Wingi wa watia nia ya Ubunge, nini kilicho nyuma ya pazia?

Michael Andrew Jr

JF-Expert Member
Jul 1, 2020
219
665
Wakuu kwema? Hivi mmejiuliza kama mimi huu utitiri wa kila anayejiona anafahamika na watu kutaka kua mbunge umetokana na nini? Waigizaji, waimba muziki, watangazaji na hata wadangaji maarufu nao wanataka kua wabunge. Je ni kweli wanautaka ubunge au wametumwa kwa malengo fulani fulani?

Ikiwa hawa wanasiasa wa kizazi kipya watapewa ridhaa ya kugombea na mwisho kuwa wabunge, vipi kuhusu nafasi ya wakongwe kwenye siasa hususani ndani ya chama tawala? Ni nini ambacho kinapangwa?? Maana haiwezekani kila mtu atake kua mbunge.

Roosevelt aliwahi kusema "kwenye siasa hakuna kitu kinaitwa bahati mbaya". By the way tusubiri tuone
 
Funguka yote kwanza maana inaonesha kuna ulichokiona au kusikia halafu Mimi na wenzangu akina Kajambanani hata hatuujui huo utitiri

Kwahiyo hebu tusaidieni kudondosha walau list ndogo tu tujionee bila kusahau na vyama walivyopitia
 
Funguka yote kwanza maana inaonesha kuna ulichokiona au kusikia

halafu

Mimi na wenzangu akina Kajambanani hata hatuujui huo utitiri

Kwahiyo

hebu tusaidieni kudondosha walau list ndogo tu tujionee bila kusahau na vyama walivyopitia
Ukiangalia kwa makini kulikua na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu na wadau wa maendeleo wa nje ikiwemo USA nk kua demokrasia ndani ya Tanzania imezorota kwa kiasi kikubwa. Na hat uchaguzi wa mwaka huu ulitabiriwa kua wa chama kimoja na vifo kwa vyama vya upinzani.

Kwa trend hii ya vijana na damu mpya kutoka kiwanda cha sanaa, kama vile Dr sheni, Steve Nyerere, babu tale, bonta nk na pia kiwanda cha utangazaji kama vile, James tupa tupa, baruhani muhuza, harris kapiga nk bila kusahau kiwanda cha dini na imani na vingine vingi.

Swali ni je hawa wote wamepata wito kutoka kwa mungu kugombea?? Wana sifa za kuwawakilisha wananchi? Au ndio kukua kwa demokrasia na kuwachallenge wale walioona Tanzania hakuna demokrasia, na uchaguzi ujao utakua igizo? Hapa ndo nataka tushirikiane kudadavua


Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Ukiacha wahamiaji kutoka upinzani, wabunge wanaotetea majimbo yao walio wengi mzee baba hawataki hivyo ili kuua soo wamealikwa wengi kugombea ili akiwakata mikia wakilalamika atawaambia waliochukua fomu walikuwa lets say 12 na wotwe wanastahili je ilikuwa lazima fulani tu ndiye ashinde?
 
Ukiacha wahamiaji kutoka upinzani, wabunge wanaotetea majimbo yao walio wengi mzee baba hawataki hivyo ili kuua soo wamealikwa wengi kugombea ili akiwakata mikia wakilalamika atawaambia waliochukua fomu walikuwa lets say 12 na wotwe wanastahili je ilikuwa lazima fulani tu ndiye ashinde?
Hakika una jicho la kuona mbali... Haiwezekani kila mtu atangaze nia... Kuna namna

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Tumeona ktka majimbo mbalimbali namna wagombea wa Ubunge wanavyomiminika kuchukua form.kiasi imefikia hatua kumekuwa na mistari mirefu ya foleni unaweza dhani ndo wanaenda kupiga kura.

Hii inaashiria nini katika siasa za tanzania? Je kumekuwa na demokrasia pana?

Je watu wamejawa na uzalendo na hamu ya kutumikia watanzania?

Je ubunge unabaki kuwa ni sehemu yenye maslahi mapana sana?

Je ni ule uhakika kuwa kwa sasa ukipitishwa na CCM tayari umekuwa Mbunge?

Tunakolekea tutaona wagombea Ubunge wanakuwa wengi kuliko wapiga kura.
Klinamaaanisha kumekua na siasa za hovyo kuwahi kutokea kwenye histiria ya nchi hiii !!! Mpaka vichaaa wanataka nafasi za uwakilishi
 
Watu wengi tanzania hawana ajira rasmi na uwezo wa kupambana kuingiza kipato kikubwa.
Uwanja wa utafutaji kiasi cha kufikia level ya kuwa milionea tanzania ni mdogo sana.
Watanzania wengi wanapenda maisha rahisi na sifa kwenye jamii, kwenyr ubunge kuna hela ya bure na sifa za bure pia.
Elimu duni itolewayo na taasisi zetu za elimu kiasi wasomi wengi wanashindwa kuwa wabunifu na kujitengenezea kupato kikubwa kupitia ajira zao na kutengeneza ajira pia wanakimbilia kwenye siasa.
CCM ni kubwa kuliko Tanzania, ukiwa kiongozi kupitia CCM basi ni Visa tayari ya kufanya mambo yako na hata uchafu wako bado ukakingiwa kifua.
Watanzania wengi ni watoto wa mama wamezoea maisha laini laini yasiyo na mikiki mikiki hali hii imesababisha watu wengi wakimbilie kila penye urahisi na kuogopa mambo magumu..

Jamii na Viongozi watambue Taifa linajengwa na vijana wenye nguvu na maarifa ya kutosha, Taifa linajengwa kwa kufanya mambo magumu na sio vitu rahisi rahisi tu..tukiiendekeza jamii hasa vijana na kuwafanya mbogamboga tutambue tunaangamiza taifa...Vijana na watu ni nguvu kazi na rasilimali pia kama tunaitumia vibaya na jamii yote inafanya siasa sasa tambueni tunaangamia.
 
Ubunge Ndio ustaa Ndo utajiri wa haraka Na umaarufu,Badala ya kuwa utumishi wa watu,yaani tz ukiwa mwanasiasa ndo unakuwa maarufu haraka na kuogopewa na wanyonge wenzio
 
Wanatafuta ajira hao hakuna kingine hata kama wana ajira tayari wanaangalia inayolipa zaidi wapo kimaslahi kuliko kitu kingine chochote...
 
Chandarua chenye matobo hukimbiliwa na mbu wa kila aina, wanaojifunza kuruka, wazee, wenye mimba hata wanaotambaa wakijua ukikifikia lazima utaweza kuingia kitandani.

Kauli za nyuma zinazowataka wasimamizi wasiwatangaze wapinzani wanaoshinda uchaguzi na zile za mwenye dola hawezi kushindwa ndizo zimewafanya hata wasiojua siasa kugombea ubunge kupitia CCM wakijua chama kikiwapitisha basi wao ni tayari wabunge!

Hawahitaji kupata kura nyingi za ushindi kwani kuna lile bao la Nape la mkono wa mungu, hapa tusichanganye na (Mungu) kwani huyu si mtenda maovu.
 
Sisi tukiingia madaramani kitu cha mwanza mbunge lazima awe na taaluma flani....haiwezekani tupeleke mipasho bungeni halafu tutegemee kuwa na katiba imara inayolinda maslahi ya taifa...emu wakasome huko ebooo
 
Wakuu kwema? Hivi mmejiuliza kama mimi huu utitiri wa kila anayejiona anafahamika na watu kutaka kua mbunge umetokana na nini? Waigizaji, waimba muziki, watangazaji na hata wadangaji maarufu nao wanataka kua wabunge!! Je ni kweli wanautaka ubunge au wametumwa kwa malengo fulani fulani??

Ikiwa hawa wanasiasa wa kizazi kipya watapewa ridhaa ya kugombea na mwisho kuwa wabunge, vipi kuhusu nafasi ya wakongwe kwenye siasa hususani ndani ya chama tawala? Ni nini ambacho kinapangwa?? Maana haiwezekani kila mtu atake kua mbunge...

Roosevelt aliwahi kusema "kwenye siasa hakuna kitu kinaitwa bahati mbaya". By the way tusubiri tuone

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Demokarasia
 
Watu wanatafuta uteuzi Kwa mkuu, wameambiwa waspojiunga huko hakuna uteuzi tena
Haswaaaa!Nimebahatika uongea na watia nia vijana wameeleza ukweli ya kuwa wanajua kupita ni vigumu lakini wanatengeneza CV na Rais ana nafasi nyingi za uteuzi.Wengi wametaja wenzao amabo wamelamba uteuzi kutokana na kuingia 2015.Mmoja aliniambaia "Hivi ukimchachafya mtu kama Pofesa uchaguzi ukiisha hata ajira unaweza kupata"
 
Hili suala Wagombea wengi kupita maelezo tunaichukulia poa sana.

Mimi najaribu kuingalia kwa jicho la tatu.

CCM wanajua fika hawawezi kushinda uchaguzi huru na wa haki. Polepole alishasema maneno haya wakati huo akiwa na akili timamu.

Sasa wamebuni hili la kuja na wagombea wengi. Kwanza ionekana wana mvuto kuliko wapinzani na pili vijana wasigombee upande wa pili.

Baada ya kuchakachua matokeo kwenye uchaguzi, wata justify ushindi hewa kwa idadi kubwa ya watia nia eti wanapendwa. Wamelenga majimbo maalum. Kwa Lema, Msigwa, Mdee nk.

Kitu vijana wengi hawajui ni kwamba wanatumiwa tu. Pengine hawajali sana ilimradi wamepata pesa.

Unawezaje kueleza ugombea wa Steve Nyerere, Mpoki, Dokii, Amberluti if all the people?

Muda utaongea!
 
Hili suala Wagombea wengi kupita maelezo tunaichukulia poa sana.

Mimi najaribu kuingalia kwa jicho la tatu.

CCM wanajua fika hawawezi kushinda uchaguzi huru na wa haki. Polepole alishasema maneno haya wakati huo akiwa na akili timamu.

Sasa wamebuni hili la kuja na wagombea wengi. Kwanza ionekana wana mvuto kuliko wapinzani na pili vijana wasigombee upande wa pili.

Baada ya kuchakachua matokeo kwenye uchaguzi, wata justify ushindi hewa kwa idadi kubwa ya watia nia eti wanapendwa. Wamelenga majimbo maalum. Kwa Lema, Msigwa, Mdee nk.

Kitu vijana wengi hawajui ni kwamba wanatumiwa tu. Pengine hawajali sana ilimradi wamepata pesa.

Unawezaje kueleza ugombea wa Steve Nyerere, Mpoki, Dokii, Amberluti if all the people?

Muda utaongea!
CCM itapata pigo kuuuuubwa sana pigo moja tu pigo takatifu pigo lililonyooka kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Watajimaliza wenyewe
tapatalk_1575089448362.jpg
 
Back
Top Bottom