Wilaya ya Temeke kupewa shilingi bilioni 3.14 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
ASANTE MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA KURIDHIA WILAYA YA TEMEKE KUPATA SHILINGI BILIONI 3.14 KWA UJENZI WA MADARASA 157 KATIKA SHULE 25🇹🇿

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo leo tarehe 03 Januari, 2022 amefanya Uzinduzi wa makabidhiano ya vyumba vya madarasa vilivyogharimu Bilioni 3.14 hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Dovya

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyumba hivyo DC Jokate amesema tayari vyumba vyote 157 vya madarasa ya sekondari katika Shule 25 vimekamilika vikiwa na meza na viti kwa wanafunzi kukalia

DC Jokate amemshukuru Mhe, Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya ya Temeke kupewa shilingi bilioni 3.14 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya fedha za mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 kwa wilaya ya Temeke

“Pamoja na mambo mengine, madarasa haya yataondoa adha ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kuripoti kwa awamu na msongamano wa wanafunzi madarasani lakini pia itaboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia na matokeo yake ni kuboreka kwa ufaulu na kujikinga kikamilifu na mlipuko wa ugonjwa wa corona maana madarasa haya yatapunguza msongamano Madarasani" - Amesema Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Jokate Mwegelo

Screenshot_20220103-123551_1.jpg
 
Back
Top Bottom