mwigamba tu wenyechama wenyewe hawanatatizo kabisa,kama uongozi no mbovu nafikiri ccm wangetaka uendelee ili chama kibomoke na wap ccm washinde kwa urahisi 2015 kama sivyo basi uongozi huu ni kichomi kwa magamba ndio maana yanaupiga vita.
 
Yenye ukweli yafanyiwe kazi kumsimamisha pekee haisaidii

Kwa nafasi yake kiuongozi alikuwa na nafasi ya kuyaongea haya ndani ya vikao vya chama, its insurbodination kwa kila mtu kuanza kujiongelea anavyotaka na akaruhusiwa, siyo sifa ya kiongozi makini mwenye kukitakia mema chama chake
 
Kiongozi wa Chadema akikosoa madhaifu anayoona anachukiwa. Ndio maana watu werevu wameshajua kuwa chadema haipo kwa ajili ya maslahi ya umma.

Chadema ni chama kinachoedneshwa katika misingi ya kilaghai...
 
ASIYE MUELEWA HUYU MASKINI MKULIMA BASI ANA PEPO LA UKAHABA, NA ASIYEMKUBALI HUYU MWIGAMBA BASI NA YEYE NI SHETANI mwenye nia ovu, ila bado sijaiafiki njia aliyoitumia, alitakiwa kwanza ajuuzulu vyeo vyote vya CHADEMA na kisha angeandika haya si kwa kutumia akaunti fake bali angeandika kwa utambulisho wake kamili.

Mimi bado naamini juu ya kutumia vikao vya chama, kama mawazo yako kwenye vikao hayaheshimiki na bado wayaona yako sahihi basi toka hadharani lakini kwa sharti ya kujiuzulu kwanza nyadhifa ambazo wazishikilia.

CHADEMA na TUBADILIKE SASA KAMA KWELI TUNATAKA kuwa watumwa wazuri kwa UMMA kinyume chake na sisi tutakuwa mafisadi kama CCM.
 
Ndiyo maana tunajitahidi kuwafungua wananchi macho kwa kuwaeleza ukweli kwamba CHADEMA ni chama cha kilaghai.

Mbona wanachama wenyewe hatusikii wakilalamika dhidi viongozi wa cdm,ni nyie magamba ndio mnaolalamikia uongozi wa fem,wakati adui yako muombee njaaa.
 
Mi sioni faida ya malumbano kwani mbuyu ulianza kama mchicha sasa basi kama uongozi unakosea, jambo la busara ni kuuonyesha kuwa unakosea na kutoa ushauri ujirekebishe vipi lakini kurukia kubadilishwa uongozi ni hatua ya mwisho ambayo mambo mengi mmeshashauri na hayakutendeka hii ni kama kweli watanzania tunahitaji mabadiliko ya uongozi kwani ndicho chama tunachoona kinaleta ufahamu na hata mabadiliko makubwa ndani ya nchi tuache ushabiki hao viongozi sio miungu wanakosea kwani ni binadamu so watanzania tufanye mambo kwa busara na kwa action sio longolongo...
 
Kwa nafasi yake kiuongozi alikuwa na nafasi ya kuyaongea haya ndani ya vikao vya chama, its insurbodination kwa kila mtu kuanza kujiongelea anavyotaka na akaruhusiwa, siyo sifa ya kiongozi makini mwenye kukitakia mema chama chake

Yawezekana kwenye vikao vya chama mawazo yake na mawazo kama yake yanapuuuzwa na kubezwa. Kwa nafasi yake aliyokuwa nayo ni mjumbe wa vikao vikubwa vya maamuzi,,,,kama ndivyo alitakiwa kusema yale huko,,,na kwa mtu kama Mwigamba na tukizingatia weledi wake huenda haya kayasema huko au alikwisha toa hoja hizi au kama walivyosema vikao chama vinapitisha mipango lakini haitekelezwi au inazimwa na watu aliowataja.

Sasa kama vikao vya chama haviheshimiwi kuna namna nyingine zaidi ya hii aliyoitumia? Mimi namlaumu endapo hoja zake hizi hakuanza kuziwasilisha kwenye vikao, lakini pia namlaumu kwa kitendo cha kuandika haya huku akiwa bado kiongozi, alitakiwa kwanza hajiuzulu na kisha ndio aseme yote yale akiwa na utambulisho wake kamili na si kwa kutumia ID fake.

WanaCHADEMA tusizibeze hoja za Mwigamba pamoja na kwamba ametumia njia chafu katika kuifikisha, tuko na wajibu wa kukitaka chama kuzifanyia kazi hoja za mwigamba, kinyume chake tutakuwa watengenezaji wa CCM mpya.
 
Mkuu, si morogoro tu bali hata kule mbeya tulisikia kuwa chadema walikuwa wanadaiwa pango la miaka miwili. Chama cha ajabu sana hiki. Akina mbowe kazi yao ni kuruka na chopa tu

Tunazijua mbinu zenu CHADEMA ITABAKI KUWA CHADEMA, unadhani mtaiua kirahis kama CUF..? sisi hatuta wasikiliza nyinyi mamuluki wa chama cha zamani, kauliyetu ni moja tu NCHI KWANZA, MAENDELEO KWA WOTE, CHUKI MWIKO. nawasihi makamanda wawe makini wasipotoshwe, SIASA NI MCHEZO MCHAFU.
 
...

......ARUSHA HATUNA MCHEZO TUKO KIKAZI SIKU ZOTE.....

Hata magamba wanalijuwa hilo........
 
[h=5]kamanda jiulize.

azimio la kuandika katiba mpya ya CHADEMA limefanyika 2004 na katiba mpya imepitishwa 2006.
inakuaje mtu amekua mwenyekiti wa mkoa wa CHAMA (CHADEMA) zaidi ya miaka 4 ahoji leo kuwa katiba iliyopishwa 2006 ilichakachuliwa.
...
bila shaka haya ni makandokando ya uchaguzi mkuu wa chama. Makamanda kuweni imara TUSIYUMBISHWE na wenyenia chafu na CHADEMA.

people's Power.[/h]
 
hao viongozi wa juu itabidi watoe ufafanuzi sio kum-discourage mleta thread
 
Uchozi mtupu. Kama Zitto ndo anatafuta uenyekiti ili atoe fadhira kwa CCM mwaka 2015 hapo amekwama. Mwaka 2015 chama kilikuwa kimefikia karibia kila mkoa na kilikuwa na viongozi wa kuteuliwa ngazi ya mkoa kwa asilimia 75. Leo tunaelekea kupata viongozi wa kuchanguliwa nchi nzima kuanzia tawi hadi Taifa kwa zaidi ya asilimia 90, hao waliokifikisha chama hapo ndio wanaoonekana hawafai kweli? Anayezua migogoro katika chama ndiye anaonekana ni muhimu? Nimeamini maneno ya akina nape na wenzake ambao lengo lake ilikuwa CHADEMA isifike 2015. Kwa hiyo naona mbinu nyingi zinazidi kutafutwa lakini, wale wanachama wa Chadema na watanzania kwa ujumla wenye nia njema na nchi hii, lazima watazame mambo haya kwa jicho pana. Quality
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…