MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Tayari vyama vingi kama si vyote vimefungua pazia kwa watia nia kuelekea ucjaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kumekuwa na pilikapilika za huku na kule kwa wanachama wa vyama vya siasa kutia nia ya kugombea ubunge.
Kwenye makundi sogozi kwa sasa kumejaa picha za watia nia wakijitangaza kuwa wako tayari kuwatumikia wananchi.
Cha kushangaza ni kuwa hata wasiotarajiwa kuwa wangeweza kutia nia sasa wefanya hivyo.
Wengine tunawajua uwezo wao wa kiuongozi na kiutendaji kwani tumesoma nao shuleni na vyuoni.
Ni watu ambao hata uwezo wa kujijitea wao wenyewe hawana mpaka watetewe na wenzao. Sasa mtu ambae hawezi kujisemea na kujitetea mwenyewe atamtetea nani?
Ubunge umerahosishwa sana kiasi kwamba kila mmoja anaona kama anatosha kuwa mwakilishi jimboni.
Itafika hatua huko mbele tunaweza kuwa na wabunge wasiojiweza kiasi kwamba mbunge akamaliza miaka mitano bila kuchangia chochote bungeni.
Ni wakati wa chama kuweka vigezo muhimu na vigumu kwa watia nia ili kuwa na uhakika na na hao watia nia ambao ni wabunge watarajiwa.