Italia yazilaumu nchi za Magharibi kwa kuivamia kijeshi Libya wakati wa Gaddafi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Italia yazilaumu nchi za Magharibi kwa kuivamia kijeshi Libya wakati wa Gaddafi

Waziri wa Mambo ya Nje ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa Italia amezilaumu nchi za Magharibi kwa kuivamia kijeshi Libya wakati wa harakati za wananchi za kuipindua serikali ya kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi lakini ameshindwa kulaumu uharibifu mkubwa uliofanywa na madola hayo ya Magharibi katika uvamizi wao huo.

Kwa mujibu wa Russia Today, Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu wa Itali, Antonio Tajani, amesema kuwa, nchi za Magharibi zilifanya makosa makubwa kwa kuingilia kijeshi katika harakati za wananchi wa Libya za kumpindua Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Amedai kuwa, kifo cha Gaddafi kilisababisha machafuko na migogoro ya miaka mingi kwa Libya lakini ameshindwa kutamka sababu hasa ya machafuko na migogoro hiyo kwamba ni madola hayo vamizi ya Magharibi yaliyoongozwa na Marekani ambayo baada ya kufanya uharibifu mkubwa yaliacha silaha zikiwa zimeenea mikononi mwa makundi chungu nzima hasimu nchini Libya.

Madai haya ya Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu wa Italia yalitolewa wakati nchi hiyo ya Ulaya nayo inashutumiwa kwa kuhusika katika vurugu na machafuko ya kisiasa tangu wakati wa mapinduzi ya 2011 ya wananchi wa Libya ambayo yalisababisha kupinduliwa kwa serikali ya muda mrefu ya Muammar Gaddafi. Marekani iliongoza madola mengine ya Ulaya Magharibi chini ya mwavuli wa Jeshi la Nchi za Magharibi NATO kuivamia kijeshi Libya, kufanya mashambulio mazito ya kiholole yaliyolenga moja kwa moja miundombinu ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na baadaye kuacha silaha zikiwa zimesambaa ovyo mikononi mwa makundi hasimu.

Tangu wakati huo hadi hivi sasa Libya haijawahi kuwa na utulivu wa kuaminika. Kuanzia mwaka 2014 nchi hiyo iliingia kwenye mzozo mkubwa zaidi wa kutawaliwa na serikali mbili na mabunge mawili. Ni kipindi hicho pia ndipo yalipotokea mapigano makali baina ya pande mbili kwa ajili ya kugombania mji mkuu Tripoli. Hata hivyo utulivu wa kiasi fulani ulianza kushuhudiwa nchini humo kuanzia mwaka 2020.

4c3o264d3c76892ciik_1200C675.jpg
 
Italy iache unafiki na kuwatonesha waafrika kidonda, ilikua wapi wakati Libya inavamiwa kwann haikupiga kura za veto kupinga uvamizi wa NATO Libya.
 
Italy iache unafiki na kuwatonesha waafrika kidonda, ilikua wapi wakati Libya inavamiwa kwann haikupiga kura za veto kupinga uvamizi wa NATO Libya.
Nadhani utawala wa chama kingine,tawala zinatofautiana ingekuwa USA tungesema hivyo sabb sera zao mambo ya nje haibadiriki sn hata iwe chama tofauti
 
Back
Top Bottom