Fikra za Sankara, Magufuli, Nyerere, Malema na Gadafi zaibukia kwa Ibrahim Traore

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,034
Vision of the Vision.
Mitazamo chanya juu ya Afrika.

Captein Ibrahim Traore Rais wa Burkinafaso au Bukinabe ni kiongozi ambae kajitofautisha sana na viongozi wa kiafrika ambao kazi yao kubwa ni kuzunguka na madege dunia nzima huku wakienda kuombomba fedha wakati kwao wameacha utajiri mkubwa sana wa mafuta, dhahabu, Almasi, bandari, ardhi yenye rutba, inauma.
Kitendo cha viongozi wengi kushindwa kubadilisha rasilimali walizokalia na hatimae kuzigawa kwa wafanyabiashara wazungu kwa jina zuri la wawekezaji ni ufinyu wa akili.

Kwa mfano hauwezi kwenda kuita watu wakuendeshee bandari ati kisa hauna ufanisi miaka 60 ya uhuru bado hauna ufanisi wa kuendesha hata bandari. Fikra za viongozi wa Afrika ni finyu sana sana na wao ndio huingia mikataba mibovu ya kugawa rasilimali zao kwa kigezo cha wawekezaji inasikitisha sana.

Wale mnaowaita wawekezaji kimsingi ni wafanyabiashara maana wao hutafuta faida kupitia rasilimali zenu na mikopo huchukua kwa kutumia dhamana ya rasilimali zenu inauma sana sana. Tuwapongeze na kuwakumbuka wanaafrika waliokua na mtazamo wa kiafrika hasa wa kulinda rasilimali za bara la afrika
Thomas Sankara, John Magufuli, Patrice Lumumba, Gaddafi, Julius Malema, Julius Nyerere na wengine wengi na kwa sasa Ibrahim Traore.
 
Tuseme waafrika tulibugi kuwafukuza wakoloni waliokuwa wakitujengea nchi wakituletea maendeleo,then tunahitaji Tena wawekezaji.
Mwekezaji ni mwizi anachuma faida ajengi Africa anaodoka anarudi kwao, mkoloni alikuja kustay.
Ni tamaa tu za wapigania Uhuru wao ndio wanufaika wa uhuru ikiwemo kizazi Chao kama walamba asali,huku mamilioni ya waafrika ni dhooufu hali.
Leo kijana aliyesoma na asiyesoma wote wanaendesha bodaboda.
 
Hata idd amin alivyoingia madarakan alikuwa na fiksa hizo hizo, tena yeye alifukuza wafanyabiashara wote wagen kwa kuwanyonya waganda, kilichotokea sasa
Wahindi waliofukuzwa Uganda na walioporwa Mali zao na Nyerere wengi walienda USA, Canada na UK wakiwa mikono mitupu masikini kabisa lakini walipofika huko Leo ni miongoni mwa matajiri wakubwa hadi wanashukuru kufukuzwa Afrika ikawapa speed ya kupambana zaid.
Leo nyumba zao tumeshindwa kuziendeleza.
Yale maghofu pale fire Yana fanya Nini pale eneo potential Kama lile zaidi ya NHC kulamba Kodi kwa nyumba zisizo zao.
Kwann wasipewe wawekezaji wazidevelop.
 
Vita mpya ya Mrusi na Mabeberu ikipiganwa ndani ya Ardhi ya Africa, Wagner group wapo central Africa,wapo Niger,sema Congo jamaa ni upande wa mabeberu angewapeleka kule wakamfurushe tall haachi kuiba Congo.
 
Vision of the Vision.
Mitazamo chanya juu ya Afrika.

Captein Ibrahim Traore Rais wa Burkinafaso au Bukinabe ni kiongozi ambae kajitofautisha sana na viongozi wa kiafrika ambao kazi yao kubwa ni kuzunguka na madege dunia nzima huku wakienda kuombomba fedha wakati kwao wameacha utajiri mkubwa sana wa mafuta, dhahabu, Almasi, bandari, ardhi yenye rutba, inauma.
Kitendo cha viongozi wengi kushindwa kubadilisha rasilimali walizokalia na hatimae kuzigawa kwa wafanyabiashara wazungu kwa jina zuri la wawekezaji ni ufinyu wa akili.

Kwa mfano hauwezi kwenda kuita watu wakuendeshee bandari ati kisa hauna ufanisi miaka 60 ya uhuru bado hauna ufanisi wa kuendesha hata bandari. Fikra za viongozi wa Afrika ni finyu sana sana na wao ndio huingia mikataba mibovu ya kugawa rasilimali zao kwa kigezo cha wawekezaji inasikitisha sana.

Wale mnaowaita wawekezaji kimsingi ni wafanyabiashara maana wao hutafuta faida kupitia rasilimali zenu na mikopo huchukua kwa kutumia dhamana ya rasilimali zenu inauma sana sana. Tuwapongeze na kuwakumbuka wanaafrika waliokua na mtazamo wa kiafrika hasa wa kulinda rasilimali za bara la afrika
Thomas Sankara, John Magufuli, Patrice Lumumba, Gaddafi, Julius Malema, Julius Nyerere na wengine wengi na kwa sasa Ibrahim Traore.
Haya mawazo ni mazuri kama viongozi Africa watakubali wote kuwatosa wadhungu wasaka malighafi- raw materials za Africa. Nakwambia viongozi wetu Africa wakikomaa, haitapita miaka 5 weupe watakuja kwa adabu Africa tufanye biashaha za win win situation.

Nachofikiria, hata viwanda vya raw materials inayopatikana Africa , waweke msimamo hao weupe waje wavijenge huku Africa ili wakifanya mchezo mchafu, tunawambia Chonde, Chonde....STOP .
 
Umelenga zaidi kukandia kikundi cha watu kuliko kuelezea hizo fikra za huyo ibra traore na matokeo yake pamoja na hao wengine.
 
Hakika baada ya kifo cha Gadafi tulibaki wanyonge sana katika ulimwengu usio na matumaini. Hata maduro na museveni walikuwa na cheche lakini sio zile za kutupa mwangaza. Wengi tulisalia kuamini katika mamlaka kuu ya kim jong un kiongozi mkuu!
Hakika naikumbuka ile kauli iliyotolewa wakati wa msiba wa Gadafi na Hugo Teves wakati ule ambaye naye alituacha alipo sema " utawala wa ma yuen king kamwe hauwezi kuitawala dunia"
Mzalendo mpya amechipukia bulkinafaso!!!!
 
Back
Top Bottom