MOSI:
CHADEMA inabidi ipige hatua ya ziada, humu kwenye mitandao wako wengi wanaokichafua chama kutokana na post na comments zao,,,, wapo wanaCHADEMA kwa makusudi aidha kwa kutumwa au kwa kujituma wamekuwa wakimchafua Zitto huku wakidhani kumchafua kiongozi si kuchafua chama. Watu wa namna hii lazima nao washughulikiwe.
Halafu hii tabia ya kuchafua viongozi kwa kutumia mitandao imeshakuwa ndio tabia ya watu fulani humu kwenye mitandao, afadhali ya Mwigamba kafanya hivyo[kawachafua viongozi] kwa kujenga hoja, lakini wengine wanawachafua viongozi wengine bila hata hoja,,,husani wale wanamchafua Zitto sikuzote wanafanya hivyo bila hata hoja zaidi ya mtu akimua kuchafua hali ya hewa, basi anafanya hivyo. Nimesema Mwigamba kawachafua viongozi kwasababu amewakosoa viongozi nje ya utaratibu wa kichama, TABIA KAMA HII NA IKOME.
PILI:
Naunga mkono hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya Mwigamba, kwani kitendo cha Mwenyekiti wa chama mkoa kutumia mitandao kukosoa chama lazima kihesabike kuwa ni hujuma dhidi ya chama na njama za kukichafua chama hata kama hoja zake zitakuwa lulu kwa kiasi kikubwa. Hivyo, hatua hizi ziwe fundisho kwa viongozi wenye tabia kama zake.
TATU:
CHADEMA lazima iangalie mfumo wake wa kupokea mawazo mapya, maoni na utaratibu mzima wa vikao vya chama. Kwa vyovyote vile hizi hoja za Mwigamba hazijalishi mbaya au nzuri atakuwa amekosa jukwaa la kuzisemea ndani ya chama au chama kina mfumo usio rasmi wa kubeza mawazo mapya. Kama hali hii ndivyo ilivyo ndani ya chama chetu, kwa vyovyote watu watatafuta majukwaa ya kuibua mawazo mapya na kutoa maoni nje ya majukwaa rasmi ya CHADEMA, kwa kuzingatia wazo jipya huboresha au hupinga wazo la zamani hivyo basi mtoa wazo jipya au maoni ataonekana ni msaliti pamoja na nia yke nzuri kwa chama.
NNE:
Nimesoma hoja za Mwigamba, labda uwe mwendawazimu, au kibaraka wa mfumo ulikosolewa na hoja za Mwigamba ndio utaweza kuona kuwa MWIGAMBA hoja zake hazina mashiko, lakini kiukweli CHADEMA haitakiwi kuzijibu hoja za Mwigamba bali inatakiwa kuzifanyia kazi. Isishie kumchukulia hatua za kinidhamu tu bali pia izifanyie kazi hoja zake, kwani zinaeleweka na kwa vyovyote vile amezitoa kwa lengo la kujenga chama na si vinginevyo.
MUNGU IBARIKI CHADEMA.