Wikileaks yajibu kitendawili cha kwanini Muammar Gaddafi aling'olewa madarakadi na hatimae kuuawa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Sababu hasa za kuwindwa, kungolewa madarakani na hatimae kuuawa kwa Muammar Gaddafi zawekwa wazi kupitia mtandao wa Wikileaks

IMG_20180323_164236.jpg

IMG_20180323_164236.jpg
 
Wazungu walimpigia mahesabu siku nyingi sana na hilo lilikuwa kamilisho tu
Mwaka 1999-2002 Gordon Brown aliuza dhahabu za kwenye hazina ya UK na walilalamika sana wasiokuwa wanajua kinachoendelea.
Hapo utajua hawa jamaa ni wabaya na waroho wa mali
Mnapoambiwa serikali haina dini ina maana kubwa sana
 
Mtoa mada jenga uwezo wa kudadavua unapoweka thread hii n habar au ripoti
Mtoa mada amenukuu kutoka wikileaks sasa wewe kazi yako ni kufanya utafiti zaidi. Hivi ni sawa ndani ya karne hii nyama ununuliwe, upikiwe, ulishwe na bado unataka huyo anayekulisha aisukume kwenda tumboni????
 
Aisee US na washirika wake ni mashetani haya sasa democrasi waliyoipeleka Libya ona inavowataabisha walibya bora angebaki Gadaff misha yalikua murua almost kila kitu kilikua rahisi kukipata Libya....
 
Kiukwel nina kadegree kangu tena kile chuo pendwa but lugha ii lugha ii narudia tena kwa harufi KUBWA LUGHA II YA UZUNGUNI NIMETOKEA KUTOIELEWA MAELEZO YAKIWA MAREFU
 
Aiseee. Mfaransa alihakikisha anaendelea kuyakamua makoloni yake mpaka mwisho wa Dunia.
Chezea wanawake wa kizungu hata uwale 0714...
Ila usichezee hela, mafuta, gold, almasi, madini yoyote duniani, hata kama ni yako, mzungu hakuachi salama...
Mashetwani kabisa wale...
 
Aisee US na washirika wake ni mashetani haya sasa democrasi waliyoipeleka Libya ona inavowataabisha walibya bora angebaki Gadaff misha yalikua murua almost kila kitu kilikua rahisi kukipata Libya....
Kinachoimaliza libya sio demokrasia ila kipindi cha mpito baada ya VITA mbona misri na tunisia walipindua nchi zao wameweka demokrasia ila hakuna makundi ya kigaidi kma libya???

Kama gadaffi angeondoka kwa amani kusingekuwepo na ISIS wala Al qaeda ama makundi yanayovuruga nchi so wakulaumiwa ni gadaffi sio marekani

Kingine tusilaumu wazungu ilihali waafrika wenyewe tunawaachia mashimo..... Kama gadaffi asingekuwa dikteta wangepata sababu ya kumtoa?? Hivi leo akitolewa museveni au kabila na wazungu mtasema wazungu wabaya?? Wakati chanzo ni udikteta wao???

Hicho ni kipindi cha mpito tuu ambacho hta uganda ilipitia baada ya kumtoa idd amin ssa je na wao watulaumu kwamba baada ya nyerere kumtoa amin uganda ilikuwa ina vikundi vya waasi zaidi ya 100 hivyo watanzania tulifanya kosa kumtoa idd amin? Does it make sense?? Mobutu alikuwa dikteta haswaa ila baada ya kutolewa congo ina waasi kibao makundi zaidi ya 200 mashariki ya congo pekee je walaumu kutolewa kwa mobutu na demokrasia kuletwa kisa tu kipindi cha mpito baada ya vita?????

Tusichanganye mambo madhara ya vita hayahusiani na sababu za kumtoa dikteta hta mobutu angeondoka kwa amani kma zimbabwe mbona hatuoni makundi ya waasi?? Afrika kusini alitoka kwa amani hakuna waasi ila mugabe angepigana vita nako nchi ingesambaratika ssa utalaumu wazungu hapo???
 
Back
Top Bottom