MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Huu wimbo ni mzuri na nimeusikiliza japo Diamond Platnumz kaimba sehemu ndogo sana peke yake, ila sehemu kubwa kafanya Back-Vocals. Mwanzo mzuri kwake na natumai atatumia nafasi hii kujinoa vizuri maana Alicia Keys na mume wake ni wataalamu na walimu wakubwa wa muziki. Ndugu Diamond Platnumz ukumbuke kwamba huyu dada Alicia Keys alishawahi kushinda shindano kubwa la muziki The Voice America akiwa na mwanafunzi wake Chris Blue huku akishindana na wasanii wenzake nguli kama Adam Lavine, Blake Shelton na Miley Cyrus.
Sasa kama utatumia huu mwanya kujifunza zaidi naamini hii ni nafasi yako ya kipekee kabisa kujifunza kutoka kwa huyo dada na utajifunza mengi mno. Binafsi naamini Diamond Platnumz ni mtu ambaye anapenda kujifunza hivyo utapata ujuzi mwingine mkubwa. Kiufupi hii Album ni nzuri sana japo hujasikika sehemu kubwa sana kwenye wimbo, usikate tamaa tambua kwamba hii kwako ni nafasi ya kujifunza zaidi na kufahamiana na watu wapya.
Hii Album ni kali sanaaaaaa nzuri hivyo naamini wengi wataisikiliza na watapenda kufahamiana na wewe, hata kufanya kazi na wewe. Wimbo "Wasted Energy" ushafika Rap Genius na mistari ya kiswahili ishatafsiriwa kwa lugha ya kiingereza. Nimefuatilia mtandaoni watu wameupenda sana wimbo na wametaka kujua nini kilichoimbwa na Diamond Platnumz: Hili ni jambo jema sana. Kaza buti ndugu yangu na endelea kutuwakilisha vyema. Nimeweka wimbo wenyewe na baadhi ya nyimbo za kwenye album..

Attachments
-
Wasted_EnergyFt_Diamond_Platinumz@soundcitieee_Alicia_keys@soundcitieee.mp37.9 MB · Views: 7
-
Authors_of_Forever@soundcitieee_Alicia_keys@soundcitieee.mp36.6 MB · Views: 5
-
Good Job[@soundcitieee]_ Alicia keys[@soundcitieee].mp36.4 MB · Views: 4
-
Time Machine[@soundcitieee]_ Alicia keys[@soundcitieee].mp38 MB · Views: 6