Wimbo Wangu Maalumu kwaajili ya John Pombe Magufuli unapatikana YouTube kwenye channel yangu HAITHAM KIM

Komaa tu! Kuna yule bwana aliimba Kama sio juhudi zako na Uhuru tungepata wapi! Ohoo Kama sio.

Aliumba Kama masikhaa tu lakini ukawa ndo hit song ya maombolezo na Hadi leo unafit kila mahali na naamini hata Nyerere huko kaburini akiusikia anafarijika na kupiga chafya kwa furaha.

Imba tu mkuu.
 
Watanzania Tunakulilia Baba 😭

@haithamkim X @wyse_tz
Official Video is out ‼️

Ahsante sana ndugu yetu, sote tunalia nawe kwa kupoteza kiongozi shupavu katika bara la Afrika, Afrika nzima wanamlilia Magufuli kwa uzalendo wake na uchapakazi
 
Watanzania Tunakulilia Baba 😭

@haithamkim X @wyse_tz
Official Video is out ‼️

Dr Magufuli wewe ulikua zaidi ya Rais zaidi ya Mzazi zaidi ya Kiongozi, Ulitupa ujasiri tulipokua na hofu, Ulitutia matumaini tulipokata tamaa, ulituheshimisha tulipodharauliwa, Ulitupenda pale tulipochukiwa, Ulitufundisha namna bora ya kujipatia maendeleo kwa kutumia hata kipato kidogo kidogo tulichokua nacho, Ulitutia moyo pale tulipoona hatuwezi chochote, kwanini umewahi mapema tukiwa bado tunakuhitaji nimeamini vizuri havidumu tangulia baba hakika wewe ni shujaa Ee Mwenyezi Mungu wa rehema tunakuomba umpokee Baba yetu katika makao mema ya milele😭😭😭😭😭 Pia mpe nguvu Mama yetu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan tunaimani atatuvusha pia ninaimani kuwa Mungu una mapenzi mema na nchi yetu ya Tanzania, Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.
 
Ila hayati alituacha watu wa mtandaoni tukiwa na mazingira magumu sana,hebu fikiria eti mpaka YouTube channels & blogs ilitakiwa tuzilipie million 1@year

Na kwa sasa alikuwa ametoa maagizo kwa tcra waangalie namna ya kuibana WhatsApp,yaani huyu kwa hatua alizokuwa anakwenda kuzichukua imebidi tu malaika jabir atumwe kumuondoa
 
Back
Top Bottom