Wito kwa wana CHADEMA wote!

Dec 27, 2011
27
38
Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wa chama.

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.

Naandika nikiwa mwana
CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Ni mawasiliano baina yetu wana CHADEMA na tunahitaji tutulie na kutafakari.

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika. Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio,
CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong'ang'ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwinginekidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kilamwanachama.

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.


Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49. Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzitoza kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao. Leo nitaainisha mambo machachetu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripotiza fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi yakakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwambakiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michangoya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni
questionable.

3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tuniliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka' kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, nahivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndotoya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari napikipiki zote za M4C.

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo Mwenyekiti Taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake yatenda. Huu si ufisadi ni nini?

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi namauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu.


Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama upinzani.

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.


Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetuwakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli piakwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapondipo mtakapojua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.

Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.

Ahsanteni kwakunisoma
!

------------------------------------

Kwa nini mabadiliko CHADEMA ni Lazima!

CHADEMA ilisajiliwarasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wenyeviti wa taifawawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Mzee Edwin Mtei aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 1993 hadi 1998 na kumwachia Mzee Bob Makani ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzonimwa 2004 na kumwachia Freeman Mbowe ambaye yuko madarakani hadi hivi sasa.

Mbowe aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwatena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili. Napenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wenyeviti wetu wote waliopita walizozifanya katikakuhakikisha chama chetu kinakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katikamazingira yaliyowakabili.

Mwaka 1995 chini ya Mzee Mtei tulipata wabunge watatu. Mwaka 2000 chini ya Mzee makani tukapata wabunge wanne mmoja wa viti maalum nakufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya Mbowe, tulipata wabunge watanowa kuchaguliwa na viti maalum sita jumla wakawa 11. Mwaka 2010 chini ya Mbowehuyo huyo, wakaongezeka na kuwa 23 na wa viti maalum 25 na kufanya idadi kuwa48 kabla ya kushinda uchaguzi mdogo Arumeru mashariki mwaka jana na kufanyasasa wawe 49.

Tunapopongezajuhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanzaambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badalayake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka nakimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga chamaimara kinachojali demokrasia na haki ya kila mwanachama. Ni kwa msingi huowaliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngaziyoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimojacha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili chamiaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ilealiyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kilewalichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwilivilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza natusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Napendakuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo:

Moja, wakatiKatiba ya CHADEMA ikifanyiwa mabadiliko mwaka 2006, mabadiliko hayo hayakugusakipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi yavipindi viwili vya miaka mitano mitano. Niliyaona makabrasha yaliyogawiwa kwawajumbe wa mkutano mkuu yaliyokuwa na mapendekezo ya Baraza kuu ya mabadilikoya katiba na mkutano mkuu kuyapitisha mapendekezo yale yote. Lakini wakati katibainachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwamakusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hikikinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanawezakutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika nawanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa chamachetu.

Vitainayoendelea leo kati ya Mbowe na Zitto ya kupigania uenyekiti wa chama katikauchaguzi ujao kiasi cha kuumiza chama, isingekuwepo maana Mbowe alikuwaharuhusiwi kugombea kwa mara ya tatu mfululizo. Kitendo cha Freeman Mbowekutaka kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha tatu mfululizo tofauti na msingiwalioujenga waliomtangulia, ni uthibitisho kamili kwamba kile kipengelekiliondolewa kwa maelekezo yake ili baadaye atakapotaka kung'ang'ania madaraka asionekaneanavunja katiba. Mbowe sasa anataka kuwa mwenyekiti wa design ya akina LyatongaMrema, John Cheyo, Chipaka, Makaidi, Mtikila, na kadhalika, jambo ambalo hatupaswikulikubali wana chadema.

Pili nambaya zaidi, anang'ang'ania madarakani wakati ambapo ameishiwa mbinu zakukikuza chama. Enzi zile za 2005 kuelekea 2010 chama kilikuwa kinaishi kwaissues, lakini leo kinaishi kwa matukio. Ni ujinga wa CCM tu kutupatia matukiolakini wakitunyima matukio chama kinakufa. Mbowe siku hizi anafanya kazi kwa kushauriwana vijana waliojaa mihemko kama Lema, Nassari, Wenje na Msigwa. Hawa hawanauwezo wa kukaa chini na kutengeneza mkakati (strategy) wa kuingiza chamamadarakani. Wanachojua ni kufanyia propaganda kila tukio linalotokea na kufanyamikutano ya hadhara, basi! Hatuwezi kuingia madarakani kwa mtindo huu. Hili waasisiwetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozikwenye mwongozo katiba ili kiongozi asing'ang'anie kuendelea kuongoza wakatiameshachoka.

Kuchoka kwauongozi wetu kunazidi kujidhahiridha katika mipango program mbalimbali za chamakwa miaka kadhaa sasa. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha Operesheni Sangara.Operesheni hiyo ilifanywa katika mikoa kadhaa ya kanda ya ziwa na hatimayeikafa kimya kimya. Hiyo ilikuwa ni baada ya kufa kwa program ya CHADEMA ni tawina CHADEMA ni msingi. Baada ya uchaguzimkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwayakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote.Kumbukumbu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwendakwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyikaMwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya,Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende.

Kisha mwaka2012 likaanzishwa Vuguvugu la Mabadiliko ama Movement for Change (M4C) Hiyoilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumlazilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia yamikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanyamafunzo kwa viongozi. Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kishaikaenda kufia Iringa. Mwaka huu 2013 viongozi wetu wamekuja na ugatuajimadaraka kutoka makao makuu ya chama na kupeleka madaraka kwenye kandambalimbali. Program hii ilikufa kabla ya kuanza pale Mwenyekiti Mbowe alipobadilishamaazimio ya Baraza Kuu na kutekeleza matakwa yake ikiwa ni pamoja na kuletasuala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri waratibu na maofisakama ilivyoazimiwa kwenye Baraza kuu la Januari mwaka huu.

Naamehakikisha anaweka watu wake kwenye uongozi wa muda katika kila kanda kwakuanzisha kitu kinaitwa kuzindua kanda ambacho hakikuwemo kwenye azimio laBaraza kuu na kimekula pesa nyingi kwa yeye mwenyewe kwenda kila kanda na timukubwa ya wakurugenzi na maofisa wa makao makuu waliolipwa posho na gharama zausafiri lukuki. Pesa hizo zilitumika kwa kiwango kikubwa wakati ofisi za kandahazina ruzuku tuliyoipitisha kwenye Baraza kuu na wala ofisi za mikoa, wilayana majimbo hazina hata shilingi ya kuendesha chama. Matokeo yake ni nini? Matokeoyake ni kwamba kile kilichopitishwa na Baraza kuu mwanzoni mwa mwaka ni hewa.Kama huamini tazama ratiba iliyopitishwa na Baraza kuu mwezi Januari mwaka huu:

Januari 2013: Vikao vya Kamati ku u na Baraza kuu. Februari20 13: -Kanda: Kuunda timu za operesheni na kutafuta nyenzo na fedha zaoperesheni, - Makao makuu: kuandaa vifaa, vipeperushi vya ujumbe wa operesheni,mfumo wa utoaji taarifa na mafunzo kwa timu za kanda. Machi 2013: Kutoamafunzo, kwa timu za operesheni za kanda, Kusambaza vitendea kazi katika kanda,Kuteua waratibu na maafisa wa kanda, Kupatikana kwa ofisi za kanda na kupatiwavitendea kazi. Aprili hadi Septemba 2013: Operesheni kikanda, chaguzi zamisingi, matawi, kata, majimbo na wilaya. Oktoba 2013: Kumalizia chaguziza majimbo na wilaya. Novemba 01 - 18, 2013: Chaguzi za mikoa. Desemba2013: Uchaguzi ngazi ya Taifa - Desemba 18: BAWACHA, Desemba 19:BAVICHA na WAZEE, Desemba 20: Kamati kuu, Desemba 21: Barazakuu, Desemba 22: Mkutano mkuu, Desemba 23: Baraza kuu jipya, Desemba24: Kamati kuu mpya. Nani leo anaweza kusimama na kubisha kwambatulichokipitisha kwenye Baraza kuu ni kiini macho kama leo mwezi wa kumitulikuwa tunatakiwa kumalizia chaguzi za majimbo na wilaya lakini hata misingihatujafanya uchaguzi?

Kitendo hiki kwa pekeyake, cha kufeli kwa kila mpango unaoletwa na viongozi wetu katika hatua zautekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mpango, ni kiashiria tosha kwambauongozi uliopo umechoka. Nimejitoa mhanga kuwaelimisha wanachadema kote walikoTanzania kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa kwenye uongozi wa kitaifa katikauchaguzi watakaoutisha iwe ni mwaka huu ama mwakani ama mwaka keshokutwa.Hatuwezi kuendelea na hawa watu. Tuwape nafasi watulie ili Mbowe afanye vizurikazi yake ya uongozi wa kambi ya upinzani bungeni na Dr. Slaa apate nafasinzuri ya kujiandaa kuja kuwa Rais wa Tanzania hapo mwaka 2015.

clip_image001.gif

Itaendelea juma lijalo…..

 
Nimesoma robo tu nikapata picha nzima! Kwamba CHADEMA imefikia hapa ilipo kwa kupiga vita ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali nk, pia nikaona kuwa umemsifia Mbowe na Slaa kwa kuwezesha chama kufikia hapa kilipo.

Ila PIA ume propose hao hao waliotufikisha hapa wasaidiwe kwa kutimuliwa! Sijaona ukionyesha sehemu yoyote kuwa vita yetu sasa imekwisha!!au tumeshinda ama tumeshindwa! Kama ufisadi umeisha nchi hii! Au kama rasilimali zetu sasa zinatumika vizuri ungepaswa kutuonyesha kuwa vita sasa imekwisha,na hivyo tuwapumzishe wapiganaji wetu, ila kama vita bado inaendelea,na wewe ukataka tuwakimbize wapiganaji wetu wa mstari wa mbele ambao umeukiri utendaji wao kuwa bora!! Ni kuthibitisha kiwango chako cha juu cha usaliti (kama ulikuwa kweli miongoni mwa wapiganaji) au wewe ni MAMLUKI usiyejitambua, angalau ungesema tuwa support ungekuwa na ka point.
 
Baada ya Video feki sasa mmekuja na la matumizi ya vyama. Nilikuwa naangalia walengwa ni kina nani katika hili, sasa nimetambua kumbe hapa yawezekana wanaolengwa haswa ni CHADEMA kupitia mamluki wao ambao pia wapo kwenye safu ya uongozi wa juu lkn pia wanakula sahani moja na CCM, wakuu wa kaya na wakuu wa intelijensia. Ngoja tuone safari hii mambo yatakuwaje. Hii ya sasa itakuwa kali zaidi. Lkn bado ninawasiwasi kama upande wa mamluki utashinda.
 
Acha kuwa muongo,
Kwanza, Zitto amekurupuka uwezi kusema tunazuia pesa eti kwasababu vyama vya siasa avijapeleka mahesabu, alipaswa kuwasikiliza kwanza ndo akimbilie kwenye vyombo vya habari kama alivyomsikiliza msajili wa vyama vya siasa na CAG ndio alitakiwa awasikilize na vyama vya siasa ndio aende kwenye vyombo vya habari.

Pili, kuna vyama vya siasa ambavyo vinasema vilikwishamkabidhi msajili wa vyama mahesabu yao, sasa inawezekana ccm ndio ambao hawakukabidhi kwa kuhofia chama tawala msajili ikambidi azuie na za vyama vingine ili ionekane ni wote na si ccm tu ambao hawajapeleka

Tatu, wewe si mwanachadema wa ukweli nimefuatilia mtiririko wa hoja zako nimeshindwa kuona mantiki ya hoja yako ina base wapi, ila kuna kitu nimegundua na napenda kusema kuwa. Ninachokiona ni kwamba unajaribu kushusha credibility ya viongozi wetu wa chadema lakini unasema kwenye uongozi kuna tatizo ila kama kna tatizo na zitto ni sehemu pia ya tatizo sasa mbowe anakuaje tatizo mpaka useme aachie uwenyekiti, na kusema kwamba zitto anafaa kuwa mwenyekiti mzuri. Huku ukiwa umeshasema kuna tatizo ila zitto anafaa japo na yeye ni sehemu ya tatizo

Mwisho, nilichogundua kuwa ukitakii mema chadema, na pia unapotosha umma, kwa sababu walichokilalamikia uongozi wa chadema ni kwamba wao hawana shida na walisha timiza wajibu wao kwa upande wa mahesabu, ila kauli iliyotolewa ya kusitisha ruzuku kwao ni kikwazo kwa kuwa izo fedha ni msaada katika shughuli za kichama sasa kama ccm hawajapeleka taarifa za mahesabu yao wote wasipate ruzuku mpaka ccm apeleke. maana ndio tafsiri ya zitto na wao walitaka kamati ikutane nao ili nao wasikilizwe then ndio uende kwenye maamuzi/
 
Sasa wewe mwanadamu kama ni kiongozi, wa chama umeshindwa nini kutaja jina lako hilisi ewe Mr Kiongozi? Si upeleke hasira za hoja zako huko kwenye chama chenu? Mianasiasa ya bongobana inachojua ni siasa za mtaroni, kuviziana na kutukanana tu,nyambaf kabisa.
 
ni wapi ambapo cdm imemsakama zitto kwenye haya mambo ya ukaguzi ? Vinginevyo tutakuchukulia kama mpiga porojo tu anayejitafutia elfu 7 kwa siku .
 
Lakini anayoyazungumza jamaa kama yana ukweli flani hivi ndani yake.

Unajua hapa Morogoro mjini maeneo ya Bigwa ninakoishi kuna Ofisi ya CHADEMA kata ya Bigwa ilifunguliwa na Dr Slaa miezi kama mitano hivi iliyopita cha ajabu ni kwamba sijawahi kuiona hiyo Ofisi ikifanya kazi yaani wakati wote imepigwa kufuri sasa ukiangalia na hizi tuhuma za kwamba kuna pesa zinatolewa kwa Vyama vya Siasa kwaajili ya kuendesha shughuli za Siasa Mikoani kwamba hazifiki na hazieleweki zinakwenda wapi zinanifanya niamini hizi tuhuma na kwa utaratibu huu sidhani kama CHADEMA tutaitoa CCM madarakani kama Viongozi hawa hawatakuwa tayari kuziwezesha Ofisi za Mikoani kifedha ili ziweze kuendesha harakati za kisiasa za Chama.

Viongozi wa Kitaifa wanapaswa ku-concentrate katika katika mambo ya Chama yaliyo na sura ya Kitaifa zaidi kama vile Viongozi wa Taifa wa Chama kujitokeza zaidi katika Media na kunadi mawazo na sera mbalimbali za Chama wakati Viongozi wa Mikoani wakiandaa mikutano,Semina & Makongamano mbalimbali ya kukieneza Chama
 
Mleta mada ni msaliti ama mwanaccm anayejisingizia kuwa ni Chadema. Mtu mwenye akili hubaini tatizo, chanzo na suluhisho. Wewe unashauri uongozi ung'olewe? halafu?

Jaribu kufanya utafiti mdogo tu n utaubaini ukweli.Kuna baadhi ya Ofisi za CHADEMA hapa Morogoro zimepigwa kufuri na tunasikia kwamba Chama kinapata fedha za kutosha sasa huwa zinakwenda wapi?WanaCHADEMA msijifanye wajinga kama wale wa CCM wasiotaka kushughulisha akili zao kufanya uchunguzi kubaini namna CCM ilivyo kikwazo kwa maendeleo ya Nchi hii.Uongozi huu wa CHADEMA una matatizo na ili CHADEMA tufikie malengo tuliyojiwekea ni lazima Uongozi huu wa sasa akiwemo Zitto mwenyewe ung'oke la sivyo Ikulu tutaisikia kwenye bomba.Kama kuna kitu ambacho kitaniumiza kweli moyo wangu basi ni kuiona CCM ikirejea madarakani 2015 ila kwa Uongozi huu wa akina Mbowe nina wasi wasi kwamba Watanzania tutaendelea kuongozwa na Mafisadi wa CCM.Akina Mbowe hamna kitu,Wanamharibu mpaka Dr Slaa.
 
Kazi tunayo...bado tuna safari ndefu, uliyeandika thread hii kama ni mwanachadema utakuwa mbaya kuliko hata mwanaccm, maana yeye tayari tunamfaham na tunatahadhari naye, wewe ni hatari kuliko hata mwigulu, unao uwezo wa kuua na kuzika mwenyewe



Kama kweli wewe ni kiongozi, nani amekwambia kuwa jf ndio kamati kuu ya CHADEMA?..unataka kusema kwamba masuala mhimu kama haya yanamalizwa jf, kweli wewe si mzalendo, ni msaliti mbaya kuliko kawaida, lakini hutashinda, sasa una viata na Mungu, atakushughulikia Mungu wa kweli..Mungu wa Israel, atashuka mwenyewe kukushughulikia
Tatizo lenu wafuasi wa chadema mnalewa viroba hadi uwezo wenu wa kufikiri unapotea. Hoja iliyotolewa ni nzuri sana. Mnapaswa kuitafakari kwa kina
 
Jaribu kufanya utafiti mdogo tu n utaubaini ukweli.Kuna baadhi ya Ofisi za CHADEMA hapa Morogoro zimepigwa kufuri na tunasikia kwamba Chama kinapata fedha za kutosha sasa huwa zinakwenda wapi?WanaCHADEMA msijifanye wajinga kama wale wa CCM wasiotaka kushughulisha akili zao kufanya uchunguzi kubaini namna CCM ilivyo kikwazo kwa maendeleo ya Nchi hii.Uongozi huu wa CHADEMA una matatizo na ili CHADEMA tufikie malengo tuliyojiwekea ni lazima Uongozi huu wa sasa akiwemo Zitto mwenyewe ung'oke la sivyo Ikulu tutaisikia kwenye bomba.Kama kuna kitu ambacho kitaniumiza kweli moyo wangu basi ni kuiona CCM ikirejea madarakani 2015 ila kwa Uongozi huu wa akina Mbowe nina wasi wasi kwamba Watanzania tutaendelea kuongozwa na Mafisadi wa CCM.Akina Mbowe hamna kitu,Wanamharibu mpaka Dr Slaa.
Mkuu, si morogoro tu bali hata kule mbeya tulisikia kuwa chadema walikuwa wanadaiwa pango la miaka miwili. Chama cha ajabu sana hiki. Akina mbowe kazi yao ni kuruka na chopa tu
 
Chadema lazima wakubali kukosolewa, kuna jambo la chadema kuwezesha ofisi zake za wilayani na majimboni muhimu sana! Kuna mikoa kama lindi, mtwara, ruvuma, iringa, rukwa na tabora, ni vizuri wakaiangalia kwa upana zaidi.
 
Uzuri ni kwamba wale viongozi wa chama mikoani, mawilayani, majimboni, wananielewa vizuri ninayoyaongea. Hawa walevi wanaoniita mamluki hawajawahi kuwa hata makatibu kata wa chama. Ndiyo maana sihangaiki kujibizana nao! Watu kama Tumaini Makene, ofisa habari wa chama badala ya kueleza jinsi chama kitakavyopeleka ripoti kuthibitisha usafi wake katika hili, anakimbilia kuanzisha thread ya kumshambulia Zitto kwa kashfa za uzushi. Na ndio mwamko ninaouona humu ndani. Nyinyi pigeni makelele halafu mtaona wenye chama watakachokifanya. Uongozi unaweza kufanya mazuri lakini ukifika mwisho huwezi kuulazimisha kuendelea. Marcio Maximo aliisaidia sana Taifa Stars, lakini ilifika mahali tukasema uwezo umefika mwisho aondoke. The same kwa Mbowe!
 
Maskini Mkulima, TECH WIZ, Chabruma, na nkongu ndasu, haya ni baadhi ya matamshi yenu;

  • Chama kinachoongozwa na mbumbumbu usitegemee kuwa kinaweza kukubali kukosolewa.
  • Chama cha ajabu sana hiki. Akina mbowe kazi yao ni kuruka na chopa tu.
  • Uongozi unaweza kufanya mazuri lakini ukifika mwisho huwezi kuulazimisha kuendelea.
  • Akina Mbowe hamna kitu,Wanamharibu mpaka Dr Slaa.
  • Tatizo lenu wafuasi wa chadema mnalewa viroba hadi uwezo wenu wa kufikiri unapotea.
Duh! Eti viongozi mbumbumbu, wafuasi walewa viroba! Kaazi kweli kweli!
 
Uzuri ni kwamba wale viongozi wa chama mikoani, mawilayani, majimboni, wananielewa vizuri ninayoyaongea. Hawa walevi wanaoniita mamluki hawajawahi kuwa hata makatibu kata wa chama. Ndiyo maana sihangaiki kujibizana nao! Watu kama Tumaini Makene, ofisa habari wa chama badala ya kueleza jinsi chama kitakavyopeleka ripoti kuthibitisha usafi wake katika hili, anakimbilia kuanzisha thread ya kumshambulia Zitto kwa kashfa za uzushi. Na ndio mwamko ninaouona humu ndani. Nyinyi pigeni makelele halafu mtaona wenye chama watakachokifanya. Uongozi unaweza kufanya mazuri lakini ukifika mwisho huwezi kuulazimisha kuendelea. Marcio Maximo aliisaidia sana Taifa Stars, lakini ilifika mahali tukasema uwezo umefika mwisho aondoke. The same kwa Mbowe!

Mbowe siyo kwamba amisaidia cdm tu, bali amechange sura nzima ya how politics is done in TZ, including ccm, bunge etc.

Acha kupiga kelele zako hapa, upinzani siyo lelemama, ukishindwa jiunge chama cha magamba.
 
"nilibahatika kushika nafasi mbalimbali ndani ya chadema"ina mana sasa hivi hupo ndani ya chadema upo wapi?kilichokutoa chadema ni kitu gani?lumumba boy kalale.
 
vijana wenzangu sometime inabidi tutulie na kujadili hoja na siyo kumattack mtu kiasi hicho au na nyie mmetumwa na hao waliotajwa kuivuruga hoja hii??? one purpose....one goal......
 
Lakini anayoyazungumza jamaa kama yana ukweli flani hivi ndani yake.Unajua hapa Morogoro mjini maeneo ya Bigwa ninakoishi kuna Ofisi ya CHADEMA kata ya Bigwa ilifunguliwa na Dr Slaa miezi kama mitano hivi iliyopita cha ajabu ni kwamba sijawahi kuiona hiyo Ofisi ikifanya kazi yaani wakati wote imepigwa kufuri sasa ukiangalia na hizi tuhuma za kwamba kuna pesa zinatolewa kwa Vyama vya Siasa kwaajili ya kuendesha shughuli za Siasa Mikoani kwamba hazifiki na hazieleweki zinakwenda wapi zinanifanya niamini hizi tuhuma na kwa utaratibu huu sidhani kama CHADEMA tutaitoa CCM madarakani kama Viongozi hawa hawatakuwa tayari kuziwezesha Ofisi za Mikoani kifedha ili ziweze kuendesha harakati za kisiasa za Chama.Viongozi wa Kitaifa wanapaswa ku-concentrate katika katika mambo ya Chama yaliyo na sura ya Kitaifa zaidi kama vile Viongozi wa Taifa wa Chama kujitokeza zaidi katika Media na kunadi mawazo na sera mbalimbali za Chama wakati Viongozi wa Mikoani wakiandaa mikutano,Semina & Makongamano mbalimbali ya kukieneza Chama

Hata za ccm hapa tabora mjini nyingine hazifanyi kazi maamuzi yetu ni kujaribu na ofisi nyingine hapa tanzania.....kwanini tuendelee kuwa conservatives.
 
Hata za ccm hapa tabora mjini nyingine hazifanyi kazi maamuzi yetu ni kujaribu na ofisi nyingine hapa tanzania.....kwanini tuendelee kuwa conservatives.

Point yangu ni kwamba badala ya Viongozi wa Kitaifa kupoteza mamilioni ya pesa katika Mikutano ya Hadhara kwanini pesa hizo zisielekezwe katika ofisi hizo za Mikoani ili ziweze kuendesha shughuli za uimarishaji wa Chama Mikoani.Najaribu pia kujiuliza busara iliyotumika ya Viongozi Makao Makuu kushindwa kuziwezesha Ofisi za Mikoani kifedha ili ziweze kusimamia zoezi zima la ukusunyaji wa maoni kwa Wanachama kipindi kile Vyama vya Siasa vilipotakiwa kukusanya maoni ya Wanachama wao juu ya Katiba kisha wayasilishe kwa Tume ya Katiba ya Jaji Warioba badala yake Viongozi wa Kitaifa wakadandia fursa hiyo na kujifanya eti wanakusanya maoni ya Watanzania wote na pia walijua fika kabisa kuwa Tume ya Katiba wasingeyapokea maoni hayo ila kwasababu hawakuwa wanazunguka bure bali kulikuwa na per diem wakaendelea na mipango yao kama kawaida.
 
Back
Top Bottom