With President Kikwete we are not safe!

INFORMANT

Member
Dec 9, 2010
26
0
Hakika, hatuko salama, hatukuwa salama, na hatutakuwa salama.Mizaha mizaha tu, maisha ya watanzania yanapotea hivi hivi tu.

Si mara ya kwanza, nasema na kwa uthabiti kabisa, si mara ya kwanza, tumechoka, enenda zako!!!!

:sad:
 
Kumbe tumeweka more effort kununua mabomu ya machozi tukasahau kuyamatain mabomu makubwa.

Mauaji, mauaji, damu:msela:
 
DR Slaa alisema kurudi kwa kikwete madarakani ni maafa sijui alimaanisha haya tunayoyapata sasa!??
 
imagine leo ingekuwa siku ya uchaguzi mkuu..............!!!!!!
 
Hakika, hatuko salama, hatukuwa salama, na hatutakuwa salama.Mizaha mizaha tu, maisha ya watanzania yanapotea hivi hivi tu.Si mara ya kwanza, nasema na kwa uthabiti kabisa, si mara ya kwanza, tumechoka, enenda zako!!!!:sad:

halafu huyu rais si alikuwa ni mwanajeshi? au ni rais buyu
 
Mi naona hakuna link ya kueleweka kati ya JK na wasaidizi wake ndio maana kila baya linaibuka ktk uongozi wake tuu.
 
Hakika, hatuko salama, hatukuwa salama, na hatutakuwa salama.Mizaha mizaha tu, maisha ya watanzania yanapotea hivi hivi tu.Si mara ya kwanza, nasema na kwa uthabiti kabisa, si mara ya kwanza, tumechoka, enenda zako!!!!:sad:

Bosi sijakupata vizuri, ni kwamba yote hayo yamesemwa na presda Kikwete ama kuna yako umeongeza maana sijakupata sawa sawa before natoa comments zangu.
 
KWANI SISI TUNAPOPIGA MAKELELE KUSEMA kuwa hakuna acting goverment mnadhania tunatania?
tz kila kitu ni hovyo hovyo tu
 
hata mimi nimeongea na jamaa yangu mjeshi kaniamabia kuna hali ya kinyongo miongoni wa wajeshi. hawamtaki shimbo na mwamnyange kwa sababu uteuzi wao ulizingatia uswaiba badala ya weledi. tena kasema kimsingi hao jamaa niliowataja hapo juu hawana sifa kwenye nafasi hizo ila mkuu kawapa kishikaji .
 
Mkuu Mallaba , itakuwa ngumu sana kama teuzi zitafuata mtu anayependwa Jeshini , labda kama mtazamo ndio huo basi katika mabadiliko ya katiba watoe mapendekezo CDF awe anapikiwa kura na jamii ya TPDF - LOL
 
halafu huyu rais si alikuwa ni mwanajeshi? au ni rais buyu

Alikuwa ni mwanajeshi pia amesoma uchumi. Lakini si inaruhusiwa kusahau? hakumbuki mambo hayo tena.

True hii nchi tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu serikali iko likizo ya kijeshi. Lakini kila siku tunasema yote yana mwisho mbona wanazidi kutuonea na mwisho hauonekani? Siko tayari kukubali sababu yoyote ya mlipuko wa mabomu hayo iliyotolewa au itakayotolewa. Hadi sasa sijasikia aliyewajibika/wajibishwa!!!!!!! kana kwamba ni mabanda fulani ya kuku yameungua? This is too much
 
Kipindi cha giza huko ulaya wana historia hukiona kama kipindi kirefu sana, kwangu mimi kipindi cha utawala huu kimekuwa kipindi kirefu sana na cha giza tororo sana. Nawaambia Watanzania kama hatutafanya kitu wakati huu basi wajukuu wetu watakuja kusema kipindi chetu kilikuwa kipindi cha giza. Inakuwaje mambo yanatokea mfululizo namna hii na hakuna hata mtu anayetaka kusimama kuwasema viongozi? Inakuwaje kila mtanzania anaogopa tu? Ni woga gani huu tulionao?
 
Hakika, hatuko salama, hatukuwa salama, na hatutakuwa salama.Mizaha mizaha tu, maisha ya watanzania yanapotea hivi hivi tu.Si mara ya kwanza, nasema na kwa uthabiti kabisa, si mara ya kwanza, tumechoka, enenda zako!!!!:sad:
wangekuwa wanafukuzwa hivyo mbona maisha yangekuwa marahisi sana? ila tupo pamoja ndugu. Hakika hatuko salama
 
na bado mpaka mkome,si mlimchagua wenyewe?

Wenyewe wanaita kwa kishindo na kushangilia wakashangilia kwa nguvu. Mara nyingi huwa nakutana na watu wanalalamika serikali hii mara hili mara lile na yote ni serious issues lakini huwa nauliza mbona yapo miaka nenda rudi na bado hatuwawajibishi? Ndiyo maana JK anasema kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi. We need will power and commitments to overhaul this Government otherwise we are doomed
 
Back
Top Bottom