Wito kwa wana CHADEMA wote!

Wito kwa wana CHADEMA wote!

Haya yote nataka kuyasikia baada tu ya CDM kuwa Ikulu late 2015. Tutaongea vizuri kuhusu katiba ya chama na wapinzani wetu ccm watatusaidia kujilekebisha vizuri wakati huo.
 
Mwenyekiti wa NGO na katibu wake huwa hawabadiliki, wanaobadilika ni wanachama tu. stukaaa!!!
 
Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wa chama.

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.

Naandika nikiwa mwana
CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Ni mawasiliano baina yetu wana CHADEMA [FONT=Book Ant UCHAMBUZI MZURI SANA NA WA KINA. LAKINI NI SAWA NA MAMBO YENU NDANI YA NDOA KUYAPELEKA KWA MAJIRANI. HAKUNA USHAURI WA MAANA UTAKAOPATIKANA, WENGINE WATAKUONA UMECHANGANYIKIWA, WENGINE WATAKUNG'ONG'A NA WACHACHE SANA WATAKUPA USHAURI WA BUSARA. MI BINAFSI NAKUPONGEZA KWA KUWA MKWELI KIASI HIKI, NI WACHACHE WENYE UTHUBUTU WA HIVI.
 
Umerudishiwa kompyuta yako...au umeazima/nunuliwa/nunua nyingine...maana taarifa zilizopo PC yako ilikuwa chini ya uchungunzi wa ITs wa CDM. Ila una hoja ambazo zinahitaji majibu makini....viginevyo msemo wa Wassira kuwa CHADEMA maji ya shingo unaweza uwe na mashiko, nisingependa hilo litokee.
 
kama angekuwa ni jk ana nyumba marekani, uingereza, afrika kusini, na dubai, cjui mngesemaje!! maana chadema kwa kujadili watu wengine ndo sera zao. na sasa mnamjadili zito, badala ya kujadili mapato na matumizi ya chama chenu. mkija kushtuka mmetafunwaaaa
 
kama angekuwa ni jk ana nyumba marekani, uingereza, afrika kusini, na dubai, cjui mngesemaje!! maana chadema kwa kujadili watu wengine ndo sera zao. na sasa mnamjadili zito, badala ya kujadili mapato na matumizi ya chama chenu. mkija kushtuka mmetafunwaaaa

JK maisha yake yote amekuwa ni mwanasiasa. Mbowe anafanya biashara maisha yake yote. Kama huna akili inayosukumwa kwa 7000 utaelewa tofauti zao. JK hajakatazwa kujenga hata Makka akitaka. Tatizo ni uhalali wa fedha za kujengea huko nje.
Ukikutana na ushahidi wa fedha haramu za Mbowe leta hapa jukwaani tumdadavue
 
Umerudishiwa kompyuta yako...au umeazima/nunuliwa/nunua nyingine...maana taarifa zilizopo PC yako ilikuwa chini ya uchungunzi wa ITs wa CDM. Ila una hoja ambazo zinahitaji majibu makini....viginevyo msemo wa Wassira kuwa CHADEMA maji ya shingo unaweza uwe na mashiko, nisingependa hilo litokee.

Usiseme ana hoja. Sema ana propaganda zinazohitaji majibu
 


Tunapopongezajuhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanzaambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong’ang’ania madaraka na badalayake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka nakimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga chamaimara kinachojali demokrasia na haki ya kila mwanachama.

Nadhani lazima kuna watu wana Nakala ya Katiba ya CDM ya awali kabisa! Hoja hii inaonekana imekaa kiumbeya -umbeya zaidi

Ni kwa msingi huowaliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngaziyoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimojacha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili chamiaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ilealiyoitumikia kwa vipindi viwili.
Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kilewalichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwilivilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.


Je 2006 Mwandishi alikuwa nani ndani ya CDM mpaka amekosa kuwa na nakala ya hicho anachodai kuiona!
Kweli unaweza kutoa tuhuma kubwa kama hii bila vidhibitisho?.
Ni mjinga tu anayeweza kuamini hoja ya aina hii tena toka kwa mtu mwenye akili ambayo wengi wanaimani na uwezo wake.

Moja, wakatiKatiba ya CHADEMA ikifanyiwa mabadiliko mwaka 2006, mabadiliko hayo hayakugusakipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi yavipindi viwili vya miaka mitano mitano. Niliyaona makabrasha yaliyogawiwa kwawajumbe wa mkutano mkuu yaliyokuwa na mapendekezo ya Baraza kuu ya mabadilikoya katiba na mkutano mkuu kuyapitisha mapendekezo yale yote. Lakini wakati katibainachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwamakusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hikikinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanawezakutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika nawanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa chamachetu.



Hapa/na hasa aya hii Kama kweli mwandishi na ikadhibitika kuwa ni Kiongozi wa CDM kamati ya Nidhamu na shauri isirudi nyuma kwa namna yoyote ile ni lazima afukuzwe Uongozi wa CDM na hata kama ataomba radhi aina ya watu kama hawa hawafai abaki kuwa mwanachama wa kawaida si chini ya Miaka saba.



Pili nambaya zaidi, anang’ang’ania madarakani wakati ambapo ameishiwa mbinu zakukikuza chama. Enzi zile za 2005 kuelekea 2010 chama kilikuwa kinaishi kwaissues, lakini leo kinaishi kwa matukio. Ni ujinga wa CCM tu kutupatia matukiolakini wakitunyima matukio chama kinakufa. Mbowe siku hizi anafanya kazi kwa kushauriwana vijana waliojaa mihemko kama Lema, Nassari, Wenje na Msigwa. Hawa hawanauwezo wa kukaa chini na kutengeneza mkakati (strategy) wa kuingiza chamamadarakani. Wanachojua ni kufanyia propaganda kila tukio linalotokea na kufanyamikutano ya hadhara, basi! Hatuwezi kuingia madarakani kwa mtindo huu. Hili waasisiwetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozikwenye mwongozo katiba ili kiongozi asing’ang’anie kuendelea kuongoza wakatiameshachoka.


Hivi unaweza kujitoa muhanga nyuma ya pazia na ukaaminika!

Nimejitoa mhanga kuwaelimisha wanachadema kote walikoTanzania kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa kwenye uongozi wa kitaifa katikauchaguzi watakaoutisha iwe ni mwaka huu ama mwakani ama mwaka keshokutwa.Hatuwezi kuendelea na hawa watu. Tuwape nafasi watulie ili Mbowe afanye vizurikazi yake ya uongozi wa kambi ya upinzani bungeni na Dr. Slaa apate nafasinzuri ya kujiandaa kuja kuwa Rais wa Tanzania hapo mwaka 2015.

 
hizo ni hadithi za bunuasi or fisi na sungura, Chadema ata wabunge 25 hawatafika na amini majimbo yote ya mjini yanaludi Ccm. kufanyika kwa uchaguzi chadema ni lazima kumbukeni Chadema ni Taasisi, lazima uchaguzi uweopo.

Ccm wanahangaika sana lakini mbowe na dr slaa sisi kama Chadema tunawakubari nyinyi mbulula semeni lakini wataongoza mpaka ushindi 2015
 
Chadema lazima wakubali kukosolewa, kuna jambo la chadema kuwezesha ofisi zake za wilayani na majimboni muhimu sana! Kuna mikoa kama lindi, mtwara, ruvuma, iringa, rukwa na tabora, ni vizuri wakaiangalia kwa upana zaidi.
Mimi nadhani fedha wanazopata CDM ni chache sana kulinganisha na mahitahitaji ya kuhudumia ofisi za wilayani. Sisemi hawatakiwi lakini nadhani hata hizo ruzuku hazitoshi. Kama tunataka wilaya na mikoa ihudumie ofisi zake vizuri lazima wanachama wilayani na mikoani wajitolee. Nadhani fedha nyingi zinazotumiwa na chama zitakuwa zinatoka kwa viongozi wakuu hasa Mbowe na wachache wao, hili si jambo jema kwa chama kama kinataka kujijjenga kama chama imara cha siasa.
 
Point yangu ni kwamba badala ya Viongozi wa Kitaifa kupoteza mamilioni ya pesa katika Mikutano ya Hadhara kwanini pesa hizo zisielekezwe katika ofisi hizo za Mikoani ili ziweze kuendesha shughuli za uimarishaji wa Chama Mikoani.Najaribu pia kujiuliza busara iliyotumika ya Viongozi Makao Makuu kushindwa kuziwezesha Ofisi za Mikoani kifedha ili ziweze kusimamia zoezi zima la ukusunyaji wa maoni kwa Wanachama kipindi kile Vyama vya Siasa vilipotakiwa kukusanya maoni ya Wanachama wao juu ya Katiba kisha wayasilishe kwa Tume ya Katiba ya Jaji Warioba badala yake Viongozi wa Kitaifa wakadandia fursa hiyo na kujifanya eti wanakusanya maoni ya Watanzania wote na pia walijua fika kabisa kuwa Tume ya Katiba wasingeyapokea maoni hayo ila kwasababu hawakuwa wanazunguka bure bali kulikuwa na per diem wakaendelea na mipango yao kama kawaida.

chadema si waaminifu hakuna hata sura ya kiongozi wa chadema inayofaa kuwa rais 2015,wote wamekaa kwa kuiba iba tuu,kuna watu wao wakisikia jambo flani wao ni kupinga tuu wakizingizia ni mamluki,ngoja watu wajitafunie mihela mnayochanga,we pinga kila jambo na wakati hata fom ya uongizi wa chadema hujui ipoje,katibu msaidizi wa chama anakuambua kuwa hakuna ripot ya fedha wewe unasema hawakupewa nafasi wazungumze ,wazungumze nini? kila kitu kuzungumza tunataka vitendo,mamilion ya sabodo na yako yamejenga majumba south,kenya hahahaa
 
Tatizo lenu wafuasi wa chadema mnalewa viroba hadi uwezo wenu wa kufikiri unapotea. Hoja iliyotolewa ni nzuri sana. Mnapaswa kuitafakari kwa kina

na tatizo lenu wafuasi wa ccm mna ugonjwa wa kupakatwa.
 
Jaribu kufanya utafiti mdogo tu n utaubaini ukweli.Kuna baadhi ya Ofisi za CHADEMA hapa Morogoro zimepigwa kufuri na tunasikia kwamba Chama kinapata fedha za kutosha sasa huwa zinakwenda wapi?WanaCHADEMA msijifanye wajinga kama wale wa CCM wasiotaka kushughulisha akili zao kufanya uchunguzi kubaini namna CCM ilivyo kikwazo kwa maendeleo ya Nchi hii.Uongozi huu wa CHADEMA una matatizo na ili CHADEMA tufikie malengo tuliyojiwekea ni lazima Uongozi huu wa sasa akiwemo Zitto mwenyewe ung'oke la sivyo Ikulu tutaisikia kwenye bomba.Kama kuna kitu ambacho kitaniumiza kweli moyo wangu basi ni kuiona CCM ikirejea madarakani 2015 ila kwa Uongozi huu wa akina Mbowe nina wasi wasi kwamba Watanzania tutaendelea kuongozwa na Mafisadi wa CCM.Akina Mbowe hamna kitu,Wanamharibu mpaka Dr Slaa.

Rejea dhana ya ukuaji wa shughuli za chama DUNIA nzima siyo Tanzania peke yake, Ruzuku haijawahi kujenga ofisi au kukiinua chama chochote Tanzania, baada ya awamu ya kwanza na kidogo ya pili ambapo ofisi za CCM mikoani na kwingineko serikali ilihusika kutoa fedha au kutaifisha majengo hayo.....Ruzuku ni kiini macho kinacho pewa uwezo usilo kuwa nao eti iendeshe shughuli zote za Chama mpaka mikoani?

Ikumbukwe Ruzuku hutolewa na serikali kuu ambayo kwa zaidi ya miaka 50 inajiita "sekretarieti ya CCM"
inawezekana vipi tuamini CCM inatoa fedha kukijenga CHADEMA?

Huko Morogoro kufungwa makufuli ofisi za CDMM ndiyo picha halisi ya Uanachama wa watu wa eneo husika, uhai wa Chama unatokana na Ushiriki wa watu na kujitoa kwao, unapoanza kutumia fedha ili ionekane ofisi ipo mahali hapo hiyo siyo uvuguvugu wa siasa bali ni ubaridi kwani itakua unaajiri watendaji ambao kimsingi hawana mamlaka ya kiutendaji zaidi ya shughuli za ukuaji wa chama jambo ambalo linahitaji zaidi ushiriki wa kila mwanachama na siyo ruzuku.

Hebu sote tuwe wanahisabati.....ruzuku hutolewa kwa kuzingatia idadi ya wabunge Bungeni (Bunge la Muungano) ... CHADEMA Ina wabunge pungufu kidogo ya asilimia 20% ya wabunge wote Tanzania. Km tunajua nini maana ya hesabu hii ya ruzuku ..... hata kwa mtoto hata wa darasani la Saba atajua haitoshi kwa Tanzania nzima km uwiano ndio huo.... km asilimia 20% ya wabunge wanaweza kuzalisha ruzuku ya kukiendeaha Chama Tanzania nzima basi itakapo fikia asilimia 60% basi chama kitakua na majengo mpaka india...!
 
chadema si waaminifu hakuna hata sura ya kiongozi wa chadema inayofaa kuwa rais 2015,wote wamekaa kwa kuiba iba tuu,kuna watu wao wakisikia jambo flani wao ni kupinga tuu wakizingizia ni mamluki,ngoja watu wajitafunie mihela mnayochanga,we pinga kila jambo na wakati hata fom ya uongizi wa chadema hujui ipoje,katibu msaidizi wa chama anakuambua kuwa hakuna ripot ya fedha wewe unasema hawakupewa nafasi wazungumze ,wazungumze nini? kila kitu kuzungumza tunataka vitendo,mamilion ya sabodo na yako yamejenga majumba south,kenya hahahaa

Wewe ndio umeongea vizuri.... ili uwaone viongozi wa CDM hawafai lazima uwe na ufikiri huu "hakuna sura ya kiongozi wa CHADEMA inayofaa kuwa raisi"..... inaelekea mwenzitu unapenda sana sura ...!

Wana CCM wote wa leo wako km wewe ... ufahamu wa kisiasa kwao ni mwiko ..... wao wamezoea vijembe ka vya taarabu hivi eti ndio uwezo wa utawala ka nape alivyo....au mwigulu...au kinana ..... au hata kikwete (anayeshangiliwa kwa vigelegele mikutanoni).

Yaani sina hakika hata km utanielewa... ila dawa ya kuhangaika na mjinga nikuwa mwerevu tu...! hata km utaona (mwerevu) haueleweki kauli za mwerevu zinaishi hata baada ya uhai wake. Kwa hiyo hata wapuuzi wakionekana kuishinda ...... sauti ya mwerevu asiye hai huzishinda hila na fikiri za wajinga..... Mfano kuna watu walio hai ambao wanahangaika na sauti ya Nyerere mpaka leo na ngoma nzito kuishinda sauti ya aliyesimamia utu na haki.
 
Baada ya kusimamishwa katibu msemakweli w chadema mh mwigamba kwa kuhoji ukweli juu ya viongoz masultan ndani ya Chadem (mbowe na slaa) kuwa wamachomoa kipengele cha katiba kinachosema kila kiongoz awe na ukomo wa miaka mitano kwa awamu mbili.

Kijana huyu ameshindw kueleza kwa uwaz kwani akizungumza angefukuzwa! Alafu ndio wanasema hiki ni chama cha Demokrasia.

Naanza kuamini kuwa ZITTO sio mbaya kwa chadema. napia naanza kuamin kwa halii bora LOWASA 2015 kuliko SLAA NA MBOWE kuwa viongoz wa nchi yetu. ukweli ndio huo hata ukibisha we zombi. ngoja nitafute softcopy ya katba niwaekee muone.
Hapa ndipo palipo na ajenda ya SIRI.... KWA NINI MACCM wote tena wale ambao hamkufuata sera bali ajenda ya siri mtu mzuri ndani ya CDM ni ZITTO?... WHY??!!!!!!!!...... KWA NINI?!!!!...
 
kama angekuwa ni jk ana nyumba marekani, uingereza, afrika kusini, na dubai, cjui mngesemaje!! maana chadema kwa kujadili watu wengine ndo sera zao. na sasa mnamjadili zito, badala ya kujadili mapato na matumizi ya chama chenu. mkija kushtuka mmetafunwaaaa
Hapa ndipo palipo na ajenda ya SIRI.... KWA NINI MACCM wote tena wale ambao hamkufuata sera bali ajenda ya siri mtu mzuri ndani ya CDM ni ZITTO?... WHY??!!!!!!!!...... KWA NINI?!!!!...
 
Nimesoma robo tu nikapata picha nzima! Kwamba CHADEMA imefikia hapa ilipo kwa kupiga vita ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali nk, pia nikaona kuwa umemsifia Mbowe na Slaa kwa kuwezesha chama kufikia hapa kilipo.

Ila PIA ume propose hao hao waliotufikisha hapa wasaidiwe kwa kutimuliwa! Sijaona ukionyesha sehemu yoyote kuwa vita yetu sasa imekwisha!!au tumeshinda ama tumeshindwa! Kama ufisadi umeisha nchi hii! Au kama rasilimali zetu sasa zinatumika vizuri ungepaswa kutuonyesha kuwa vita sasa imekwisha,na hivyo tuwapumzishe wapiganaji wetu, ila kama vita bado inaendelea,na wewe ukataka tuwakimbize wapiganaji wetu wa mstari wa mbele ambao umeukiri utendaji wao kuwa bora!! Ni kuthibitisha kiwango chako cha juu cha usaliti (kama ulikuwa kweli miongoni mwa wapiganaji) au wewe ni MAMLUKI usiyejitambua, angalau ungesema tuwa support ungekuwa na ka point.

Capt Tamar,
umekuwa very bias sana na bila shaka ni kwa kuamua kuw mvivu kuisoma vyema taarifa hii. Pamoja na kuwa pro Chadema sana tu, lakini hoja yake huyu bwana ni ya msingi sana, Kiongozi hata kama angekuwa ametuvusha na kutufikisha tunapopataka napaswa kuwa mwadirifu tu, na ni kwa mantiki hiyo basi, hawa watu kama wamekosa uadirifu wakati muhimu kama huu ambapo tunapaswa kupiga kelele za ufisadi, wivi wa rasilimali zetu, rushwa nk, vile vile walipaswa kuongoza kwa mifano/vitendo.
Huyu bwana si mamruki kama wengi wanavyotaka kuaminishwa, the problem ninayoiona kwake ni namna ambavyo amewasilisha, platform haikuwa sahihi, hata kama kuna uhuru wa kutoa maoni, lakini lazima kupima nafasi yako kama kiongozi na madhara yapi yanaweza kusababishwa na namna ya utoaji habari. Lakini bottom line, ukweli unapswa kubaki kama ulivyo na kufanyiwa kazi.
 
Pale Bukoba mwaka wa uchaguzi uliopita kuna mgombea wa chadema misenyi alijitoa kugombea baada ya kunyimwa msaada katika harakati za kugombea ubunge, baada ya nguvu kupewa Rwakatale tu. I wish huo ni udhaifu, jamaa aliacha, akaendelea na mambo yake. Nafikili wanachama wa chadema mnaugua ugonjwa wa wanachama wa CCM wa kutokubali ukweli. Vyama vimewaharibu vijana, hawawezi ku argue tena, wanataka kufikili kama wanasiasa. Nafikiri kuna haja ya kutafakali kauli hii, na mkumbuke kilichoiua CCM ni makundi siyo umaarufu wa chadema. Umaarufu wa chadema umetokana na ubovu wa CCM, ndo kusema CCM akitokea mtu akachange mwelekeo wa chama, watu wake watarudi. Huwezi kuamini, ila mpasuko kwenye vyama ni hatari. Sipendekezi afukuzwe, ila kama katiba inasema ni miaka 10, lazima kuheshimu hata kama bado umri unaruhusu, na kama kweli katiba imebadilishwa kinyemela, ni hatari, ni kma yale wanayolalamikia ya serikali kubadili vifungu kinyemela. Someni katiba zote muangalie vifungu hivyo vipo na kama ni kweli vimeondolewa, mtaelewa kama jamaa ni pandikizi. Kauli za chadema kumshambulia zito hata mie nimezisikia laivu kwenye vyombo vya habari, mengine yana ukweli hata kama si sehemu sahii ya kuyawasilisha.

Jmaa mwingine nilisoma thread yake akilalamika kuwa si vema kuwachangisha watu kwenye mikutano eti wasaidie kuendesha chama, wakati watu wanapanda chopa, wakati magari yanatumia gharama nafuu kuliko chopa. Think
 
Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wa chama.

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.

Naandika nikiwa mwana
CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Ni mawasiliano baina yetu wana CHADEMA na tunahitaji tutulie na kutafakari.

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika. Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio,
CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwinginekidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kilamwanachama.

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.


Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49. Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzitoza kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao. Leo nitaainisha mambo machachetu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripotiza fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi yakakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwambakiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michangoya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni
questionable.

3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tuniliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, nahivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndotoya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari napikipiki zote za M4C.

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo Mwenyekiti Taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake yatenda. Huu si ufisadi ni nini?

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi namauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu.


Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama upinzani.

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.


Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetuwakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli piakwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapondipo mtakapojua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.

Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.

Ahsanteni kwakunisoma
!


kama kuna ukweli hapo basi CCM kutoka madarakani itakuwa ni kama ni ndoto za alinacha duuuuuuuuuuuuh pia naomba hao makatibu wa wilaya na mikoa wadhibitishe kweli kama hawajapokea hizo fedha au na huyu naye anahasira zake na kiongozi fulani ndio akaona bora aje amalizie hapa hapa.
 
Back
Top Bottom