Will the real Paul Makonda please stand up?

Nyani ngabu assume ww ndio huyo Paulo makonda wanaedai vyeti vyake vinatumika na mtu mwingine, ungejitokeza hadharani ukizingatia uhalisia wa viongozi wa nchi za dunia ya tatu?
 

Ok, sawa tuendelee.

Nianze na suala la Gwajima.

Hakuna kitu kilicho personal. Simjui na hanijui kabisa. Na kusema ukweli nimemjulia humu humu JF kipindi kile cha Dkt. Slaa kuondoka CHADEMA. Hizo kejeli ziko based na kile ninachokijua juu yake hususan maneno yake mwenyewe...sikuamini masikio yangu alivyomtukana kadinali Pengo.

Na nadhani umenisoma vibaya. Mimi si dismiss kabisa tuhuma dhidi ya Makonda.

Lakini nachosema ni kwamba, kama Makonda mwenyewe anasuasua kuzijibu hizo tuhuma kwa nini basi [1] wasimburute mahakamani ambako huko atalazimishwa kuzijibu na [2] kwa nini yeye huyo Gwajima asitusaidie kwa kutuonyesha huo ushahidi aliosema anao?

Now tell me Bossman, what is so unreasonable about that?

All I want is to get to the bottom of it, one way or the other.
 


Kama unakubali kumburuta mahakamani ni second or third option sina shida
mradi tukubaliane kuna option ya kwanza ambayo ni yeye Makonda kuja clean
au ya serikali kutoa tamko na msimamo wa serikali....na kutueleza ukweli ni upi..

Binafsi naona Gwajima ni very very irrelevant kwenye hii issue ....
Wapo waliosema vyuo alivyosoma ndo vijitokeze na kuonesha vyeti alivyo wasilisha
naonna hiyo ni better option...

Lakini kwa nini yeye hajibu au kulazimishwa kujibu? hilo tu huoni kuwa ni ishara ya ukweli wa tuhuma?
Au kwa nini Magufuli yuko quick kufukuza na kutolea matamko mambo mbalimbali lakini hili yuko kiimya?
 
Kama unakubali kumburuta mahakamani ni second or third option sina shida
mradi tukubaliane kuna option ya kwanza ambayo ni yeye Makonda kuja clean
au ya serikali kutoa tamko na msimamo wa serikali....na kutueleza ukweli ni upi..

Ni kweli. Yeye Makonda ndo anaweza kufunga huu mjadala. Hilo siwezi kabisa kukataa.

Binafsi naona Gwajima ni very very irrelevant kwenye hii issue ....
Wapo waliosema vyuo alivyosoma ndo vijitokeze na kuonesha vyeti alivyo wasilisha
naonna hiyo ni better option...

Kwangu ni very relevant maana kasema anao ushahidi wa kilicho kiini katika tuhuma nzima.

Kwa sababu hiyo naamini he can do us all a big favor kwa kutuonyesha huo ushahidi alonao.

Kukiwa na kesi mahakamani yeye ndo atakuwa ni mmoja wa key witnesses. Naamini hivyo ingawa mimi siyo kaka msomi.

Lakini kwa nini yeye hajibu au kulazimishwa kujibu? hilo tu huoni kuwa ni ishara ya ukweli wa tuhuma?
Au kwa nini Magufuli yuko quick kufukuza na kutolea matamko mambo mbalimbali lakini hili yuko kiimya?

Hilo la yeye na Magufuli wake kuwa kimya hakika linatia shaka. Hapo napo siwezi kukataa.
 


Na hili la watuhumiwa wa madawa kumnunulia magari je umelisikia?
umelionaje? hadi card za magari zimewekwa online
na picha akitumia hayo magari pia
 
Tatizo lako mkuu una haraka mno. Mambo ya koromije huwa yanaenda polepole. Ukweli utajulikana tu na kuna mtu atakuja kuaibika hasa. Kila kitu kipo na nyaraka zote zipo na wahusika wote wapo.
 
Well, hata akili ya kawaida inahoji pia kuwa ni kweli huyo mtu yupo au hayupo?
Kaka, hakuna Paul Makonda halisi au feki....

Hapa kilichoibiwa na majina ya mwanzo...Paulo Christian Muyenge.
Huyo Muyenge ndio halisi sasa, ila Daud Albet Bashite, aliapa mahakamani, kuondoa Muyenge...iwe Makonda.

Pia posibility zilizopo (sina hakika), huu mkataba wa kuuziana cheti, ulifanywa baina ya Albert na Dada wa Paul Christian Muyenge.

So, yawezekana hata Paul halisi, kajua kipindi hiki kuwa cheti changu kiliwahi kutumika, na wakamuwahi kumzima.

Ila huyu Muyenge inasemekana yuko Tabora
 
Na hili la watuhumiwa wa madawa kumnunulia magari je umelisikia?
umelionaje? hadi card za magari zimewekwa online
na picha akitumia hayo magari pia

Yeah, hilo nalo nimeliona.

Ila sina taarifa za kutosha kuweza kulitolea maoni kikamilifu maana sasa hivi kuna hali ya chuki na visasi na kila aina ya mazagazaga.

Inahitaji utulivu wa akili kidogo na si kukurupuka tu.

Ila nakubali kuwa vitu havijakaa sawa kabisa na huyo bwana.

Anaonekana ana utoto utoto mwingine na ulimbukeni na hana kabisa busara.

Anaonekana ni mtu wa kujipendekeza sana.

Rejea tu jinsi yeye na Magufuli walivyomtendea yule mkurugenzi wa jiji Bw. Kabwe ile mwaka jana.

That was so beneath the offices they hold.
 
Yaani hayo yote hata mimi nimejiuliza pasipo na majibu.
Wewe ni kilaza sana hakuna mtu anaitwa Paul makonda.Paskali amekujibu vizuri Ila umepotezea majibu yake.yupo Paul christian M.
 
Mtu ambaye aliyetoa Cheti kwa Daudi Albert Bashite(Alias Paul C. Makonda) anaitwa Paul Christian Muyenge sasa Bwana Daudi Bashite Kuogopa ufanano wa Majina akaamua abadilishe Muyenge iwe Makonda na hilo Makonda ni kutokana na Kazi ya Ukonda aliyoifanya enzi za kutafuta maisha.
 
Unahongwa na wauza madawa ya kulevya kuja kumchafua shujaa wetu wa Dar??

Kila siku makonda makonda who are you??
Hivi atakuwa ni shujaa kweli? Nadhani angekuwa shujaa kama angethubutu kutoa gamba lake halisi!
 
Jiulize kwa nini hawajafanya hivyo, au zua uzushi mwingine.

Wanaotaka kujua nani ni nani Tanzania waende RITA

Wanaotakakuona cheti cha elimu ya mtu waende shule/chuo alikosomea.

Mpumbavu na lofa hurukia mambo bila kufikiri.
 
Hoja ya kwamba Paul halisi atakuwa anaogopa kujitokeza haina mashiko.

Kama wameweza kuweka mpaka kadi za magari yanayodaiwa ya Makonda wanashindwaje kumuibua mtu huyo hata picha tu?
 

Mifumo yetu ya sheria inafahamika kuwa kuna mapungufu mengi sana......hilo liko wazi kwa kuwa kwa namna moja au nyingine tulishawahi kuathiriwa na ukiritimba huo......

Lakini hilo halisababishi watu wasitafute haki kwenye vyombo vya sheria....na watu wanapata stahiki zao kwa mujibu wa sheria.......

Tulichokuwa tunakitaka ili kukata mzizi wa fitina....hilo shauri lifikishwe polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Makonda aliyeghushi vyeti.....( kama kweli)......

Naamini ushahidi upo wa kutosha wa kumtia mtuhumiwa hatiani na hili suala likafikia mwisho......

Mbona mashauri mengi tu....wapinzani wanayapeleka mahakamani na kupata haki.....!!!
 
The Real Paul Makonda ndiye huyo Daudi Bashite.

Daudi Bashite( kwa masimulizi ya Gwajima) alisaidiwa na mpenzi wake ambaye alimuahidi kuwa wataoana baadae (Hilo halikutimia/ Daudi hakutimiza ahadi aliyompa Dada huyo) kupata kivuli cha cheti cha form 4 cha Paul M. Daudi alitumia kivuli hicho kuombea masomo. Paul M mwenyewe inawezekana hakujua kabisa kwamba Cheti chake kilitolewa kivuli na huyo ndugu yake wa kike.

Ili kuona utata na maelezo ya kina angalia hii

 
Jiulize kwa nini hawajafanya hivyo, au zua uzushi mwingine.

Wanaotaka kujua nani ni nani Tanzania waende RITA

Wanaotakakuona cheti cha elimu ya mtu waende shule/chuo alikosomea.

Mpumbavu na lofa hurukia mambo bila kufikiri.

Walituambiaga Lowasa ni fisadi na ushahidi wanao.....leo hii wanatuambia kuwa mwenye ushahidi aende polisi........

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni......
 
Hoja ya kwamba Paul halisi atakuwa anaogopa kujitokeza haina mashiko.

Kama wameweza kuweka mpaka kadi za magari yanayodaiwa ya Makonda wanashindwaje kumuibua mtu huyo hata picha tu?

Hata Le Mutuz walimwibia passport yake wakaipiga picha wakairusha mtandaoniπŸ˜€πŸ˜€.

Kweli watu wana hila za fisi, si mchezo.

Nilicheka sana.
 
Makonda ana kinga ya Mkulu inayompa nguvu kubwa sana, ndiyo maana watu wanajiuliza kabla ya kumburuza mahakamani. Makonda na Guardian Angel wake wana nguvu ya ajabu. Makonda amelivimbia Bunge na mahakama muda si mrefu, na bado hakuna kilichotokea, nani leo ajitoe muhanga kupambana naye? Vyombo vyote vya kupambana naye kuhusu suala lake, viko chini 'yao'.

Swali la msingi ni; Kama kweli Makonda anasingiziwa ya Bashite, kwanini asiwashtaki hao kina Gwajima kwa kumchafua??
 
Ninachoshangaa mimi ni kitendo cha eti 'Mange' anaweza kupata copy ya kadi ya gari na kuipost mtandaini,,,, lakini eti anacho cheti cha 0 leo wiki ya tatu hajakitoa..... na kwa tunavyomfahamu mange alivyokuwa mmbea wa dunia, awe na cheti asikitume mtandaoni hadi leo, sio yeye. Hii kitu ni kelele tu, no one with undeniable evidence.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
"Ila huko nyuma kuna mtu aliitwa Daudi Albert Bashite, huyu alizaliwa Kolomije, akasoma Kolomije na kumalizia Nyanza. Akafeli la saba, lakini akafanya maarifa akasoma Pamba sekondari ya serekali, alipomaliza form IV alipata zero, na hadithi ya Daudi Bashite ikaishia hapo."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…