Ni jambo la ajabu sana kama watu hawatakuwa na haki ya kuongea yaliyomo ndani ya nsfsi zao na hawatapewa muda wa kuwasikiliza watu wengine.Nchi hii ni yetu sote watanzania,na ni jukumu letu sote kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kuijenga bila kujali tunaijenga kupitia CDM,CCM,CUF,TLP ama vyama vingine au taasisi na nyanja nyingine.
Kama mtu upo ndani ya taasisi fulani,halafu ikatokea hupendezwi na mambo yanavyoendeshwa hapo taasisini,jambo la msingi la kwanza ni kupeleka hoja yako ya msingi kwenye ngazi ama vikao husika,halafu unasubiria kupewa majibu na ikiwezekana kuona hatua zinachukuliwa. Kama umefuata taratibu husika za hiyo taasisi kuwasilisha hoja yako lakini hujasikikiliza na wala hoja yako kufanyiwa kazi,basi hapo sasa ndipo panapokuja suala la kuangalia hatua nyingine za kuchukua ili hoja yako isikilizwe na ifanyiwe kazi.
Tatizo la vijana wengi walio na mapenzi ya upofu ya watu fulani katika vyama ni kuona kuwa mtu yeyote anayemuongelea vibaya mtu anayempenda ni msaliti hata kama kuna ukweli na ushahidi katika jambo linalozungumzwa.
Haya mapenzi ya upofu yatatugharimu sana watanzania kwani yatatufanya tuwe watu wa "ndio mzee" na kuogopa kusema ukweli hata kama mtu anakosea.
MAPENZI YA UPOFU KWA MUSTAKABALI MWEMA WA TAIFA HILI TUYAWEKE PEMBENI,tufanye yale mambo amabyo ni kwa ajili ya ustawi wa tanzania hata kama yatakuwa hayapendwi na baadhi ya wapendwa wetu.