Wito kwa wana CHADEMA wote!

Wito kwa wana CHADEMA wote!

Kiongozi anayeng'ang'ania Madaraka ujue amefanya madhambi kwa hiyo yuko tayari kuharibu uimara wa taasis husika au nchi kabla ya kutoka madarakani ili isiwe na uwezo wa kumwajibisha. Mbowe akiogopa kuachia madaraka na kutaka kuua Chama basi tujue atakuwa amefanya dhambi ndani ya Chadema kwa hiyo anaogopa kuhukumiwa.

Kuna makala hii hapa Raia Mwema inatoa picha kubwa pia ya kinachoendelea ndani ya Chadema. Mbowe amefikia hatua ya kuwaongezea Wakurugenzi wake mishahara ili wambakishe madarakani. Pia ameajiri vijana ambao wamekuwa wakimpigia debe mitandaoni ili kuongeza nguvu ya kumsafisha na kumchafua Zitto namaanisha Ben Saanane na Mohamed Mtoi - Raia Mwema - Dhana ya ugaidi ndani ya vyama vya siasa Tanzania
 
Ukitaka kujua watanzania walipofikia ni rahisi tizama hoja hii ya Mh Zitto ya kukaguliwa kwa mahesabu ya vyama kwamba kila kitu tanzania ni siasa tena chafu mno. Cuf wanapata fedha hakuna anaesema, TLP, UDP,CCM, ppt maendeleo, NCCR, huko hakuna ubadhilifu ila CDM,
 
Ni wapi ambapo CHADEMA wameungana na CCM kumshambulia Zitto kama ulisoma vizuri CHADEMA walijikita zaidi kwenye utetezi baada ya kutuhumiwa na kamati ya Zitto.CCM kwa kupitia katibu mwenezi wao Nape walijikita zaidi kwa kuishambulia CHADEMA utafikili ndiyo imegeuka kuwa kamati ya Zitto iliyowaita.
 
Kwanini wafuasi wa CCM na anti CHADEMA wote wanataka uongozi wa CDM ubadilike?Wenye akili zetu tunajua kwamba huu ndio Uongozi utakaoipeleka CDM ikulu na kutuondoa kwenye utawala wa mkoloni mweusi CCM
 
Kwanini wafuasi wa CCM na anti CHADEMA wote wanataka uongozi wa CDM ubadilike?Wenye akili zetu tunajua kwamba huu ndio Uongozi utakaoipeleka CDM ikulu na kutuondoa kwenye utawala wa mkoloni mweusi CCM

Utakuwa unajidanganya CHADEMA haitaingia madarakani chini ya kanjanja wa Siasa Mbowe,CHADEMA itaingia madarakani kama itaongozwa na Watu wengine.

Mbowe anatudanganya tu hata hili suala la Katiba natumaini CUF Zanzibar watakomaa lakini Mbowe hapa amaeshatuuza ile Mikutano ya Hadhara ni danganya toto tu.

Unajua Mbowe ni mfanyabiashara sasa jiulize hivi kwa siasa za Kibongo za kutishana kweli Mbowe hatakuwa anafanya biashara na CCM ili kulinda maslahi yake ya kibiashara?

Kama Mbowe angekuwa na dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM madarakani sina uhakika biashara zake zingekuwa katika hali gani.CCM wanajua vizuri kuwa uongozi wa Mbowe hauna madhara kwao kwasababu ni mwenzao.

Hivi pia ulishawahi kujiuliza kwanini akina Mbowe walimchagulia Dr Slaa Mgombea Mwenza mwenye elimu ya Std 7?
 
Utakuwa unajidanganya CHADEMA haitaingia madarakani chini ya kanjanja wa Siasa Mbowe,CHADEMA itaingia madarakani kama itaongozwa na Watu wengine.Mbowe anatudanganya tu hata hili suala la Katiba natumaini CUF Zanzibar watakomaa lakini Mbowe hapa amaeshatuuza ile Mikutano ya Hadhara ni danganya toto tu.Unajua Mbowe ni mfanyabiashara sasa jiulize hivi kwa siasa za Kibongo za kutishana kweli Mbowe hatakuwa anafanya biashara na CCM ili kulinda maslahi yake ya kibiashara?Kama Mbowe angekuwa na dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM madarakani sina uhakika biashara zake zingekuwa katika hali gani.CCM wanajua vizuri kuwa uongozi wa Mbowe hauna madhara kwao kwasababu ni mwenzao.Hivi pia ulishawahi kujiuliza kwanini akina Mbowe walimchagulia Dr Slaa Mgombea Mwenza mwenye elimu ya Std 7?

Makanjanja wa siasa utawajua tu. Mnajiita wanaChadema huku mnaihubiri ccm! Bahati nzuri tunazidi kuwabaini makamanda feki!
 
Tunashukukuru kwa taathimin yako nzur ni wakati sasa wa kufanya mabadiliko sahihi kwa manufaa ya wote sema tu kama mleta wazo umeshindwa kuonyesha wapi pa kuanzia
 
Kwa wale wote wadau wa siasa na wafuatiliaji wa mambo ya siasa wanafahamu kuwa mbowe amekuwa mwenyekiti wa chadema tangu 2003 hadi sasa.

kwa mantiki hiyo anastahili pongezi kwa kukifikisha chama hapo kilipofika kwani ni hatua amabayo mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuibeza hata kidogo.

kwa mujibu wa katiba ya chadema mbowe anamaliza mda wake wa uongozi mwaka huu mwezi disemba ambapo tunategemea apatikane mwenyekiti mwingine wa kuendeleza mazuri yaliyofanywa na mbowe na kuacha mapungufu yaliyokuwepo wakati wa uongozi wa mbowe.

kwa maoni yangu ni vema mbowe akastafu kwa heshima pasipo kukatalia madarakani kama wanavyofanya baadhi ya wanasiasa hasa wa kiafrika.

Mazuri yaliyofanyika wakati wa uongozi wa mbowe ni pamoja na kuongeza wabunge,kuongeza,wanachama,kukua na kuenea kwa chama nk.

Lakini pia chini ya uongozi wa mbowe kumekuwepo na mapungufu mengi ambayo kwa kweli mbowe hatumhitaji tena kuendelea kuwa mwenyekiti wa chadema haya ni baadhi tu ya mapungufu.

1.mbowe amepitisha kujilipa mshahara takribani tsh 1722000 kwa mwezi,
2.mbowe amekubali dr slaa alipwe mshahara wa tsh12570000 kwa mwezi,
3.mbowe ameruhusu heche alipwe mshahara wa tsh takribani 9000000 kwa mwezi,
malipo haya siyapingi kama kungekuwa na usawa na uwazi kwenye ulipaji wa hizi pesa lakini cha ajabu mpaka hela za ruzuku za chama zinatumika kulipa watumishi kitu ambacho ni kinyume na sheria hata hivyo kumekuwa na tofauti kubwa sana ya malipo baina ya mtumishi mmoja na mwingine,

Lakini kitu cha kushangaza zaidi tumeambiwa kuwa mkutano wa jangwani uliojumuisha vyama vitatu chadema ndiyo iliyogharimia uendeshaji wa mkutano huo kwa maana ya kulipa posho za viongozi,kukodi magari ya kupeleka na kurudisha watu,kulipa magari ya matangazo,vikundi mbalimbali ambapo gharama zake tumeambiwa ni kama milioni700,000,000 kitu ambacho hakiingii akilini hata chembe.

Sote tunakumbuka wakati wa mabaraza ya katiba mbowe aliruka na helkopita mara kumi kwenda kuongea na wanachama sehemu mbalimbali,wakati slaa aliruka mara saba gharama zote zilifika 680,000,000 mln kitu ambacho ni hatali sana kwa kuwa na matumizi ya namna hii kwenye chama ambacho tunaamini kinapigania haki za wanyonge.

Hapo ndipo ninapopingana na mbowe kwa kuwa na matumizi makubwa kwenye chama tena yanayolenga baadhi ya watu halafu hawataki yahojiwe kweli tunajenga chama kwa namna hii au tunanufaisha baadhi ya watu?,kwa mpango huu naona dalili kwa mbali inakuja upo uwezekano wa baraza la wazee kukubali kubadili vifungu vya katiba vya chadema ili mbowe aendelee kuwa mwenyekiti kitu ambacho wengi wapenda mabadiliko hatukipendi.
USHAURI;
MDA WAKO UKIISHA MBOWE ONDOKA NA HESHIMA YAKO USIKATALIE MADARAKANI
 
Mbowe amekuwa kisiti forsometime now .CCM kila wakijaribu mbinu za kijinga wanakuta mbele giza .Mbowe si Mrema Mzee .Mbowe anamaanisha siasa .Kazi mnayo sana .
 
MAGAMBA mnaangaika sana na CHADEMA...
Kwa hiyo umeona uje na dili la mishahara feki hapa jukwaani...hahahaaa...kazi mnayo...na bado tupo vijijini huku Ngara tunatoa elimu kwa wanavijiji ambao wanaishia kuuza kura zao kwa t shirt, kanga na gongo...kipindi hiki tumewashika Magamba
 
Mbowe amekuwa kisiti forsometime now .CCM kila wakijaribu mbinu za kijinga wanakuta mbele giza .Mbowe si Mrema Mzee .Mbowe anamaanisha siasa .Kazi mnayo sana .

sijui kama unajitambua vizuri mkuu unahitaji maombi ya hali ya juu.
 
Nikupongeze kwa mpangilio mzuri wa thread yako. Kuhusu ukweli wa ulichokiandika, nitafanya uchunguzi binafsi.
 
Chama Kipya,
Kwanza niliisha kuahidi katika jamvi hili kuwa uchochezi na uwongo wowote hautaachwa bila kujibiwa. Pamoja na kuwa fedha za Chama ni haki kwa wanachama kupata taarifa sahihi, haki hiyo hiyo inamtaka yeyote anayepotosha ajibiwe palepale ili wanachama, wapenzi na wananchi kwa ujumla wasipotoshwe na propaganda zisizo na maana. Dr Slaa ndiye accounting Officer, yaani msimamizi Mkuu wa fedha na Mali za Chama kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chadema ( tz Katiba Toleo la 2006). Hivyo:

1. Chama kipya, Kama wewe si mwongo, mchochezi, many propaganda, weka hadharani vielelezo kuwa Mbowe na Dr Slaa wanalipwa mishahara hiyo. Mimi Kama Accounting Officer, na kwa mujibu wako mnufaika mmojawapo wa hiyo fedha sijawahi kulipwa wala kupokea. Njia ya kuondoa majungu na watu wakuamini ni kwa wewe kuweka hadharani nyaraka husika. Chadema hatutoi fedha Kama Karanga, kuna nyaraka nyingi zinahitajika hadi pesa, hata sentimmoja kulipwa. Hivyo weka hizo nyaraka jukwaani ili watu wakuamini. Vinginevyo wewe ni mwongo, na unaajenda yako, au kwa kutumwa.

2. Aidha Chama Kipya, ni kweli mkutano wa Jangwani una gharama, kwani Jukwaa ni gharama, viti hukodishwa, mikutano hutangazwa, hata kwenye harusi au sherehe yeyote ni hivyo hivyo, huhitaji elimu ya juu kuelewa hivyo. Lakini kwa makusudi imeamua kupotosha. Kiwango ulichokitoa ni cha uwongo wa kupindukia. Ili watu wakuamini na kukuona wewe ni wa maana, weka nyaraka za malice hayo ikiwa ni pamoja na fedha za posho ya viongozi na kukodi magari ya kubeba watu. Usipoweka hadharani watu wakuone mwongo, na mpotoshaji mkubwa na mharibifu wa demokrasia ya kweli katika nchi yetu.

3. Sababu unazotoa kuwa Mbowe anang'ang'ania uwenyekiti na kuwasemea vijana unawasemea vijana gani. Kwa utaratibu wa kawaida tu, ukikisemea kundi ni kuwa lilikutana mahali. Tuwekee hadharani ni kikao gani cha vijana kilifqnya tathmini ya utendaji wa Mbowe na kuweka azimio lililofikiwa kuwa " anang'ang'ania na akifanya watahama". Kikao hicho kilifanyika ukumbini gani na tarehe ngapi? Ukishindwa kuweka hadharani, ueleze umma wa Watanzania kwanini usikuone mwongo, mchonganishi, mharibifu na usiyetakia mema Tanzania na adui wa ukombozi wa kweli, kwani watanzania wengi wametoa Mali zao, damu Yao, wengine Leo vilema kwa ajili ya kupigania ukombozi wa pili nawe bila aibu unaleta hoja za kichonganishi na kipuuzi. Muda wa kubembelezana umeisha, na Kama nilivyosema, jukumu la katibu Mkuu ni pamoja na kulinda Taswira ya Chadema inapotaka kuchafuliwa bila sababu ya msingi na bila ukweli. Ukweli kwa mtu yeyote mstaarabu ni msingi wa kutoa hoja, Kama hakuna ukweli katika unayosema, jitafakari uhalali wa kauli yako!

4.Chadema ni chama chenye Katiba, Kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali. Kama unayoyasema yana hata chembe ya ukweli na Kama kweli una nia njema, weka hadharani Kama ulikwisha kuwasilisha malalamiko yako kuhusiana na hayo unayosema kwa chombo chochote cha maamuzi. Mbowe na Slaa siyo wa mwisho ndani ya Chadema. Wanasimamiwa na Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu. Weka hadharani kuwa malalamiko yako hayakufanyiwa kazi, yamepuuzwa, hukutendewa haki. Bila ushahidi huo, ni kwanini watanzania wasikuweke kwenye kundi la maadui wa Ukombozi wa Taifa hili. Tangu lini JF au chombo chochote kile Kama hicho kimegeuka kuwa chombo cha nidhamu ya chama. Kama hujui hata Katiba ya Chama chako, na taratibu za utendaji ndani ya Chama, hata vita dhidi ya ufisadi ambayo kwa muda mrefu chadema imesimamia na itaendelea kusimamia kwa Taratibu za kisheria, ndio maana hatuna uwoga, wewe utawezaje kusimamia misingi hiyo, Kama jambo dog Kama hili umeshindwa kulielewa.

5. Kwa manufaa ya wasomaji wetu, licha ya jukwaa, viti, Mkutano wa Jangwani ulichangiwa na vyama vyote vitatu, na formula ya kuchangia mkutano huo ilikubaliwa kwenye vikao rasmi na wala siyo barabarani Kama unavyotaka kuwaaminisha watanzania. Ni upuuzi kurukia vita na kuyapotosha kwa lengo lako binafsi. Kwa mujibu wa formula hiyo, Chadema ilipangiwa kugharimia mkutano huo kwa asilimia 57 na Kila chama kilipewa asilimia yake kwa kuzingatia vigezo mbalimbali. Kazi hizi zinafanyika kisayansi, tofauti na unavyofikiri na kundi lako. Kati ya hizo asilimia 57 sehemu kubwa ya matumizi hayo ilitumika kulipia matangazo ya moja kwa moja ya ITV ( live Transmisdion) ili ujumbe uwafikie Watanzania wote).

Sasa utuambie Kama Live transmission haikufanyika. Ni kwa msingi huo ninawaomba Watanzania kumpuuza Chama Kipya na wote wa aina yake, kwani kwa upuuzi wao huu wana nia tu ya kutuondoa kwenye hoja muhimu, na kujenga hisia ya matumizi mabaya ndani ya chadema, au kugombania vyeo. Narudia ten a, vyeo ndani ya Chadema ni dhamana na havigawiwi Kama karanga. Mtu atuhumiwe kwa utendaji wake mbovu, na utendaji mbovu hupimwa kwa vigezo dhahiri na siyo kwa hisia, au kwa " kuambiwa..." au " kusikia" Kama Chama Kipya anavyodhihirisha katika indigo lake.mapambano daima, na kwa dalili hizi naona ukombozi wa oil umekaribia, kwani hila hizi zimeshindwa hata kabla hazijaanza.
 
Makanjanja wa siasa utawajua tu. Mnajiita wanaChadema huku mnaihubiri ccm! Bahati nzuri tunazidi kuwabaini makamanda feki!

Ili imani yangu irudi kwa Mbowe itabidi apishe ili uchaguzi wa Viongozi wapya wa Chama hatimaye ufanyike katika mazingira ya kidemokrasia na haki.Chama kinahitaji Watu wenye mawazo mapya na mbinu mpya ya kupambana na CCM na ninaamini CHADEMA watashinda katika Chaguzi zijazo.
 
Miongoni mwenu kuna atakayenisaliti ili NENO litimie!
 
CHADEMA ilisajiliwarasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wenyeviti wa taifawawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Mzee Edwin Mtei aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 1993 hadi 1998 na kumwachia Mzee Bob Makani ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzonimwa 2004 na kumwachia Freeman Mbowe ambaye yuko madarakani hadi hivi sasa.

Mbowe aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwatena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili. Napenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wenyeviti wetu wote waliopita walizozifanya katikakuhakikisha chama chetu kinakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katikamazingira yaliyowakabili.

Mwaka 1995 chini ya Mzee Mtei tulipata wabunge watatu. Mwaka 2000 chini ya Mzee makani tukapata wabunge wanne mmoja wa viti maalum nakufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya Mbowe, tulipata wabunge watanowa kuchaguliwa na viti maalum sita jumla wakawa 11. Mwaka 2010 chini ya Mbowehuyo huyo, wakaongezeka na kuwa 23 na wa viti maalum 25 na kufanya idadi kuwa48 kabla ya kushinda uchaguzi mdogo Arumeru mashariki mwaka jana na kufanyasasa wawe 49.

Tunapopongezajuhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanzaambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badalayake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka nakimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga chamaimara kinachojali demokrasia na haki ya kila mwanachama. Ni kwa msingi huowaliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngaziyoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimojacha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili chamiaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ilealiyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kilewalichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwilivilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza natusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Napendakuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo:

Moja, wakatiKatiba ya CHADEMA ikifanyiwa mabadiliko mwaka 2006, mabadiliko hayo hayakugusakipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi yavipindi viwili vya miaka mitano mitano. Niliyaona makabrasha yaliyogawiwa kwawajumbe wa mkutano mkuu yaliyokuwa na mapendekezo ya Baraza kuu ya mabadilikoya katiba na mkutano mkuu kuyapitisha mapendekezo yale yote. Lakini wakati katibainachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwamakusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hikikinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanawezakutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika nawanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa chamachetu.

Vitainayoendelea leo kati ya Mbowe na Zitto ya kupigania uenyekiti wa chama katikauchaguzi ujao kiasi cha kuumiza chama, isingekuwepo maana Mbowe alikuwaharuhusiwi kugombea kwa mara ya tatu mfululizo. Kitendo cha Freeman Mbowekutaka kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha tatu mfululizo tofauti na msingiwalioujenga waliomtangulia, ni uthibitisho kamili kwamba kile kipengelekiliondolewa kwa maelekezo yake ili baadaye atakapotaka kung'ang'ania madaraka asionekaneanavunja katiba. Mbowe sasa anataka kuwa mwenyekiti wa design ya akina LyatongaMrema, John Cheyo, Chipaka, Makaidi, Mtikila, na kadhalika, jambo ambalo hatupaswikulikubali wana chadema.

Pili nambaya zaidi, anang'ang'ania madarakani wakati ambapo ameishiwa mbinu zakukikuza chama. Enzi zile za 2005 kuelekea 2010 chama kilikuwa kinaishi kwaissues, lakini leo kinaishi kwa matukio. Ni ujinga wa CCM tu kutupatia matukiolakini wakitunyima matukio chama kinakufa. Mbowe siku hizi anafanya kazi kwa kushauriwana vijana waliojaa mihemko kama Lema, Nassari, Wenje na Msigwa. Hawa hawanauwezo wa kukaa chini na kutengeneza mkakati (strategy) wa kuingiza chamamadarakani. Wanachojua ni kufanyia propaganda kila tukio linalotokea na kufanyamikutano ya hadhara, basi! Hatuwezi kuingia madarakani kwa mtindo huu. Hili waasisiwetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozikwenye mwongozo katiba ili kiongozi asing'ang'anie kuendelea kuongoza wakatiameshachoka.

Kuchoka kwauongozi wetu kunazidi kujidhahiridha katika mipango program mbalimbali za chamakwa miaka kadhaa sasa. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha Operesheni Sangara.Operesheni hiyo ilifanywa katika mikoa kadhaa ya kanda ya ziwa na hatimayeikafa kimya kimya. Hiyo ilikuwa ni baada ya kufa kwa program ya CHADEMA ni tawina CHADEMA ni msingi. Baada ya uchaguzimkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwayakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote.Kumbukumbu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwendakwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyikaMwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya,Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende.

Kisha mwaka2012 likaanzishwa Vuguvugu la Mabadiliko ama Movement for Change (M4C) Hiyoilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumlazilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia yamikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanyamafunzo kwa viongozi. Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kishaikaenda kufia Iringa. Mwaka huu 2013 viongozi wetu wamekuja na ugatuajimadaraka kutoka makao makuu ya chama na kupeleka madaraka kwenye kandambalimbali. Program hii ilikufa kabla ya kuanza pale Mwenyekiti Mbowe alipobadilishamaazimio ya Baraza Kuu na kutekeleza matakwa yake ikiwa ni pamoja na kuletasuala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri waratibu na maofisakama ilivyoazimiwa kwenye Baraza kuu la Januari mwaka huu.

Naamehakikisha anaweka watu wake kwenye uongozi wa muda katika kila kanda kwakuanzisha kitu kinaitwa kuzindua kanda ambacho hakikuwemo kwenye azimio laBaraza kuu na kimekula pesa nyingi kwa yeye mwenyewe kwenda kila kanda na timukubwa ya wakurugenzi na maofisa wa makao makuu waliolipwa posho na gharama zausafiri lukuki. Pesa hizo zilitumika kwa kiwango kikubwa wakati ofisi za kandahazina ruzuku tuliyoipitisha kwenye Baraza kuu na wala ofisi za mikoa, wilayana majimbo hazina hata shilingi ya kuendesha chama. Matokeo yake ni nini? Matokeoyake ni kwamba kile kilichopitishwa na Baraza kuu mwanzoni mwa mwaka ni hewa.Kama huamini tazama ratiba iliyopitishwa na Baraza kuu mwezi Januari mwaka huu:

Januari 2013: Vikao vya Kamati ku u na Baraza kuu. Februari20 13: -Kanda: Kuunda timu za operesheni na kutafuta nyenzo na fedha zaoperesheni, - Makao makuu: kuandaa vifaa, vipeperushi vya ujumbe wa operesheni,mfumo wa utoaji taarifa na mafunzo kwa timu za kanda. Machi 2013: Kutoamafunzo, kwa timu za operesheni za kanda, Kusambaza vitendea kazi katika kanda,Kuteua waratibu na maafisa wa kanda, Kupatikana kwa ofisi za kanda na kupatiwavitendea kazi. Aprili hadi Septemba 2013: Operesheni kikanda, chaguzi zamisingi, matawi, kata, majimbo na wilaya. Oktoba 2013: Kumalizia chaguziza majimbo na wilaya. Novemba 01 - 18, 2013: Chaguzi za mikoa. Desemba2013: Uchaguzi ngazi ya Taifa - Desemba 18: BAWACHA, Desemba 19:BAVICHA na WAZEE, Desemba 20: Kamati kuu, Desemba 21: Barazakuu, Desemba 22: Mkutano mkuu, Desemba 23: Baraza kuu jipya, Desemba24: Kamati kuu mpya. Nani leo anaweza kusimama na kubisha kwambatulichokipitisha kwenye Baraza kuu ni kiini macho kama leo mwezi wa kumitulikuwa tunatakiwa kumalizia chaguzi za majimbo na wilaya lakini hata misingihatujafanya uchaguzi?

Kitendo hiki kwa pekeyake, cha kufeli kwa kila mpango unaoletwa na viongozi wetu katika hatua zautekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mpango, ni kiashiria tosha kwambauongozi uliopo umechoka. Nimejitoa mhanga kuwaelimisha wanachadema kote walikoTanzania kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa kwenye uongozi wa kitaifa katikauchaguzi watakaoutisha iwe ni mwaka huu ama mwakani ama mwaka keshokutwa.Hatuwezi kuendelea na hawa watu. Tuwape nafasi watulie ili Mbowe afanye vizurikazi yake ya uongozi wa kambi ya upinzani bungeni na Dr. Slaa apate nafasinzuri ya kujiandaa kuja kuwa Rais wa Tanzania hapo mwaka 2015.

clip_image001.gif

Itaendelea juma lijalo…..
 
Magamba bana! Mpini aukalie mwingine, mauno mkatike nyie. Sijaonaga Unafiki wa kiwango kikubwa namna hii. Sisi Chadema tumetulia tulii, nyie Magamba ndio mnaweweseka. Hata kama hamumtaki Mbowe kwasababu anawatesa, yeye ndiye atakayeendelea kuwatesa mpaka 2015 mtakapopelekwa kaburini. Dadadadeq!
Hatubadilishi uongozi kwasasa, Mapandikizi mliyoyaandaa ili yaje kuchukua uongozi mtapiga nayo picha mwaka huu, lazima yawadodee. Dadeq!
 
Maskini Mkulima
Januari 2013: Vikao vya Kamati k
u u na Baraza kuu.
Februari20 13: -Kanda: Kuunda timu za operesheni na kutafuta nyenzo na fedha zaoperesheni, - Makao makuu: kuandaa vifaa, vipeperushi vya ujumbe wa operesheni,mfumo wa utoaji taarifa na mafunzo kwa timu za kanda. Machi 2013: Kutoamafunzo, kwa timu za operesheni za kanda, Kusambaza vitendea kazi katika kanda,Kuteua waratibu na maafisa wa kanda, Kupatikana kwa ofisi za kanda na kupatiwavitendea kazi.
Aprili hadi Septemba 2013: Operesheni kikanda, chaguzi zamisingi, matawi, kata, majimbo na wilaya.
Oktoba 2013: Kumalizia chaguziza majimbo na wilaya.
Novemba 01 - 18, 2013: Chaguzi za mikoa.
Desemba2013: Uchaguzi ngazi ya Taifa -
Desemba 18: BAWACHA,
Desemba 19:BAVICHA na WAZEE,
Desemba 20: Kamati kuu,
Desemba 21: Barazakuu,
Desemba 22: Mkutano mkuu,
Desemba 23: Baraza kuu jipya,
Desemba24: Kamati kuu mpya. Nani leo anaweza kusimama na kubisha kwambatulichokipitisha kwenye Baraza kuu ni kiini macho kama leo mwezi wa kumitulikuwa tunatakiwa kumalizia chaguzi za majimbo na wilaya lakini hata misingihatujafanya uchaguzi?


Naamini ni washabiki wazuri wa JF waje na majibu.
CC: Tumaini Makene, Ben Saanane, Kurugenzi ya Habari, Dr.W.Slaa
 
Last edited by a moderator:
Magamba bana! Mpini aukalie mwingine, mauno mkatike nyie. Sijaonaga Unafiki wa kiwango kikubwa namna hii. Sisi Chadema tumetulia tulii, nyie Magamba ndio mnaweweseka. Hata kama hamumtaki Mbowe kwasababu anawatesa, yeye ndiye atakayeendelea kuwatesa mpaka 2015 mtakapopelekwa kaburini. Dadadadeq!
hizo ni hadithi za bunuasi or fisi na sungura, Chadema ata wabunge 25 hawatafika na amini majimbo yote ya mjini yanaludi Ccm. kufanyika kwa uchaguzi chadema ni lazima kumbukeni Chadema ni Taasisi, lazima uchaguzi uweopo.
 
Back
Top Bottom